Papa:Familia ni kiini cha jamii,ni hazina adhimu ya kutegemezwa na kuilinda!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 29 Desemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amewakaribisha kwa furaha mahujaji wote kuanzia na warumi. Papa ameongeza kusema kuwa: “Leo ninatoa salamu maalum kwa familia zilizopo hapa na wale waliounganishwa kutoka nyumbani kwa njia ya mawasiliano. Familia ni kiini cha jamii,familia ni hazina adhimu ya kutegemezwa na kuilinda!
Ukaribu kwa familia za Korea
Papa Francisko akiendelea kwa njia hiyo mawazo yake yaliwaendelea: “familia nyingi nchini Korea Kusini zinazoomboleza leo hii kufuatia ajali mbaya ya ndege. Ninaungana katika maombi kwa ajili ya waliookoka na waliokufa. Na tunaombe."
Tusali kwa ajili ya familia zinazoteseka na vita
Papa Francisko vile vile amesema, "pia tusali kwa ajili ya familia zinazoteseka kwa sababu ya vita: katika Ukraine inayoteswa, Palestina, Israeli, Myanmar, Sudan, Kivu Kaskazini. Tunaziombea familia hizi zote kwenye vita.”
Salamu za Papa kwa makundi mbali mbali
Papa Francisko vile vile amewasalimu waamini wa Pero-Cerchiate, kikundi cha Dekania ya Varese, vijana wa Cadoneghe na Mtakatifu Pietro huko Cariano; wanafunzi wa kipaimara kutoka Clusone, Chiuduno, Adrara, Mtakatifu Martino na Almenno, Mtakatifu Bartolomeo; Skauti wa Latina, Vasto na Soviore." Kadhalika Papa amewasalimu vijana wa Parokia ya Kirumi ya Mtakatifu Maria Mkingiwa! Amewatakia Dominika njema wote na mwisho wa mwaka wenye amani. Tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kukuona!"