Papa kwa Wanahija wa Santiago:Ninahiji na kurudi kama mtume kumtangaza Yesu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Makatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 19 Desemba 2024 amekutana na Wanahija wa Italia katika Hija ya Santiago nchini Hispania. Papa amewakaribisha katika Kaburi ya Petro. Hawa walikuwa ni kundi kubwa sana. Amemsalimia Askofu Mkuu Francisco Prieto Fernández, wa Santiago de Compostela. Mkuu wa Shirika la Mapadre wa Guanella na Wajumbe wa Familia nzima ya Guanella. Amewapongeza kuwa kwa karibu miaka 15 wanafanya kazi katika Kanisa lile la Galizia, la Santiago na la Finisterre, ili kutoa makaribisha ya kiroho wanahija. Wao kama wanahija kidogo ni jaribio hai kwa jitihada yao ya kitume. Baba Mtakatifu Francisko alisalimia hata udugu wa Mtakatifu Yakobo kutoka Perugia, Italia ambao walikuwapo hata Baba wao wa kiroho, Askofu Mkuu Paolo Giulietti wa Jimbo Kuu katoliki la Lucca; hata wao wanajikita katika huduma hiyo ya Uinjilishaji. Papa amesema kuwa inashangaza kuona jinsi ambavyo idadi imeongezeka ya wanahija kuelekea Santiago katika miaka 30 ya mwisho.
Na kati ya hawa pia walikuwepo watangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko kama Mtakatifu Yohane Paulo II na Benedikto XVI, ambapo Papa alisisitiza kwamba, walitaka kutembelea mahali Patakatifu, zaidi ya yote kwa umuhimu wake mkubwa katika historia ya Kikristo ya Ulaya. Ukuaji huu wa idadi ni ukweli mzuri sana, na wakati huo huo unaleta swali zito: je, watu wanaofanya Safari ya Santiago wanafanya hija ya kweli? Hili ndilo swali, na lazima tujibu. Au ni kitu kingine? Au ni wazi kuna uzoefu tofauti, lakini swali linatufanya tutafakari, Papa alisisitiza. Kwa kufafanua zaidi aliongeza kusema: “Tunaweza kutambua hija ya Kikristo kwenye Makaburi ya Mitume kwa ishara tatu. Ishara ya kwanza ni ni ukimya, kwa sababu alisema “Safari iliyoishi kwa ukimya inakuwezesha kusikiliza, hasa kwa moyo wako, na hivyo kupata, wakati wa kutembea, kupitia jitihada, majibu ambayo moyo unatafuta, kwa sababu moyo unauliza maswali.”
Na kwa hakika Mungu anazungumza kwa ukimya, kama upepo mwepesi: hebu tukumbuke histotia ya Eliya (rej. 1 Wafalme 19:9-13). Pili, Injili na lazima kuwa na Injili kila mfukoni. Papa Francisko ameisisitiza zaidi kuwamb: “Ninapendekeza hii, kununua Injili ndogo, yenye ukubwa wa mfuko na kuiweka mfukoni mwako na usome kitu, kila siku; kuifunga hivyo na kuisoma. Ni njia nzuri ya maombi. Injili ya mfukoni, haigharimu chochote, lakini ikiwa mtu hawezi kulipia, nitalipia, niombeni…. walicheka. Lakini ni muhimu kubeba Injili mfukoni mwako.” Hija inafanywa kwa kusoma tena safari ambayo Yesu aliichukua, hadi karama kuu yake mwenyewe. Njia ya kweli zaidi, ni ile ya Kikristo, ambayo zaidi inaongoza kwa kujitoa mwenyewe na kujitoa kwa uhuru, katika huduma kwa wengine.
Papa aliongeza kusema kuwa: Na Roho Mtakatifu hufanya hivyo tunaposoma Injili kila siku. Lakini je ni kwa nini jambo fulani linatokea, , Papa alieleza. “Tunaweza kusoma riwaya, nzuri, labda ni nzuri kwetu, kusoma habari za kila siku, nyingine zinatufanya tulie, lakini tunaweza kuzisoma; lakini tunaposoma Injili kuna mmoja aliye karibu nasi. Lakini tunapokuwa tunasoma habari, hayupo. Ni pale tu tunapokuwa tunasoma Injili kuna mtu aliye karibu nasi. Ni Roho Mtakatifu. Ni Yeye anayetufanya tuelewe vizuri kile ambacho Injili inafanya. Naye, Roho Mtakatifu, ambaye anafanya hivyo.” Baada ya kufafanua jambao la Kwanza la ukimya, pili, Injili na la tatu alisema ni, “Itifaki ya Mathayo 25”, yaani “kile mlichomtandea mmoja wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mt 25:40). Kwa njia hiyo Ukimia, kusoma Injili na kutenda mema, hata kwa watu walio wadogo kabisa, watu wasiojiweza. Daima ni kutendani wema.”
Njiani, kuwa makini na wengine, hasa wale wanaohangaika zaidi, wale ambao wameanguka, wale wanaohitaji... Mtakatifu Luigi Guanella alisema kuwa lengo la maisha ya wale wanaoamini ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma. Wapendwa wa Wanahija wa Santiago, Papa amewatia moyo katika utume wao wa uinjilishaji na makaribisho. Mahujaji wa kale wanatufundisha kwamba kutoka katika hija za Kikristo tunarudi kama mitume! Ninahiji na kurudi kama mtume kumtangaza Yesu. Familia Takatifu ya Nazareti, mhujaji katika ardhi ya Palestina, awe kielelezo kwetu katika wakati huu wa kusubiri. Papa amewashukuru kwa kufika kwao. Amewabariki kwa moyo na kuwaombea wakati huo huo akiwaomba nao wamwombee.