Papa Francisko:Utumwa mamboleo ni uhalifu na madhara kwa binadamu!
Vatican News
Katika fursa ya Siku ya Kimaitafa Duniani ya Kukomesha Utumwa na Utumwa mamboleo ifanyikayo kila ifikapo Desemba 2, ya kila mwaka Baba Mtakatifu Francisko katika chapisho la akaunti ya @Pontifex, ameandika kwamba: “Utumwa mamboleo wa biashara haramu ya binadamu, kazi ya kulazimishwa, ukahaba, usafirishaji wa viungo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Sisi sote ni vielelezo vya sura ya Mungu na hatuwezi kuvumilia kuona sura ya Mungu aliye hai ikitendewa vibaya zaidi.” Hii ni Siku iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kukumbuka tarehe 2 Desemba 1949, wakati Baraza Kuu lilipoidhinisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kukomesha Biashara Haramu ya Binadamu na unyonyaji wa ukahaba na wengine mengi.
Ujumbe wa Siku ya Sala dhidi ya Usafirishaji haramu wa binadamu
Utumwa umekuwa na sura nyingi sana kadiri siku zinavyopita. Mnamo mwaka 2024, Papa Francisko kwa mara nyingine tena alitoa sauti yake dhidi ya aina hizi za utumwa mamboleo, hasa katika ujumbe wake kwa Siku ya X ya Sala na Tafakari dhidi ya Usafirishaji haramu wa binadamu duniani mnambo Februari 8, katika kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Josephine Bakhita, mtawa Mkanosa aliyezaliwa Sudan na ambaye aliuzwa utumwani akiwa mtoto. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anafafanua “biashara haramu ya binadamu ni janga la kimataifa, ambalo lakini hatujachelewa sana kuamua kuitikia wito wa kukomesha. Kwa kumkumbuka Mtakatifu Bakhita, Papa Francisko alisisitiza kuwa, “sisi sote tunaitwa kutosimama watulivu badala yake ni lazima kuhamasisha nguvu zetu zote, kuitikia wito huo wa mabadiliko ili kufikia mzizi wa jambo hili, na kutokomeza sababu zake.
Kutambua utu wa kila mtu na kuchukua hatua dhidi ya biashara haramu na aina yoyote ya unyonyaji.” Usafirishaji haramu mara nyingi hauonekani. Vyombo vya habari, shukrani pia kwa waandishi wa habari wenye ujasiri, vilitoa nuru ya utumwa wa wakati wetu, lakini utamaduni wa kutojali unalegeza hali hiyo. Kwa njia hiyo Papa alisisitiza kwamba “Tusaidiane kwa pamoja kuitikia, kufungua maisha yetu, mioyo yetu kwa dada na kaka wengi wanaotendewa kama watumwa.” Baba Mtakatifu Francisko pia alituomba tusikilize kilio cha kuomba msaada kwa wale wanaoteseka katika migogoro au vita, wale walioathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, wahamiaji wa kulazimishwa na wale ambao ni lengo la unyonyaji wa ngono au kazi, hasa wanawake na wasichana. .
Malkia Isabella aliyewaachilia watumwa
Mnamo Septemba 19, katika ujumbe ulioandikwa wakati wa uwasilishaji wa kitabu kiitwacho “Wakati uliopita,Uliopo na Ujao wa Mpito wa Haki: Uzoefu wa Amerika ya Kusini katika kujenga amani duniani,” Baba Mtakatifu Francisko alikumbusha majibu ya Malkia Isabella wa Castile alipopata habari kuhusu kuuzwa kwa watu wa kiasili kama watumwa, baada ya mojawapo ya safari za kwanza za Columbus kuelekea Amerika. Mfano wazi, kwa Papa Francisko, wa hali ya migogoro na ukandamizaji ambapo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu umetokea, ukifuatiwa mara moja na msururu wa hatua zilizopitishwa na Taji, ambayo itakuwa kiini cha maazimio yetu ya kisasa, ya haki za binadamu.”
Baba Mtakatifu Francisko alitoa mafunzo matatu kutoka kwahistoria: Funzo la kwanza ni kwamba "historia hairudi nyuma" na kwamba ukweli wa haki zaidi lazima ujengwe upya kutoka katika majeraha ya hali fulani. Fundisho la pili "ni jibu la mara moja" kwa Malkia Isabella kama mamlaka ya kisiasa na kama dhamiri ya maadili ambayo inasimama kutetea utu wa binadamu na inaweza kuwa suluhisho la kijasiri, ubunifu na thabiti, ikichukua hatua hasa ya kuwakomboa watumwa hata kwa gharama ya pesa zao na mageuzi ya kitaasisi, kukataza utumwa na kudai haki za kimsingi za walioharibiwa kwa njia ya haraka na muhimu. Fundisho la tatu, linalofafanuliwa na Papa Francisko kama labda gumu zaidi, linahusu “utumiaji mzuri na thabiti wa masharti hayo ya Mkataba, saini, sheria, na kwamba inaweza kuwa barua iliyokufa ikiwa njia hazijatayarishwa ili kwa umakini, akili ya kawaida na uvumilivu, sio barua tu, bali pia roho inayoihuisha, iweze kuwafikia wale ambao ni walengwa wa moja kwa moja.
