Tafuta

Papa kwa Makardinali wapya:Jenga umoja na kuacha ushindani!

Mara nyingi sana mambo ya pembeni huchukua nafasi ya yale ambayo ni muhimu,mambo ya nje hushinda kile ambacho ni muhimu sana tunaingia kwenye shughuli ambazo tunaziona kuwa za dharura,bila kufikia moyoni.Badala yake,tunahitaji kurudi katikati,kurejesha msingi,kujivua yale ambayo ni ya ziada ili kumvaa Kristo.Ni katika mahubiri ya Papa wakati wa kuvalishwa kofia nyekundu kwa Makardinali wapya 21 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,jioni tarehe 7 Desemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Desemba 2024, katika mkesha wa Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, Baba Mtakatifu ameunda makardinali wapya katika Baraza la Makardinali katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican.  Hawa ni Makadinali 21 wapya wanaowakilisha Kanisa lote la Ulimwengu waliopokea kofia nyekundu kwenye Baraza hilo la makardinali. Kabla ya kuanza tendo la kukabidhi  Baba Mtakatifu Francisko alitoa tafakari baada ya usomaji wa Injili. "Hebu tufikirie kuhusu hiyo kidogo ambayo  Yesu anapanda kuelekea Yerusalemu. Kwake siyo kupaa kwa utukufu wa ulimwengu huu, bali kwa utukufu wa Mungu, ambao unahusisha kushuka kwenye shimo la kifo. Katika Mji Mtakatifu, kiukweli, atakufa msalabani, ili kutupatia uzima tena. Lakini, Yakobo na Yohane, ambao badala yake wanawazia hatima tofauti ya Bwana wao, wanatoa ombi lao na kumwomba sehemu mbili za heshima: “Utujalie kuketi katika utukufu wako, mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto(Mk. 10:37)," alisisitiza Papa.

Kofia nyekundu
Kofia nyekundu

Akiendelea Papa alisema kuwa Injili inakazia tofauti hii kubwa: wakati Yesu anachukua njia  yenye kuchosha na yenye mlima ambayo itampeleka hadi Kalvari, wanafunzi wanafikiria njia tambarare na ya kuteremka ya Masiha mshindi. Na hatupaswi kukashifiwa na hili, lakini kwa unyenyekevu tutambue kwamba, kwa  kusema na Manzoni - "hivi ndivyo mkanganyiko huu wa moyo wa mwanadamu unafanywa" (Promessi sposi, sura ya 10). Ndivyo ilivyo. Hili linaweza kututokea hata sisi pia: kwamba mioyo yetu inapoteza njia yake, ikijiruhusu kushangazwa na kupumbazwa na ufahari, kwa kushawishiwa na mamlaka, na shauku ya kibinadamu kwa ajili ya Bwana wetu. Hii ndiyo sababu ni muhimu kuangalia ndani yetu wenyewe, kujiweka kwa unyenyekevu mbele za Mungu na kwa uaminifu mbele yetu wenyewe, na kujiuliza je: moyo wangu unakwenda wapi? Moyo wangu unakwenda wapi leo? Je, unaelekea upande gani? Labda ninakwenda njia mbaya? Hivi ndivyo Mtakatifu Agostino anavyotuonya: “Kwa nini unakwenda kwenye barabarazisizo na watu? Rudi kutoka katika upotofu wako uliokupoteza; Rudi.  Je Wapi? Kwa Bwana. Lakini bado ni mapema: Rudi moyoni mwako […].

Waliopkea kofia ya ukardinali
Waliopkea kofia ya ukardinali

Baba Mtakatifu albainisha kwamba kwa maana sura ya Mungu inapatikana humo; Kristo anakaa ndani ya mtu, ndani yako unafanywa upya sawasawa na sura ya Mungu” (Tafakari ya  Injili ya Yh, 18, 10). Papa ameanza kutafakari zadi ya kifungu cha Rudi moyoni kwamba “. Kurudi moyoni ina maana ya  kurudi kwenye njia sawa na Yesu, hii ndiyo tunayohitaji. Na leo hii hasa kwao Ndugu wapendwa wanaopokea ukardinali na kwamba  wawe  makini kwa kufuata njia ya Yesu Kuifuata njia ya Yesu kunamaanisha kwanza kabisa kurudi Kwake na kumweka tena katikati ya kila kitu. Katika maisha ya kiroho kama katika maisha ya uchungaji, wakati mwingine tunahatarisha kuzingatia mipaka, na kusahau mambo muhimu, Papa alionya. Mara nyingi sana mambo ya pembeni  huchukua nafasi ya yale ambayo ni muhimu, mambo ya nje hushinda kile ambacho ni muhimu sana, tunaingia kwenye shughuli ambazo tunaziona kuwa za dharura, bila kufikia moyoni.  Na badala yake, kila mara tunahitaji kurudi katikati, kurejesha msingi, kujivua yale ambayo ni ya ziada ili  kumvaa Kristo (rej. Rum 13:14).

