Papa kwa waamini wa Siracusa:Kwa mfano wa Lucia,wanawake wana njia zao za kufuata Yesu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Siku ambayo mama Kanisa anafanya Kumbu kumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Lucia wa Siracusa kisiwani nchini Italia, Baba Mtakatifu amemsifu Mtakatifu huyo katika hafla ya Mwaka uliowekwa kwa ajili ya Lucia huku kwao ambapo mabaki yake yanarudi kwa muda katika mji wake alikozaliwa na kuzikwa baada ya mauaji ya chuki kwa imani yake, tuki lililotendeka katika mateso ya mwaka 304 na wakati huo huo mabaki ya mwili wake uliibwa na kuishia kwanza huko Constantinopoli na kisha, baada vita kubako mwaka 1204, yalipelekwa huko Venezia, hadi sasa. Kwa njia hiyo katika barua iliyotumwa kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Siracusa, Francesco Lomanto, Baba Mtakatifu anabainisha alivyofurahishwa “kusikia kwamba Kanisa la Siracusa linaadhimisha Mwaka wa Lucia, mwaka wa wakfu kwa Bikira na Shahidi Lucia, raia mwenzenu.”
"Kupyaisha roho ya Injili"
Mapendo ambayo yanawaunganisha kwa Mtakatifu Lucia kwa hivyo Papa amesema yamewarudisha kwenye ufahamu wa Kikristo wa zamani zaidi: "Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza hata kidogo" (1 Yh 1:5). Na kukumbuka kwamba Mtume aliongeza kusema mara moja kwamba: “Tukisema kwamba tuna ushirika naye na tunatembea gizani, sisi ni waongo na hatuifanyii ukweli katika vitendo, bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi” (1 Yh 1:6-7). Baba Mtakatifu katika siku kuu ya Mtakatifu Mlezi wao, anamwandika Askofu Mkuu huyo, na jumuiya nzima ya jimbo kuu, ili maneno haya ya wokovu pia yaweze kuongoza njia yao leo na kuwapyaisha katika roho ya Injili, vifungo vya familia, kikanisa na kijamii ambavyo mji wao mzuri umefumwa.
"Jubilei: Mahujaji wa Matumaini "
Mwezi wa Desemba utafikia kilele mwaka huu katika kuanza kwa Jubilei inayoita: "Mahujaji wa matumaini," lakini ni alama kwao na hija nyingine, ile ya Mtakatifu Lucia kutoka Venezia hadi Siracusa yaani, kutoka katika mji ambao umelinda mwili wake kwa karne nane hadi ule ambao ushuhuda wake uling’aa hapo mwanzo, ukieneza nuru katika ulimwengu wote. Mwendo wake kuelekea kwao unaakisi fumbo la Mungu ambaye daima huchukua hatua ya kwanza, na ambaye haombi kamwe kile ambacho mtu mwenyewe hayuko tayari kufanya. Baba Mtakatifu ameandika kwamba Mtakatifu Lucia anakwenda kwao, ili wao wenyewe wawe wanaume na wanawake wa hatua ya kwanza, mabinti na wana wa Mungu wanaokusanyika pamoja. Ushirika kati ya Makanisa mawili mahususi, ambao ulifanya tafsiri hii ya muda iwezekane, kwa upande mwingine unaonesha njia ya kuishi katika ulimwengu unaoweza kushinda giza linalouzunguka, kwamba kuna nuru ambapo zawadi hubadilishwa, na ambapo hazina ya mtu ni mali kwa kila mmoja. Uongo unaoharibu udugu na kuharibu uumbaji, na unapendekeza, hata hivyo, kinyume chake: kwamba mwingine ni mpinzani na ni tishio. Na kwa bahati mbaya mara nyingi sana wanadamu hujiona hivyo.”
Wanawafuzi wa kike wa Yesu zamani na leo hii
Baba Mtakatifu Francisko akimfafanua mtakatifu huyo amesisitiza kuwa “Lucia ni mwanamke na utakatifu wake unaonesha kwao na kwa Makanisa yote ni kiasi gani wanawake wana njia zao za kumfuata Bwana. Tangu masimulizi ya Injili, wanafunzi wa kike wa Yesu wameshuhudia akili na upendo ambao bila hiyo ujumbe wa Ufufuko haungeweza kutufikia. Kwa kumwiga Mlinzi wao, wakiutazama kwa uangalifu, unaonesha kwa uthabiti heshima na uwezo wa kutazama mbali, ambao wanawake Wakristo bado wanauleta katikati ya maisha ya kijamii leo, bila kuruhusu mamlaka yoyote ya kiulimwengu kufunga ushuhuda wao kwa kutoonekana na kimya. Papa ameongeza:“Tunahitaji kazi na maneno ya kike katika Kanisa linalotoka nje, ambalo ni chachu na jepesi katika utamaduni na kuishi pamoja. Na hii ni zaidi sana katika moyo wa Mediterania, chimbuko la ustaarabu na ubinadamu, kwa huzuni katikati ya dhuluma na ukosefu wa usawa ambao tangu safari yangu ya kwanza ya kitume, hadi Lampedusa, nimependekeza kubadilika kutoka kwa utamaduni wa kutupa na kuwa utamaduni wa kukutana.”
