Papa kwenye hija Corsica,kati ya Udini Maarufu na changamoto za Mediteranea!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Ziara ya kitume ya Papa Francisko itaaanza Dominika tarehe 15 Desemba 2024 hadi huko Corsica, nchi ya asili ya Napoleon, "Île de beauté", kama inavyoitwa kuwa "kisiwa cha uzuri" na mandhari yake iliyopangwa na misitu, fukwe na milima, lakini hatari ya migogoro ya mazingira inayochochewa na binadamu. Hata hivyo kwa upande mmoja, ni ucha Mungu au udini maarufu, imani ya rahisi, iliyooneshwa katika safari, matendo ya ibada katika mahali patakatifu, maandamano na nyimbo za kiutamaduni. Kwa upande mwingine, Bahari ya Mediterania na changamoto zake, matukio ya vita, janga la ajabu la uhamiaji ambao umefanya Mare Nostrum, yaani Bahari yetu kuwa "makaburi ya wazi," ambayo Kongamano atakalofunga Papa litajikita na mada kama hizo.
Ni ziara ya 47 ya Kitume huko Corsica
Hii ni ziara ya 47 ya Kitume ambapo Jorge Mario Bergoglio anafikisha idadi ya nchi 67 zilizotembelewa, na hii ambayo itkuwa kwa siku moja tu ya masaa ikilinganishwa na hija ndefu ya mnamo Septemba hadi Kusini-Mashariki mwa Asia na Oceania. Chini ya masaa kumi na mbili ambayo pia yatamuona Papa Francisko ana kwa ana kwa takriban dakika arobaini akiwa na rais wa Ufaransa, Bwana Emmanuel Macron kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege kurudi Roma jioni.
"Francescu", Papa wa kwanza huko Ajaccio
Pia hii ni ziara ya kwanza ya Papa katika mji mkuu wa Ajaccio, lakini si ya Papa wa baadaye ikizingatia ile ya Angelo Roncalli, ambaye baadaye alikuja kuwa Papa JYohane XXIII, wakati kakiwa ama Balozi wa Vatican jijini Paris alipotembelea kisiwa hicho mnamo mwaka 1952. Huu ni ukweli wa kihistoria uliokumbukwa na Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, katika mkutano wa kawaida na waandishi wa habari watakaomfuata na Papa Francisko katika ziara yake ya kimataifa. Kwa mujibu wa Dk Bruni alisema kuwa: "Papa anasonga mbele kukutana na Wakristo wa kisiwa hicho na kwa mkutano wa watu udini maarufu wa Watu."
Papa atahutubia hotuba tatu
Kwa kurejea Mada ya Kongamano la “de La religiosité populaire en Méditerranée,” ambayo ni hafla ya siku mbili iliyoandaliwa na Askofu wa Ajaccio, Kardinali François-Xavier Bustillo, ambayo itashuhudia uwepo wa washiriki zaidi ya 400, wakiwemo maaskofu wa Hispania, Ufaransa, Italia, wasomi, na wawakilishi wa maeneo mengine yanayoelekea Mediterania. Papa Francescu atawahutubia - kama inavyoweza kusomwa katika nembo ya bluu ya ziara hiyo, katika lugha ya Kikorsika - katika hotuba yake ya kwanza kati ya tatu (zote kwa Kiitaliano) ambazo zitafunga Kongamano hilo. Heshima kwa "Madonnuccia yaani “Mama" ambaye alikomboa kisiwa kutokana na janga la tauni, itakuwa tafakari juu ya mada ya udini maarufu ambayo inasikika sana Ufaransa yo," alisema Bruni.
Asilimia 80 ya wakati ni wakatoliki na ibada ya Maria inasikika sana
Hii hasa katika Corsica, ambapo 80% ya wakazi ni Wakatoliki na ambapo kuna udugu na ibada ya "Madonnuccia",Mama Bikira Maria ambaye kunako mwaka 1656 alikilinda kisiwa hicho, kisha chini ya utawala wa Genoese, kutokana na tauni, na kubadilisha mwendo wa upepo ambao ulizuia meli zilizobeba wagonjwa kutia nanga katika Ajaccio. Muujiza, huo kulingana na maelezo ni kwamba ulizuia kuenea kwa janga kwenye kisiwa hicho.
Papa atasali mbele ya picha na kuwasha mshumaa
Tangu wakati huo "Madonnuccia" yaani Bikira maria imekuwa ikiheshimiwa kama mtakatifu Msimamizi na mlinzi na sherehe kubwa imetolewa kwake katikati ya Mwezi Machi kila mwaka. Picha ya Mamama, iliyopo kwenye nembo, itaambatana na ziara ya upapa. Papa atatoa heshima kwa sanamu ya Marian "kwa muda wa kutafakari" na kuwasha mshumaa, katikati ya njia kati ya umati wa watu ambao utampeleka kwenye maeneo mbalimbali ya matukio.