Hati za utambulisho
Hati za utambulisho

Kwa kuazia zaidi alisema "Hata neno bawaba linatukumbusha hilo, linaonesha eneo ambalo mlango unaingizwa: ni hatua ya kudumu ya msaada. Papa Francisko amekazia kueleza kwamba “ Yesu ndiye msingi na tegemezo, Yesu ndiye kitovu cha uzito wa utumishi wetu, "kiini cha kardinali" kinachoelekeza maisha yetu yote. Kufuata njia ya Yesu pia kunamaanisha kusitawisha shauku ya kukutana."  Yesu kamwe hasafiri peke yake; kifungo chake na Baba hakimtengi na matukio na maumivu ya ulimwengu. Kinyume chake, kwa usahihi kuponya majeraha ya mwanadamu na kupunguza mizigo ya moyo wake, kuondoa mawe ya dhambi na kuvunja minyororo ya utumwa, na kwa sababu hiyo ndiyo ilimleta.  Na hivyo, njiani, Bwana hukutana na nyuso za watu walio na alama ya mateso, huja karibu na wale ambao wamepoteza tumaini, huwainua wale walioanguka, huponya wale walio wagonjwa. Mitaa ya Yesu ina watu wa nyuso na historia na, anapopita, nakausha machozi ya wale wanaolia, Yesu "huponya mioyo iliyovunjika na kuzifunga jeraha zao" (Zab 147:3).

Wakati wa kupokea kofia makardinali wapya

Matukio ya njia, furaha ya kukutana na wengine, kujali walio dhaifu zaidi: hii lazima ihuishe huduma yao kama makadinali. Na mtu mashuhuri, Padre Primo Mazzolari wa Italia, alisema: “Kanisa lilianzia njiani; na kando ya barabara za ulimwengu Kanisa linaendelea na ili kuingia ndani mwake  hauitaji kubisha hodi mlangoni au kutengeneza chumba cha kulala. Tembea na utapata; tembea naye atakuwa kando yako; tembea na utakuwa ndani ya Kanisa" (Tempo di crede, Bologna 2010, 80-81). "Tusisahau kuwa uchovu huharibu mioyo na maji yaliyotuama ndiyo ya kwanza kuharibika."

Makardinali wapya
Makardinali wapya

Kwa Kuifuata njia ya Yesu inamaanisha, hatimaye, kuwa wajenzi wa ushirika na umoja. Papa alisema kuwa "wakati mdudu wa mashindano akiharibu umoja katika kundi la wanafunzi, njia ambayo Yesu anachukua inampeleka Kalvari." Na msalabani anatekeleza utume aliokabidhiwa: kwamba hakuna aliyepotea (Yh 6:39), kwamba ukuta wa uadui hatimaye umebomolewa ( Efe 2:14) na sote tunaweza kugundua kwamba sisi ni watoto wa Baba mmoja na ndugu miongoni mwetu.  Kwa sababu hiyo, akiwaweka mtazamo wake makardinali, wanaotoka katika historia na tamaduni mbalimbali na wanawakilisha ukatoliki wa Kanisa, Bwana anawaita wao kuwa mashuda, mashahidi wa udugu, anawaita wa kuwa mafundi wa ushirika na wajenzi wa umoja. Na hii ndiyo dhamira yao. Akizungmza tu na kundi la makardinali wapya, Mtakatifu Paulo wa Sita alisema kwamba “sisi, kama wanafunzi, wakati mwingine tunajiingiza katika majaribu ya kujigawa; badala yake, “ni katika bidii iliyowekwa katika kutafuta umoja ambapo wanafunzi wa kweli wa Kristo wanatambulika”. Na Papa Mtakatifu huyo aliongeza: "Tunataka kila mtu ajisikie raha katika familia ya kikanisa, bila vizuizi au kutengwa kudhuru umoja katika upendo, na kwamba tusitafute kuenea kwa wengine kwa madhara ya wengine. […] Ni lazima tufanye kazi na kuomba, kuteseka, kupigana ili kutoa ushuhuda wa Kristo Mfufuka" mwisho wa kunukuu (Hotuba ya tukio la kuwasimika, 27 Juni 1977).

