Tafuta

Papa kwa waandishi wa habari kuelekea Corsica:"Asante kwa huduma yenu"

Baada ya kupaa kutoka Roma,Papa Francisko aliwasalimia takriban waandishi 70,wapiga picha walioandamana naye katika ziara yake ya kitume hadi Ajaccio:"Ni safari fupi ya ndege,lakini nilitaka kuwasalimu na kuwashukuru kwa kazi yenu". Zawadi nyingi kwa Papa,ikiwa ni pamoja na sanamu ya Malaika iliyoharibiwa na matope kutoka parokia ya Valencia iliyoharibiwa na dhoruba Dana.

Na Salvatore Cernuzio – Mwakilishi wa Vatican huko Ajaccio

"Habari za asubuhi na asante kwa kuja!." Chini ya dakika ishirini baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Roma-Fiumicino, muda mfupi kabla ya kutua huko Ajaccio, mji mkuu wa Corsica, katika marudio ya ziara yake ya  47 ya Kitume, Papa Francisko alitaka kuwasalimia binafsi waandishi wa habari 67, na wapiga picha wanaoandamana naye kwa takriban saa kumi na mbili za safari kwenye kisiwa cha Mediterania.

Salamu kwa waandamanaji wa safari"

“Ninawatakia safari njema na asante sana kwa huduma yenu. Asante sana…”, Papa alisema hayo kwenye maikrofoni, akiwa na George Koovakad, Kardinali mpya tangu tarehe 7 Desemba 2024 na mratibu wa safari za Kipapa. "Ni safari fupi sana ya ndege - aliongeza  Papa Francisko kwamba - hatuwezi kuwa na mazungumzo ya kawaida lakini nilitaka kuja kutoa salamu na asante kwa kazi yenu. Asante!"

Zawadi kwa Papa

Kwa sababu ya muda na nafasi kuwa kuwa kidogo kwa  safari ya ndege - takriban saa moja na robo kwenye Ndege ya (Ita Airways Airbus A320 Neo), Papa Francisko hakukamilisha ziara ya kiutamaduni kati ya safu za viti ambapo amezoea kuwazungukia wote. Kile ambacho katika ziara zote za kitume, kiliwakilisha fna ursa ya kubadilishana salamu, vichekesho, maswali, maombi ya sala na waandishi wa habari na zaidi ya yote, kuwasilisha barua, vitabu na zawadi. Zawadi hizo hata hivyo ziliwasilishwa kwa Papa kupitia kwa msemaji  mkuu Matteo Bruni.

Sanamu ya Malaika kutoka Valencia iliyeharibiwa na dhoruba Dana

Kama kawaida iliyotolewa na mwandishi wa Radio Cope ya Hispania, Eva Fernandez, ilikuwapo kati ya zawadi hizo. Inajitokeza kwa ishara yake dhabiti na kwa kuja kutoka eneo la Ulaya ambalo lilipata moja ya janga mbaya zaidi la 2024 huko  Valencia. Hii ni sanamu ya Malaika iliyoharibiwa na matope asiye na kichwa na asiye na mbawa, lakini akiwa na mikono yake safi katika ishara ya kuabudu. Sanamu ya Malaika ilikuwa ni sehemu ya jozi (ya nyingine ambayo ilikuwa imeharibika sana kiasi cha kutotambulika)-inayotoka kwenye hema la Parokia ya Picanya, mojawapo ya maeneo yaliyoharibiwa zaidi na dhoruba ya Dana ambayo ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 200, wengine kujeruhiwa na watu wengi waliopotea na kuwepo kwa uharibifu usiohesabika.

Kwa kumbukumbu ya waathiriwa, wakujitolea na makuhani

Askofu wa eneo la mji mkuu wa Valencia, Jesús Corbí, alituma barua pamoja na zawadi ambayo alieleza kwa Papa kwamba sanamu hiyo inataka kuwa "kumbukumbu ya wale waliokufa katika mafuriko haya, ya familia nyingi ambazo zilipoteza kila kitu", lakini pia "ishara ya shukrani kwa waliojitolea wote ambao walitusaidia" na kwa makuhani "ambao walilia na kujihusisha na watu, kuomba, kusafisha, kutia moyo na kuzika wapendwa wao". "Mateso na kazi ya watu wetu ni ishara ya sala ili, tukitembea pamoja, tuwe mahujaji wa matumaini katika hali hii ya kushangaza" tunasoma katika barua kutoka kwa askofu ambaye pia alishukuru kwa ziara ya mwezi Novemba ya Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamaisha  Maendeleo  Fungamani ya Kibinadamu, huko Valencia na miji ya jirani ambako alileta ukaribu na upendo wa Papa.

15 December 2024, 10:24