"Mauaji ya Mtakatifu Lucia yatufundishe kilio cha huruma na upole"
Papa Francisko amefafanua kwamba: “Mauaji ya Mtakatifu Lucia yatufundishe katika kilio, huruma na upole na hizi ni fadhila zilizothibitishwa na Machozi ya Mama huko Siracusa. Si fadhila za Kikristo tu, lakini pia za kisiasa. Zinawakilisha nguvu ya kweli inayojenga jiji. Zinatupatia mitazamo ya nyuma ya kuona, kuona kwamba kutojali hutufanya tupoteze sana. Na ni kwa jinsi igani ilivyo muhimu kusali ili macho yetu yapone! Papa Francisko amekazia kusema kuwa “ Kwa upande wa nuru, pia hutuweka wazi kwenye kifo cha imani. Labda hautaweka mikono yao juu yetu, lakini kuchagua upande, kutaondoa amani ya akili. Kwa sababu kuna aina za utulivu, kiukweli, zinazofanana na amani ya makaburini. Kutokuwepo, kana kwamba tumekwisha kufa; au sasa, lakini kama makaburi ambayo ni mazuri kutokea nje, lakini ndani yake ni matupu na mifupa. Badala yake, tunapaswa kuchagua maisha. Hatungeweza kufanya vinginevyo: “Kwa maana uzima ulifunuliwa, tuliuona”(1Yh 1:2),” Papa alisisitiza.
"Kuzunguka Lucia ni kuona misha ya sasa na kuchagua nuru"
Papa Francisko vile vile amefikiria umati mkubwa unaozunguka Mtakatifu Lucia huko Siracusa kwamba “Kukusanyika karibu na Mtakatifu, inamaanisha kuona maisha yakijidhihirisha na sasa kuchagua upande wa nuru. Kuwa wazi, watu wa kweli; kuwasiliana na wengine kwa njia ya wazi, na ya heshima; kuepuka utata wa maisha na mafungamano ya uhalifu.” Kwa hiyo wasiogope magumu. Papa amesisitiza kwamba wasichoke kamwe kuelimisha wasichana na wavulana, vijana na watu wazima – kwa kuanzia na sisi wenyewe, kwa kusikiliza mioyo, kutambua mashahidi, kukuza hisia za kukosoa, na kutii dhamiri. Mungu ni nuru na tafakari yake ni jumuiya ya kaka na dada waliofunzwa katika uhuru, ambao hawatulii kwa mashaka katika kile wanachosema - hakitabadilika kamwe.
"Msisahau kuwapeleka katika sherehe kaka na dada wanaoteseka ukosefu wa haki"
Papa amesisitiza juu ya neno ‘Kuchagua’: “hapa ni msingi wa chachu ya kila wito, jibu la kibinafsi kwa wito ambao watakatifu wanawakilisha katika safari yetu. Unafichua jinsi ya kutoroka kutoka katika "makazi hayo ya kibinafsi au ya jamii ambayo huturuhusu kuweka umbali wetu kutoka katika kiini cha mchezo wa kuigiza wa mwanadamu. [...]. Tunapofanya hivyo, maisha daima yanakuwa magumu ajabu kwetu na tunaishi uzoefu mkubwa wa kuwa watu, uzoefu wa kuwa mali ya watu"(Evangelii gaudium, 270). Papa Franciko akimwelekea Askofu Mkuu na waamini wote wa Siracusa ameomba “wasisahau kuwapeleka kiroho katika sherehe yao kaka na dada wanaoteseka kwa mateso na ukosefu wa haki ulimwenguni kote.” Wajumuishe “wahamiaji, wakimbizi, maskini walio miongoni mwao.” Na tafadhali Papa amewaomba wamkumbuke katika sala pia. Kwa Maombezi ya Mtakatifu Lucia na Mama Yetu wa Machozi yawasindikize watu wake, ambao kwa upendo Papa amewatumia Baraka ya Kitume.