Papa Francisko:Tafadhali,tusizime tumaini la maskini na wahamiaji!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Fancisko, Ijumaa tarehe 6 Novemba 2024 alikutakutana mjini Vatican na Jumuiya ya Mafunzo ya Taalimungu ya Mtakatifu Paulo kutoka Catania. Alanza na salamu na Msimamizi Taasisi ya mafunzo hayo Maaskofu wengine na Mkurugenzi wa Mafunzo, walimu na maafisa wengine, wakiwemo wanafunzi wote. Utafiti wa Kitaalimungu wa Mtakatifu Paolo unaweza kuchukuliwa kuwa ni tunda la kwanza la Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kwani: ulizaliwa mwaka 1969, wakati majimbo ya mashariki mwa Sicilia yaliamua kuanzisha sehemu moja ya mafunzo ya kitaalimungua, ambayo baada ya muda yameonekana kuzaa matunda kwa mapadre na watawa, na watu wa kawaida walei. Papa Francisko anawatia moyo kuendelea mbele katika michakato ya kuendelea safari ya pamoja wakati wa mafunzo mapana ambayo yawe na uamuzi wa maisha ya kikanisa na kijamii. Pamoja na Kitengo cha Kitaalimungu cha Palermo. Ambao wao wanahusika, mafunzo yao yanaunda mitindo ambayo inatia chachu hata kwa Makanisa mengine kutembea pamoja katika muktadha huo.
Papa alisema kwamba kwa hakika, tunapozungumza kuhusu ushirika lazima pia tujumuishe uhusiano kati ya miundo ya mafunzo, ambayo inakuwa maabara ya ushirika na utume, inayohuishwa na tafakari ya kitaalimungu. Mkutano wa hivi karibuni wa Sinodi ya Maaskofu ulisisitiza mwelekeo wa sinodi ya huduma ya wataalimungu na taasisi za kitaalimungu (taz. Hati ya Mwisho, 67). Utume wa Utafiti ya Ktaalimungu haiwezi kupuuza eneo ambalo lipo. Kwa hivyo, tayari katika taaluma yao, wana uzoefu wa kuwa kikanisa, ambapo wanakuwa karibu na kila mmoja, katika utofauti wa miito na karama na katika kutafuta njia mpya za uinjilishaji. Hii nayo ni ishara ya nyakati za kushika kwa hekima; ni mtindo wa uwajibikaji pamoja ambao unafunza leo hii na ambao unapaswa kuendelea katika maisha ya Makanisa yao, wakiimarisha karama za kila moja. Kwa miaka mingi, idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka kati yao na leo hii wamejumuishwa katika jumuiya zao za kikanisa wakiwa na majukumu ya kichungaji, mafundisho ya kidini na kitaaluma: hii pia ni ishara ya nyakati, katika eneo ambalo mara nyingi wanawake wameshushwa thamani katika nafasi yao ya kijamii. Lakini tusisahau kwamba Sicili ni nchi ya mashahidi watakatifu kama Agata na Lucia, ambao walikuwa ‘mbegu’ za imani thabiti, zenye uwezo wa kujifanya upya na daima kutoa mashahidi wapya, kama vile, kwa mfano, katika wakati wetu, Mwenyeheri Giuseppe Puglisi na Rosario Livatino.
Papa aliendelea kusema kuwa ardhi yao ina uzuri wa asili na wa sanaa ya maajabu , kwa bahati mbaya inayatashwa na kutoka na uvumi na ufisadi wa kimafia, ambao unapunguza kasi ya maendeleo na kupunguza rasilimali, kulaani maeneo ya ndani zaidi ya yote kwa uhamiaji wa vijana. Sicilia inahitaji wanawake na wanaume ambao wanatazama wakati ujao kwa matumaini na kuunda kizazi kipya kuwa hururu na wazi katika utunzaji wa wema wa pamoja, na ili kuweza kukomesha umaskini wa kizamani na mpya. Papa Francisko aliwaeleza vijana haio kuwa Katika Kristo, tunageka wenye uwezo wa kuhusiana mmoja na miowngine kwa njia safi, na furaha na kujenga katika dulimwengu huu Ufalme wa upendo na wa haki. Moyo wetu uliounganishwa na ule wa Kristo una wezo wa muujiza huo wa kijamii Lett. enc. Dilexit nos, 28). “Mfanye kazi na vijana ili wanaokwenda kusoma nje warudi. Sicilia isipoteze damu yake kijana, ambaye alikwenda kusoma! Mjue jinsi ya kushuhudia kwamba tamaduni na mafunzo ya Masomo ya Kitaalimungu ni katika huduma ya watu, maskini, hata wadogo.” Katika ardhi yao, ambayo imekuwa njia panda ya watu, wahamiaji wengi hufika na wengi huacha kujumuika: “Ninawasihi muwe wakaribishaji, tuwe wabunifu katika udugu.”
