Tafuta

Watu 5 wamefariki dunia, zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa na kati yao 41 wako katika hali mbaya huko Magdeburg, Ujerumani. Watu 5 wamefariki dunia, zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa na kati yao 41 wako katika hali mbaya huko Magdeburg, Ujerumani.  (ANSA)

Papa Francisko Asikitishwa na Shambulizi Magdeburg Ujerumani

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Taleb Al Abdulmohsen, mwenye umri wa miaka 50, Daktari wa Afya ya Akili, aliyeingia nchini Ujerumani kunako mwaka 2006, Ijumaa jioni tarehe 20 Desemba 2024 alivamia Soko la Noeli, Magdeburg na kusababisha vifo vya watu 5, na kujeruhi watu zaidi ya 200 na kati yao watu 41 wako katika hali mbaya. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na tukio hili la kinyama, na ameonesha uwepo wake wa karibu kwa waathirika.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., - Vatican.

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Taleb Al Abdulmohsen, mwenye umri wa miaka 50, Daktari wa Afya ya Akili, aliyeingia nchini Ujerumani kunako mwaka 2006, Ijumaa jioni tarehe 20 Desemba 2024 alivamia Soko la Noeli, lililoko mjini Magdeburg na kusababisha vifo vya watu 5, na kujeruhi watu zaidi ya 200 na kati yao watu 41 wako katika hali mbaya. Mji wa Magdeburg ni maarufu sana kwa viwanda na bandari na huko kati kati ya Ujerumani kwenye ukingo wa Mto Elbe. Wachunguzi wa mambo wanasema Taleb Al Abdulmohsen amevamia Soko la Noeli kwa kutoridhishwa na jinsi ambavyo Serikali ya Ujerumani inavyowatendea wakimbizi na wahamiaji na bado anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa uchunguzi zaidi.

Shambulizi la kikatili wakati huu wa maandalizi ya Noeli kwa Mwaka 2024
Shambulizi la kikatili wakati huu wa maandalizi ya Noeli kwa Mwaka 2024

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko amepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa na kwamba, anaungana na watu wenye mapenzi mema kuwaombolezea wale wote waliopoteza maisha kutokana na shambulio hili na kwamba, yuko karibu na wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito! Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, anawapongeza wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa shambulio hili. Baba Mtakatifu anasali pia na kuwaweka waathirika wote chini ya Kristo Yesu, tumaini la waja wake, nuru inayoangaza kwenye giza la uvuli wa mauti. Anawaombea kwa moyo wote msaada na faraja kutoka mbinguni.

Maafa Ujerumani
22 December 2024, 09:33