Makardinali wapya
Makardinali wapya

Kwa kuhuishwa na roho hii, Papa  Francisko aliwambia makardinali wapya kuwa watafanya tofauti; kulingana na maneno ya Yesu ambaye, akizungumza juu ya mashindano ya uharibifu ya ulimwengu huu, anawaambia wanafunzi wake: "Lakini sivyo hivyo kati yenu". “Lakini sivyo ilivyo kwenu” (Mk 10:43). Na ni kana kwamba anasema: Nifuateni, katika njia yangu, nanyi mtakuwa tofauti; nifuate na mtakuwa ishara angavu katika jamii inayotawaliwa na sura na utaftaji wa nafasi za kwanza. “Msiwe hivyo miongoni mwenu”, mrudie Yesu: pendaneni kwa upendo wa kidugu na kuwa watumishi ninyi kwa ninyi, watumishi wa Injili.” Kwa kuhitimisha Papa alisema Ndugu wapendwa, katika njia ya Yesu, tutembee pamoja na tutembee kwa unyenyekevu, tutembee kwa mshangao, tutembee kwa furaha.

Muonekano wa makardinali wapya
Muonekano wa makardinali wapya

Na orodha rasmi  ya waliopokea kofia ya ukardinali ni  kama ifuatayo:

1. Askofu mkuu Angelo Acerbi, Balozi Mstaafu wa Vatican.

2. Askofu mkuu Carlos Gustavo Castillo Mattasoglio, wa Jimbo kuu la Lima, Perù

3. Askofu mkuu Vicente Bokalic Kalic Iglic C.M., wa Jimbo kuu la Santiago Argentina

4. Askofu mkuu Luis Gerardo Cabrera Herrera, O.F.M., wa Jimbo kuu la Guayaquil, Ecuador.

5. Askofu mkuu Fernando Natalio Chomalí Garib, wa Jimbo kuu la Santiago de Cile Chile.

6. Askofu mkuu Tarcisio Isao Kikuchi, S.V.D., wa Jimbo kuu la Tokyo, Japan

7. Askofu mkuu Pablo Virgilio Siongco David, wa Jimbo kuu la Kalookan, Ufilippin

8. Askofu mkuu Ladislav Niemet, S.V.D., wa Jimbo kuu la Beograd-Smederevo, Serbia

9. Askofu mkuu Jaime Spengler, O.F.M., wa Jimbo kuu la Porto Alegre, Brazil

10. Askofu mkuu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo kuu la Abidjan, Pwani ya Pembe

11. Askofu mkuu Jean-Paul Vesco, O.P., Jimbo kuu la Alger, Algeria.

12. Askofu Mkuu Domenico Batagkua wa Jimbo Kuu la Napoli Italia

13. Askofu mkuu Dominique Joseph Mathieu, O.F.M. Conv., wa Jimbo kuu la Teheran Ispahan, Iran.

14. Askofu mkuu Roberto Repole, wa Jimbo kuu la Torino, Italia.

15. Askofu Msaidizi Baldassare Reina, Jimbo kuu la Roma, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma.

16. Askofu mkuu Francis Leo, wa Jimbo Katoliki la Toronto, Canada.

Makardinali wapya: Changamoto ni ujenzi wa Kanisa la Kisinodi

Makardinali wapya: Changamoto ni ujenzi wa Kanisa la Kisinodi

17. Askofu mkuu Mwandamizi Rolandas Makrickas, Kiongozi mkuu, Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu, Jimbo kuu la Roma.

18. Askofu Mykola Bychok, C.Ss.R., wa Jimbo la “Saints Peter na Paul wa Melbourne nchini Ukraine

19. Padre Timothy Peter Joseph Radcliffe, OP, Mwanataalimungu.

20. Padre Fabio Baggio, C.S., Katibu mkuu msaidizi Idara ya Wahamiaji na Wakimbizi, Baraza la Kipapa la Maendeleo Endelevu ya Binadamu

21. Monsinyo George Jacob Koovakad, Afisa Mwandamizi Sekretarieti kuu ya Vatican na Mratibu wa Hija za Kitume za Baba Mtakatifu

Ikumbukwe kati ya Makardinali wapya, Kardinali Angelo Acerbi, ndiye mwenye umri wa miaka 99 mzee  na kijana zaidi ni Askofu Mykola Bychok, C.Ss.R., wa Jimbo la Mtakatifu Petro na Paulo huko Melbourne nchini Ukraine, Yeye ana umri wa miaka 44. 

Papa kwa makardibali wapya
07 December 2024, 17:00