Mercedes imemzawadia Papa gari jipya la wazi la umeme lililo na teknolojia za kisasa

Alasiri,jijini Vatican tarehe 4 Desemba,Mkurugenzi Mtendaji Ola Källenius na washiriki wa timu inayohusika katika uzalishaji walimkabidhi Papa Francisko gari la kipekee la kutengenezwa kwa mkono kulingana na Daraja jipya la umeme la G:"Ni heshima kubwa kwetu,kwa kuzingatia mahitaji yote ya Baba Mtakatifu."Alisema Mkurugenzi wa Mercedes.

Vatican News

Kuanzia leo tarehe 4 Desemba 2024  na kuendelea Papa Francisko  atazunguka katika  Uwanja wa Mtakatifu Petro akiwa  ndani ya gari (Popemobile) jipya la Papa. Katika hafla ya Mwaka Mtakatifu wa 2025, watengenezaji wa magari wa Mercedes-Benz walimletea zawadi siku ya  Jumatano alasiri tarehe 4 Desemba, gari la Daraja  (G) lililo wazi kabisa la umeme lililotengenezwa kwa ajili yake. Ujumbe wa Mercedes uliweza kukutana na Papa Francisko mjini Vatican kwa ajili ya kukabidhiwa gari hilo. Papa Francisko aliomba waziwazi kwamba ingekuwa vizuri wakawepo hata wahusika moja kwa moja katika uzalishaji wa gari hilo. Kwa njia hiyo kundi hilo lililoongozwa na Ola Källenius, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Mercedes-Benz, na wawakilishi wengine wa ngazi ya juu wa Kundi hilo, ambao walikuwa wametoka Ujerumani hasa kwa hafla hiyo walikuwapo.

'Ni Heshima kubwa, Zotter'

"Ni heshima kubwa kwetu kuweza kupeleka gari hili kwa Baba Mtakatifu," alisisitiza Källenius wakati wa kukabidhi gari kwa vipaza sauti vya Radio Vatican - Vatican News. Mercedes tayari inaweza kujivunia uzoefu wa miaka 100 na ile inayoitwa popemobile: gari la kwanza la kipapa lililotengenezwa huko Stuttgart lilikabidhiwa kwa Papa Pio XI mnamo 1930. Papa Francisko pia kwa sasa anatumia La daraja la G-katika katekesi zake , ingawa bado inaendeshwa kwa kutumia petroli. "Tunaelekea kwenye hatua ya sifuri na tunazindua bidhaa nyingi za umeme. Mwaka huu tulizindua umeme wa G. Tuko kwenye njia hii na tutaendelea kufanya hivyo katika miaka ijayo,” alieleza Källenius. Peter Zotter pia alifurahishwa na fursa ya kukutana na Papa na katika maendeleo ya kiwanda cha Graz, ambapo Mercedes G-Class hutengenezwa.” Aidha alisema  “Tayari tumemtengenezea Papa G-Class, lakini hiyo ilikuwa muda uliopita na sikuhusika binafsi. Kuwa na fursa ya kufanya kazi kwenye gari maalum kama hilo labda ni fursa ya kazi mara moja, "alithibitisha Zotter.

04 December 2024, 18:31