Mkutano na wanafunzi wa Leuven, Ubelgiji
Baba Mtakatifu akizungumza kuhusu aina mamboleo ya utumwa kwa wanafunzi vijana wa Chuo Kikuu Katoliki cha Louvain, wakati wa ziara yake ya kitume nchini Ubelgiji, mnamo tarehe 28 Septemba 2024, aliakisi uovu wa jeuri na kiburi ambao huharibu mazingira na watu, ambayo vita ni usemi wa kikatili zaidi. Pamoja na ufisadi na aina za utumwa mamboleo, maovu ambayo wakati mwingine huichafua dini yenyewe na kuifanya kuwa chombo cha kutawala. Lakini hii ni kufuru, alisema Papa Francisko. Muungano wa wanadamu na Mungu, ambao unaokoa Upendo, unakuwa utumwa. Hata jina la Baba, ambalo ni ufunuo wa utunzaji, linakuwa kielelezo cha kiburi.
Congo DRC na utumwa katika Afrika ya leo
Katika Katekesi ya tarehe 20 Septemba 2023, ambapo Mama Kanisa anamkumbuka ushuhuda wa askofu mmisionari Mtakatifu Daniele Comboni, Papa alisisitiza kile kilichosemwa katika mkutano na viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) huko Kinshasa, mnamo tarehe 31 Januari 2023. Kwa hiyo, alisema “kama Wakristo, tumeitwa kupambana na kila aina ya utumwa. Kwa bahati mbaya, hata hivyo, utumwa, kama ukoloni, si kitu cha zamani. Katika Afrika inayopendwa sana na Comboni, ambayo leo imesambaratishwa na migogoro mingi, baada ya ile ya kisiasa, ukoloni wa kiuchumi' wenye utumwa sawa na huo unaendelea (...). Ni mchezo kama wa kuigiza ambao ulimwengu ulioendelea zaidi kiuchumi mara nyingi hufumba macho, masikio na midomo." Papa aliongeza “Kwa hiyo ninapyaisha tena ombi langu: “Acheni kusonga Afrika: si mgodi wa kunyonywa au ardhi ya kuporwa.”
Usafirishaji haramu wa binadamu katika Laudato si'
Kwa upande sauti ya Papa kwa wanyonge, bado tunamkumbuka katika Waraka wa Kitume wa Laudato si' yaani sifa na iwe kwa Mungu kuhusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya Pamoja pamoja na Fratelli Tutti yaani wote ni ndugu ambamo pia tunapata ndani mwake aina mpya za utumwa na ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kijamii, huku akisisitiza kwamba biashara haramu ya binadamu inachochewa na dhuluma hizo. Katika waraka wa Laudato si' , Papa anatualika kupiga vita dhidi ya biashara haramu ya binadamu kupitia aina za ushirikiano wa kimataifa unaohusisha serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema. Zaidi ya hayo, anaakisi umuhimu wa kukuza utu wa binadamu, haki ya kijamii, usawa na mshikamano, ili biashara haramu ya binadamu itokomezwe.
Papa Francisko katika Waraka wake kuhusu ikolojia fungamani, kwa njia hiyo, anakemea mantiki ya kutupwa ambayo inahalalisha kila aina ya upotevu, ambayo inapelekea kuwanyonya watoto, kuwatelekeza wazee, kuwapunguzia wengine utumwani, kukadiria kupita kiasi uwezo wa soko wa kujisimamia wenyewe, kufanya biashara haramu ya binadamu na biashara ya “almasi za damu.” Ni mantiki ile ile ya vikundi vya kihalifu vya mafia wengi, wanunuzi wa viungo vya binadamu, biashara ya dawa za kulevya na kuwatupa watoto walio tumboni kwa sababu haziendani na mipango ya wazazi. Kukabiliana na haya yote, Papa alisema kuwa "tunahitaji mapinduzi ya kiutamaduni ya ujasiri" ambayo kwanza inaweka katikati thamani ya uhusiano kati ya watu na ulinzi wa maisha ya kila mwanadamu."
Wito wa Waraka wa Fratelli tutti
Hatimaye, katika Waraka wa Fratelli tutti, Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza kwamba, kazi ya siasa ni kutafuta suluhisho za kila jambo linalotishia haki msingi za binadamu, kama vile kutengwa na jamii; usafirishaji wa viungo, tishu, silaha na madawa ya kulevya; unyonyaji wa kijinsia; kazi ya utumwa; ugaidi na uhalifu uliopangwa. Na alizindua ombi kali la kukomesha biashara haramu, ambapo alisema ni aibu kwa ubinadamu, na njaa, kwani ni uhalifu kwa sababu chakula ni haki isiyoweza kuondolewa katu kwa mwanadamu.”