Tafuta

Papa Francisko:katika fumbo la Guadalupe,Maria anatualika tusiogope!

Mama Kanisa kila tarehe 12 Desemba,anakumbuka Mama Yetu Bikira Maria wa Guadalupe,ambapo Baba Mtakatifu aliadhimisha Misa alasiri katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro,Vatican.Katika Mahubiri Papa alikazia kuwa na furaha hata katika nyakati ngumu na kukumbuka maneno ya Maria aliyosema: “Usiogope Je,mimi si hapa,Mama yako?Na kwamba “Huu ndio ujumbe wote wa Guadalupe.Mengine ni itikadi."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika siku ambayo Mama Kanisa anafanya Kumbukumbu ya Mama yetu  Bikira Maria wa Guadalupe kiliturujia, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa ajili ya Fumbo hili la "Morenita", Virgen de Guadalupe, "mama" wa Mexico, kama wanavyomwita, na ambaye anayeheshimiwa barani  Amerika ya Kusini yote, lakini pia ulimwenguni, tarehe 12 Desemba 2024. Sura yake, ile iliyochorwa kwenye tilma yaani (Vazi-kanzu) la Mhindi Juan Diego mnamo Desemba 1531, ambalo lilisimamishwa katika Kanisa Kuu la Vatican, kwa ajili ya liturujia ya alasiri. Misa hiyo iliudhuriwa na jumuiya nzima ya Bara la Amerika Kusini waishio Roma katika Siku kuu kubwa sana wanayoheshimu.

Siku kuu ya Bikira Maria wa Guadalupe
Siku kuu ya Bikira Maria wa Guadalupe

Baba Mtakatifu akianza mahubiri yake rahisi kumfafanua Mama Yetu wa Guadalupe alisema: “Tukitazama sanamu ya Maria, Mama Maria wa Guadalupe, ni mja mzito, akitangaza kuzaliwa kwa Mwokozi, ni mjamzito  kama mama. Kwa huruma gani anamwambia Mhindi kuwa: "Usiogope, siko hapa, Mama yako?" (Nican Mapohua, 118-119). Uzazi wa Maria umefunuliwa.”

Mama wa Guadalupe
Mama wa Guadalupe

Baba Mtakatifu aliongeza kusema “Na juu ya fumbo hili la Guadalupe, ambalo kwa bahati mbaya itikadi nyingi zimetaka kukengeusha ili kupata faida ya kiitikadi, juu ya fumbo hili la Guadalupe mambo matatu yanakuja akilini, mambo rahisi, lakini ambayo yanafanya kuleta ujumbe wa: tilma (vazi-kanzu), Mama na waridi. Ni mambo rahisi sana.”

Misa ya mama wa Guadalupe
Misa ya mama wa Guadalupe

Papa aliongeza: “Umama wa Maria bado umewekwa kwenye tilma hii, kwenye vazi hili rahisi. Uzazi wa Maria unaoneshwa kwa uzuri wa mawaridi ambayo Mhindi alichuma na kupeleka  na umama wa Maria hukafanya muujiza wa kuleta imani kwa mioyo isiyoamini kwa kiasi fulani kwa maaskofu.”

Waamini wa Mexico
Waamini wa Mexico

Kwa njia hiyo “Tilma, mawaridi na Mhindi. Kila kitu kinachoweza kusemwa zaidi ya hili kuhusu fumbo la Guadalupe ni uwongo, ni kutaka kulitumia kiitikadi. Siri ya Guadalupe  ni kuiheshimu, na kusikia masikioni mwetu ikisema: "Sipo hapa, Mama yako?" Na kusikiliza hili katika wakati wa maisha, katika nyakati ngumu mbalimbali za maisha, katika wakati wa furaha wa maisha, na katika wakati wa kila siku wa maisha.

waamini wa Mexico
waamini wa Mexico

"Usiogope, sipo hapa, Mama yako?" Na huu ndiyo ujumbe wote wa Guadalupe. Mengine ni itikadi.” Papa alisisitiza. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu aliongeza “Tukienda mbali na picha ya Mama iliyochapishwa kwenye tilma ya Mhindi, na kusikiliza, kama katika wimbo, ambapo kwa sauti ya kurudia rudia anatuambia: "Usiogope, siko hapa, Mama yako?."Na ndivyo iwe hivyo.” Papa alihitimisha.

Mahubiri ya Papa:siku kuu ya Guadalupe
13 December 2024, 08:27