Papa alikazia kueleza kuwa "Na dhamira hii itazaa matunda zaidi ikiwa mtajua jinsi ya kufanya mazungumzo na tamaduni na dini za watu wengine wa Mediterania, ambao wanatazamia siku zijazo kwa matumaini. Tafadhali, tusizime tumaini la maskini, la wahamiaji hao maskini! Muwakaribishe wahamiaji. Jumuisha wahamiaji. Kwenu pia kuna changamoto ya wahamiaji Waislamu: jinsi ya kuwaunganisha na kuwasaidia kuingia katika majimbo. Papa alisema mafunzo yao ya kitaalimungu yalikarabatti matunda ya uhusiano na Chuo Kikuu cha Katania, Taasisi ya Kiutamaduni ya Kale sana ya Sicilia, na wakufunzi wengi wanajitahidi katika Kozi ya mafunzo ya Kikristo, Kanuni, ya bioethics yaani nyanja ya masomo na mazoezi ya kitaalamu, inayovutiwa na masuala ya kimaadili yanayohusiana na afya yanayolenga hasa binadamu, lakini pia inazidi kujumuisha maadili, ikiwa ni pamoja na yale yanayotokana na maendeleo ya biolojia, dawa na teknolojia.) Kwa njia hiyo Ushirikiano huo kwa hakika unastahili kwao, kwa sababu unafungua mafunzo yao na wakati wao ujao wa mazungumzo ambayo daima yanapaswa kukuzwa, kwa ajili ya kuelewa vema ulimwengu ambao wanaishi na kwa ajili ya kutamadunisha imani. Kwa upande mwingine, unatoa uhusiano wa matunda wa utamaduni wa watu wao, ambao wamegubikwa na majanga ya baadhi ya uzoefu wa maisha. Katika hilo Papa amesifia waandishi wa vitabu, wakubwa wa Sicilia, kwa namna ya pekee, Verga ambaye ni maarufu kwa riwaya ya “VINTI” yaani Ushindi, ambayo inajikita juu ya uchungu na umaskini. Katika mazungumzo na utanaduni huu, ambao unaeleza wazi namna nyingi za kuishi, na kufikiria watambue kubeba matumaini na jitihada, watambue kujikabidhi katika matumaini. “Msijikabidhi katika malalamiko, kwa sababu malalamiko ni jambo lisilo la kijasiri katika kukata tamaa, lakini kwenda mbele na muwe wamisionari wa fadhila hizi.”
Papa akitazama maadhimisho ya siku, alikumbusha kuwa mama Kanisa anamkumbuka kiliturujia Mtakatifu Nicola, Mtakatifu ambaye anaunganisha Mashariki na Magharibu, mchungaji wa Kanisa ambaye anatukumbusha Mtaguso wa Nikea ambapo Yeye alishiriki na kujikita na juhudi ya kutetea imani katika Umungu wa Kristo. Papa Francisko alisema, hata wao wachukue wito ambao aliutoa katika matazamio ya Maadhimisho ya Mtaguso wa Nikea ili uweze kuwakilisha mwaliko kwa Makanisa Yote na Jumuiya za Makanisa kuendelea na safari kuelekea Umoja unaonekana(Hata ra Spes non Confundit,17) na wala wasichoke kutafuta mitindo inayofaa kwa ajili ya kujibu kikamilifu kwa sala ya Yesu isemayo: “ Ili wote wawe kitu wamoja (Yh 17,21), Tusichoke, Papa alisisitza. Kwa kuhitimisha alisema Bikira Mtakatifu Odegitria, Msimamizi wa Sicilia, awasindikize daima safari yao. Amewabariki kwa moyo. Na tafadhali wasisahau kusali kwa ajili yake.