Tafuta

2024.12.04 Papa anaomba tuombee Ukraine na cnhi zote zinazoteseka kwa vita duniani. 2024.12.04 Papa anaomba tuombee Ukraine na cnhi zote zinazoteseka kwa vita duniani.  (Vatican Media)

Papa Francisko atoa wito wa kuomba amani kwa nchi zilizo kwenye vita

Baada ya Katekesi,Papa ametoa wito wa kuombea amani katika nchi zilizoathiriwa na migogoro.‘Vita ni mbaya,huharibu.Ni watoto wengi wasio na hatia wamekufa.Vita ni kushindwa kwa mwanadamu,’alisema.Alikumbuka mpango wa Poland wa Siku ya Sala na Msaada wa vifaa kwa Kanisa la Mashariki na kushukutu kwa majitoleo katika maeneo hayo,hasa Ukraine.Katika hafla ya usomaji wa kwanza katika lugha ya Kichina,Papa alituma baraka kwa watu wa China.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baadaya Katekesi yake Baba takatifu Francisko Jumatano tarehe 4 Desemba 2024, aliwasalima waamini kwa ugha mbali mbali kutoka pande zote za dunia. Akiwageukia mahujaji wanaozungumza kwa lugha ya kiitaliano aliwakaribisha kwa moyo mkunjufu na hasa kuwasalimia  kikundi cha «A Gesù per Maria», Ushirika wa Giada wa Colle Sannita, Wakujitolea wa Kikosi cha Kitaifa cha Mazingira. Hatimaye, mawazo yake  yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya. Kipindi cha Majilio, ambacho ndiyo kwanza kimeanza, kinatuonesha katika siku hizi kielelezo chenye kung'aa cha Bikira Safi. Papa Francisko aliongeza kusema kwamba kiwatie moyo  katika safari yao ya kushikamana na Kristo na kudumisha tumaini lao. Na "tafadhali, tuendelee kuomba amani! Vita ni kushindwa kwa mwanadamu. Vita haisuluhishi shida, vita ni mbaya, vita huharibu. Tunaombee nchi zilizo kwenye vita. Tusisahau Ukraine inayoteswa, tusisahau Palestina, Israel, Myanmar... Watoto wengi waliokufa, wengi waliokufa wasio na hatia! Tuombe kwa Bwana atuletee amani. Daima tuombe amani,” Papa alikazia kusema.

Wanahija wa Poland

Kwa upande wa wanahija wanaozungumza kipoland, Baba Mtakatifu Francisko alibainisha kuwa “Donimnika  ijayo ni  Siku ya XXV ya Maombi na Usaidizi wa vifaa kwa Kanisa la Mashariki ambalo litaadhimishwa nchini Poland. Ninawashukuru wale wote wanaoliunga mkono Kanisa katika maeneo hayo kwa sala na matoleo, hasa katika Ukraine, inayoteswa na vita. Ninawabariki kutoka ndani ya  moyo wangu!”

Wanahija wa China na Lugha ya kichina katika Katekesi

Baba Mtakatifu Francisko akiwageukia wanahija wanaozungumza kichina amesema: “Leo, kwa furaha kubwa, tunaanza kusoma muhtasari wa katekesi katika lugha ya Kichina. Kwa hiyo ningependa kutoa salamu zangu za dhati kwa watu wanaozungumza Kichina waliopo hapa na wale waliounganishwa kupitia njia ya mawasiliano. Juu yenu nyote na familia zenu ninaomba furaha na amani. Mungu awabariki!”

Papa baada ya Katekesi
04 December 2024, 11:28