Papa Francisko azungumza kwa simu na rais Joe Biden
Na Salvatore Cernuzio – na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa kuzingatia hitimisho la mamlaka yake mnamo Januari, kulikuwa na simu tarehe 19 Desemba 2024, usiku kati ya Rais anayemaliza muda wake wa Marekani, Bwana Joe Biden na Baba Mtakatifu Francisko. Pamoja na kiongozi wa kidemokrasia ambaye kumekuwa na mawasiliano na mikutano kadhaa katika miaka ya hivi karibuni na Papa walijadili juhudi za kukuza amani duniani wakati wa likizo ya Noeli. Mkutano huo ulitangazwa katika barua kutoka Ikulu ya Marekani, ambayo inasomeka kuwa: Biden "alimshukuru Papa kwa kuendelea kujitolea kupunguza mateso duniani, ikiwa ni pamoja na kazi yake ya kukuza haki za binadamu na kulinda uhuru wa kidini." Barua hiyo inasisitiza zaidi kuwa "Rais, pia amekubali mwaliko wa Baba Mtakatifu Papa Francisko kutembelea Vatican mwezi ujao." Na kwa hivyo ziara hiyo itakuwa ya mwisho kabla ya kuondoka Ikulu (White House) mnamo Januari 20, wakati mrithi wake Donald Trump ataapishwa kama rais mpya mteule wa Marekani.
Wasiwasi wa Papa kwa wafungwa waliohukumiwa kifo
Moja ya masuala ambayo ni karibu sana na moyo wa Papa ni lile la wafungwa katika njia ya kifo nchini Marekani. Suala ambalo daima limekuwa likipendwa na Jorge Mario Bergoglio ambaye mnamo mwaka 2018 alibadilisha kifungu namba 2267 cha Katekisimu ya Kanisa Katoliki kusisitiza kutokubalika kwa adhabu ya kifo, siku zote na kwa vyovyote vile, kwa sababu hadhi ya binadamu haishindwi hata kidogo, mtu anapofanya uhalifu mkubwa.
Matumaini ya Jubilei
Katika mojawapo ya video zake na nia yake ya maombi ya kila mwezi, mnamo mwaka 2022, Papa Francisko alibainisha kuwa “Pasiwepo hatua ambayo haitoi haki na inachochea kisasi. Takriban majuma mawili yaliyopita, alirejea kwenye suala hilo kwa kuzingatia Jubilei, ya wakati wa matumaini na huruma ambapo kama alivyoandika katika Tangazo la Hati ya Jubilei ya Spes Non Confundit, yaani Matumaini hayakatishi tamaa, ni matumaini yake kuwa hatua madhubuti zinaweza kuchukuliwa kama vile kusamehewa kwa deni la nje kwa nchi masikini na kukomeshwa kwa adhabu ya kifo katika kila nchi duniani (hadi sasa adhabu hiyo inatumika katika nchi 53 hadi 2022). Kitendo hicho ni "kinyume na imani ya Kikristo" ambacho "huondoa tumaini lolote la msamaha na kufanywa upya", aliandika Papa Francisko.
Wito wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 8 Desemba
Katika sala siku ya Siku Kuu ya Bikira maria Mkingiwa Dhambi ya Asili tarehe 8 Desemba 2024 iliyopita, Papa aliwambia waamini wote waliokuwepo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuunganisha kupitia utiririshaji, akiwaomba "kuwaombea wafungwa walio katika korido ya kifo nchini Marekani. Papa aliongeza kusema “Hebu sisi tuombe ili hukumu yao ifutwe.” Hebu tuwafikirie hawa kaka na dada zetu na tumwombe Bwana kwa neema ya kuwaokoa na kifo."
Msaada wa Maaskofu wa Marekani na vyama vya kibinadamu
Maneno ya Papa yalifuatiwa na wito wa mara moja ya Baraza la Maaskofu wa Marekani iliyoelekezwa kwa Wakatoliki wote nchini Marekani, kumtaka Rais anayemaliza muda wake Biden kutengua hukumu ya kifo kwa watu arobaini ambao kwa sasa wanahukumiwa kifo katika magereza ya shirikisho hadi kifungo cha maisha. Hata awali, Mtandao wa Kikatoliki Kuhamasisha (Cmn), shirika la Kikatoliki la kitaifa ambalo linapigania kukomeshwa kwa adhabu ya kifo nchini Marekani, lilikuwa limeanzisha kampeni ya kubatilisha hukumu za watu 40 wanaozuiliwa kwa sasa katika magereza ya shirikisho. Kulingana na mkurugenzi mtendaji, Krisanne Vaillancourt Murphy kwa Rais Biden - ambaye tayari mnamo Juni 2021 alikuwa ameweka kusitishwa kwa muda kwa hukumu ya shirikisho (ambapo Trump aliahidi kufuta) hii ni fursa ya kipekee na ya mwisho ya kukumbatia mafundisho ya Kikatoliki na kuokoa maisha ya watu hawa. Na kufanya hivyo katika mwezi wa kwanza wa Jubilei, mwishoni mwa mamlaka yake.