2024.12.20 Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Italia la mchezo wa Matufe. 2024.12.20 Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Italia la mchezo wa Matufe.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Matufe ni mchezo mzuri wa urafiki wa kijamii

Katika salamu kwa wawakilishi wa Shirikisho la Kiitaliano la sekta ya Mchezo wa matufe,Papa alionesha huruma ya mchezo huo ambao“labda kidogo huko nje ya mtindo lakini unaohusishwa na uhuishaji wa ulimwengu wa vijijini na jumuiya za parokia na kwamba ni mchezo wa utulivu mbadala wa mashine kubwa ya biashara ya michezo.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akikutana Ijumaa tarehe 20 Desemba 2024, alifurahi kukutana na, wawakilishi wa Shirikisho la mchezo wa Matufe wa Italia, pamoja na Rais wa kimataifa na baadhi ya mamlaka za kiraia, ambao amewashukuru kwa uwepo wao. Papa Francisko alibainisha anavyopenda sana mchezo wa Matufe. Kwa sababu mbili: ya kwanza, kwa sababu ni mchezo maskini, ukilinganishwa na wale wa nyota wenye mikataba ya mabilioni ya dola, ambao daima hujaza vyombo vya habari.

Papa na shirikisho la Italia la Mchezo wa Matufe
Papa na shirikisho la Italia la Mchezo wa Matufe

Nadhani mabingwa wa mchezo wa matufe ni watu ambao ni wafanyakazi, au walimu, au mafundi bomba. Kwa kifupi, watu wa kawaida ambao wana shauku ya mchezo huu, labda nje ya mtindo, lakini ni matajiri katika ubinadamu. Papa ameonesha sababu ya Pili ya kuondolea kwake mchezo wa matufe kuwa ni mchezo ambao ninashirikishana na aina fulani ya urafiki, ya urafiki wa kijamii. Hapo zamani ilikuwa umeenea sana katika vijiji, katika ulimwengu wa vijijini, kila mahali kulikuwa uwanja wa matufe hata katika maparokia.

Papa na shirikisho la Mchzeo wa matufe Italia
Papa na shirikisho la Mchzeo wa matufe Italia

Ilikuwa ni njia ya kuwa pamoja, ya kutumia muda katika ushirikai, furaha ya afya na amani. Kwa bahati mbaya, jamii imebadilika, na hivyo pia mchezo wa boce: wanawake na vijana pia hucheza; Watu wengi wenye ulemavu wanafanya mazoezi, na ninawapongeza kwa haya yote. Papa Francisko amewapongeza kwa matokeo waliyoyapata kama Shirikisho kwa kiwango cha ushindani; na zaidi ya yote kwa sababu wanaendeleza mchezo huu mbadala ikilinganishwa na mashine kubwa ya biashara ya michezo, mchezo unaojumuisha, ambao bado una ladha ya "mchezo" na kampuni nzuri. Papa amewabariki kwa moyo wote na shughuli zao. Na tafadhali wasisahau kumuombea.

Papa kwa mchezo wa matufe Italia
20 December 2024, 15:56