Tafuta

2024.12.21 Papa akutana na wafanyakazi wa Vatican na wa Roma kutakiana heri za Noeli. 2024.12.21 Papa akutana na wafanyakazi wa Vatican na wa Roma kutakiana heri za Noeli.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa awatakia matashi mema ya Noeli wafanyakazi wa Vatican:maadili ya familia

Kazi na familia ni mambo mawili ambayo Papa Francisko alikazia wakati akikutana na Wanyakazi na familia zao wa Vatican na Jimbo la Roma katika utamaduni wa kila mwaka wa kutakiana heri za siku kuu ya Noeli,Jumamosi tarehe 21 Desemba.Papa:“Kazi ya Yosefu Seremala na Familia kuwa kiukweli iliyoanzishwa na mizizi katika ndoa ndimo maisha huzaliwa na ni muhimu leo hii katika kukaribisha maisha.Amekazia kupitisha maadili,sala na ukaribu kwa Babu na Bibi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 21 Desemba 2024, mara baada ya kukutana na kutakiana heri  za siku kuu zote zanazokaribia  washiriki wa Karibu sana wa Curia Romana, vile vile amekutana na wafanyakazi wa Vatican na wale wa Jimbo la Roma wakiwa na familia zao katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Papa  akianza hotuba yake amewakaribisha na kuonesha furaha ya kubadilishana heri za Noeli. Kwanza kabisa, ametoa shukrani zake kwa kila mmoja wao  kwa kazi wanayofanya, kwa manufaa ya Jiji la Vatican na Kanisa la Ulimwengu. Kama kila mwaka, wamefika na familia zao na kwa sababu hiyo Papa alipenda kutafakari, kwa ufupi nao juu ya maadili haya mawili ya kazi na familia. Akianza kudadavua juu ya  kazi, Papa alisema wanachofanya kwa hakika ni kikubwa, wakipita katika mitaa na nyua za Mji wa Vatican, katika korido na ofisi za Mabaraza  mbalimbali na katika sehemu mbalimbali za huduma, hisia ni kuwa katika mzinga mkubwa wa nyuki. Na hata sasa kuna wale ambao wanafanya kazi ili kuwezesha mkutano huu uwezekanavyo na hawakuweza kufika na kwa njia hiyo amewashukuru wote: “tunasema asante kwao!”

Papa  na wafanyakazi wa Vatican
Papa na wafanyakazi wa Vatican

Papa aliendelea kusema kuwa Mko hapa katika "mazingira ya sherehe, na uchangamfu wa karamu moyoni mwenu, uchangamfu wa tabasamu. Kwa mwaka mzima, hata hivyo, maisha ni ya kawaida zaidi, na sio sherehe, ni kazi ya kuendelea, lakini daima na tabasamu kutoka moyoni. Baada ya yote, hizi ni nyuso mbili tofauti za uzuri ulio sawa: ile ya wale wanaojenga na kwa wengine ni kitu kizuri kwa kila mtu.” Yesu mwenyewe alituonesha sisi kuwa: Yeye ni Mwana wa Mungu, ambaye kwa kutupenda kwa unyenyekevu alikuja kuwa mwanafunzi wa seremala katika shule ya Yoseph ( Lk 2:51-52; Mtakatifu PAULo VI, Mahubiri huko Nazareth, 5 Januari 1964) . Huko Nazareti walikuwa ni watu wachache walioijua hilo, karibu hapakuwa na mtu, lakini katika karakana ya seremala, pamoja na kupitia mambo mengine mengi, wokovu wa ulimwengu ulikuwa ukijengwa na mafundi! Je! mlifikiria juu ya hili: kwamba wokovu ulijengwa "na mafundi"? Papa aliuliza swali. “ Na aliongeza - hali hiyo hiyo, inawahusu ninyi, ambao kwa kazi yenu ya kila siku, katika Nazareti iliyofichika ya kazi zenu maalum, mnachangia kuleta wanadamu wote kwa Kristo na kueneza Ufalme wake ulimwenguni pote (rej Katiba ya Dogmatic, 34-36).”

