2024.12.07 Waandaaji wa na Wasanii wa "Tamasha la Maskini" litakalofanyika tarehe 7 Desemba usiku. 2024.12.07 Waandaaji wa na Wasanii wa "Tamasha la Maskini" litakalofanyika tarehe 7 Desemba usiku.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Tamasha na maskini ni kama Jubilei inayolenga kuleta matumaini!

Papa Francisko akikutana na wahamasishaji na wasanii wa hafla ya toleo la V la Tamasha la Maskini lililopangwa kufanyika tarehe 7 Desemba 2024 usiku mjini Vatican,alisema watu dhaifu zaidi wanaalikwa kuwa sehemu ya wimbo huu wa ajabu wa upendo ambao ni Injili.Chaguo la kuwa upande wa maskini hutoa ishara ya matumaini.Hivi ndivyo Jubilei inayofuata inalenga kuzalisha ishara za matumaini,kuanzia chanzo cha upendo ambacho ni Moyo wa Yesu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 7 Desemba 2024 alikutana na wamahasishaji na wasanii katika fursa ya 'Tamasha la Maskini' lililopangwa kufanyika tarehe 7 Desemba 2024, jioni katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican  kwa ushirikiano na Kurugenzi ya  Mji wa Vatican na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo. Akianza hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko alifurahia kukutana nao tena kwa mwaka huu, kwamba ni wakati mzuri wa kuwashirikisha ndugu zetu wengi uzuri wa muziki ambao huunganisha mioyo na kuinua roho. Papa alisikia mtoto akilia na kusema kuwa “ Hata watoto wachanga hufanya muziki wanapolia!” Papa alimsalimia kwa hiyo Monsinyo Marco Frisina, ambaye kwa mara nyingine aliweza kuwaleta pamoja wasanii wa kimataifa, pamoja na Kwaya ya Jimbo la  Roma  ambayo mwaka huu inaadhimisha miaka arobaini ya shughuli, kikundi kipya ambacho pia kinashughulikia tukio hili, amewashukuru, Asante! Salamu kwa  wasanii wote, hasa, kwa ushiriki wake maalum, Mwalimu Hans Zimmer; vile vile mwigizaji Tina Guo, mtunzi Dario Vero na mwigizaji Serena Autieri.Amewashukuru pia Washirika wote waliochangia kufanikisha tukio hilo.

PAPA NA WAANDAJI NA WASANII WA TAMASHA LA MASKINI
PAPA NA WAANDAJI NA WASANII WA TAMASHA LA MASKINI

Papa alisema kuwa “Tamasha ni fumbo la kupendeza, fumbo la maelewano, hata la maelewano ya sinodi ambayo Kanisa linajitahidi kuishi kikamilifu zaidi. Kiukweli, kila alama ya muziki inachanganya ala na sauti tofauti, kila moja ikiwa na sehemu yake, na mdundo wake na sifa yake. Kila mtu katika okestra hucheza alama zake mwenyewe lakini lazima zipatane na zingine, na hivyo kuzalisha uzuri wa muziki.” Papa aliongeza “Na katika muundo, kimya, vipindi, vyake vyo vina umuhimu sawa kwa maelezo yenyewe. Mungu haumbi ubadhirifu! Kila mtu ameitwa kujieleza, kucheza sehemu yake pamoja na kila mtu mwingine. Ili kutambua mfano huu wa maelewano ni muhimu kuchagua kuwa huko. Sio kupewa.” Kwa maana hiyo alisema wote hao wamechagua kuwepo, kushiriki katika tukio hilo na watu wenye uhitaji, ambao wanajitahidi kusonga mbele kila siku. Na chaguo hilo lao hutoa ishara ya matumaini.” Kwa kuongeza Papa alisema “Hivi ndivyo Jubilei inayofuata inalenga pia kufanya kwa  kuzalisha ishara za matumaini, kuanzia na chanzo cha upendo ambacho ni Moyo wa Yesu.” Bila ushirikiano wa kila mtu maelewano ya kweli haywezi kuundwa. Ni kutoka katika tamasha la watu tofauti tu ndipo maelewano huibuka ambayo hujenga na kumfariji kila mtu. Vilevile, Kanisa linaloitwa kuwa ni ishara na chombo cha maelewano, ushirika na udugu ulimwenguni, linapaswa kuunda ndani ya moyo wa mwanadamu wimbo wa ajabu na makini wa upendo kwa Mungu na ndugu.”

WAANDAAJI NA WASANII WA TAMASHA LA MASKINI
WAANDAAJI NA WASANII WA TAMASHA LA MASKINI

“Tamasha hili na Maskini ni ishara nzuri ya upatanisho wa sinodi, hasa kwa sababu hufanyika katika ushirika na kaka na dada zetu walio dhaifu sana, walioalikwa kuwa sehemu ya wimbo huu wa ajabu wa upendo ambao ni Injili.” Papa alisisitiza. Marafiki zetu hawa, usiku wa leo, wataweza kuhudhuria tamasha kwa njia bora zaidi, kama wahusika wakuu; kwa sababu uzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa wanadamu wote, kuunganishwa kwa heshima sawa na kuitwa kwa udugu. Papa aliwakabidhi kwa Familia Takatifu ya Nazareti, iliyopitia hali ya hatari na uhamisho bila kukata tamaa. Bwana awaweke daima nuru za  matumaini zikae ndani yao! Anawaombea, kwa utambuzi wa mafanikio ya mpango huo. Na tafadhali wamwombee pia. 

Papa na wasanii
07 December 2024, 11:26