Papa na wafanyakazi wa Vatican
Papa na wafanyakazi wa Vatican

Papa Francisko akidadavua sehemu ya pili ni ile ya Familia kwamba: “Inafurahisha kukuona hapa pamoja, hata na watoto, ni jinsi gani ilivyo nzuri! Mtakatifu Yohane Paulo II alisema kwamba, kwa Kanisa, familia ni kama “kitoto chake” (Rej. Familiaris consortio, 22 Novemba 1981, 15).” Kwa njia hiyo, Papa alisisitiza juu ya kuwa na Upendo wa familia tafadhali! Na ni kweli: familia, kiukweli, iliyoanzishwa na mizizi katika ndoa, ni mahali ambapo maisha huzaliwa na jinsi gani  ilivyo muhimu, leo hii, kukaribisha maisha!” Kisha ni jumuiya ya kwanza ambamo, tangu utotoni, imani, Neno la Mungu na Sakramenti zinakutana, ambamo tunajifunza kujaliana na kukua katika upendo, katika vizazi vyote. “Imani lazima ienezwe ndani ya familia na Mtakatifu Paulo alisema hivyo  kwa Timotheo: “Mama yako, nyanya yako…” (rej. 2 Tim 1:5). Imani ilipitishwa katika familia. Kwa hiyo  Papa amewatia moyo  daima wabaki na umoja, karibu na kila mmoja na Bwana: kwa heshima, katika kusikiliza,  na kwa kujali. Hata hivyo Papa ameongeza kusema kuwa “Kuna jambo moja ambalo ningependa kusisitiza kuhusu familia. Swali ninalouliza wazazi ambao wana watoto wadogo: mna uwezo wa kucheza na watoto wenu? Je, mnacheza na watoto wenu?  Ni muhimu kulala chini na watoto wa kike, na kiume ili kucheza na watoto wenu! Kisha, jambo jingine: je, mnawatembelea babu na bibi zao? Je, babu na bibi, wako ndani ya familia au wanaishi katika nyumba ya kustaafu bila mtu yeyote kwenda kuwatembelea?

Papa na wafanyakazi wa Vatican na familia zao
Papa na wafanyakazi wa Vatican na familia zao

Inawezekana Bibi na babu ni , lazima wawe katika nyumba ya kustaafu, lakini nenda mkawatembelee! Waweze kuhisi uwepo wenu kila wakati. Daima tukiwa tumeungana,” ninapendekeza, hata katika maombi yanayofanywa pamoja, kwa sababu bila maombi hatuwezi kusonga mbele, hata katika familia. Wafundisheni  watoto kusali! Na katika suala hilo Papa Francisko ameongeza kusema “, katika siku hizi, ninapendekeza mtafute muda mfupi wa kukusanyika pamoja karibu na Pango la  Kuzaliwa kwa Yesu, kumshukuru Mungu kwa zawadi zake, kumwomba msaada kwa siku zijazo na kupyaisha upendo wenu  kwa kila mmoja, mbele ya Mtoto Yesu.

Papa na wafanyakazi na familia zao
Papa na wafanyakazi na familia zao

Papa Francisko amewashukuru kwa mkutano huo na kwa kila kitu wanachofanya. Amewatakia kila la heri kwa Noeli  Takatifu na kwa mwaka unaokaribia kuanza: Mwaka Mtakatifu wa matumaini. Matumaini hukua katika familia pia! Amewabariki na kupendkeza wamuombee. Na ikiwa kuna mtu yeyote ana shida maalum, tafadhali wazungumze, waambie watu wanaosimamia, kwa sababu tunataka kutatua shida zote. Na hili linafanyike kwa njia ya mazungumzo na si kwa kupiga kelele au kukaa kimya. Tuzungumze kila wakati! “Wasimamizi, Kardinali, Papa, Padre kwamba nina shida hii. Unaweza kunisaidia kulitatua?” Na tutajaribu kutatua shida pamoja.” Kwa kuhitimisha aliwashukuru tena na kuwatakia Noeli njema.

papa na heri za Noeli kwa wafanyakazi wa Vatican
21 December 2024, 17:14