Papa kwa shukrani:mji wa Roma uwe ujenzi wa Udugu na kukaribishe wote!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Sasa ni saa ya kushukuru na ambayo tunayo furaha ya kuiishi tukiadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Yeye ambaye analinda katika moyo wake fumbo la Yesu, anatufundisha hasa sisi kusoma ishara za nyakati kwa nuru ya fumbo hili. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko alianza tafakari yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Jumanne jioni tarehe 31 Desemba 2024 wakati wa Masifu ya kwanza ya jioni ya Mkesha wa Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, na Shukrani kwa Mungu(TE DEUM) sanjari na Siku Kuu ya Amani Ulimwenguni, inayoadhimisho kila tarehe Mosi ya kila Mwaka.
Aliongozwa na somo lililosomwa kutoka barua ya Mtakatifu Paulo kwa (Wagalatia 4,4-5) ambapo Baba Mtakatifu kwa njia hiyo akiendelea alisema kuwa Mwaka ambao tunaofunga umekuwa mwaka mgumu katika mji wa Roma. Wazalendo, mahujaji, watalii na wale ambao walikuwa wanapitia, walifanya uzoefu wa aina hiyo ya hatua ambayo iliyotangulia Jubilei, kwa kuongezeka kazi kubwa na ndogo. Papa aliongeza “katika jioni hii ni wakati wa kutafakari kihekima, kwa kuzingatia kazi hiyo yote, zaidi ya thamani ambayo inachukua yenyewe, imekuwa na maana ambayo inaendana na wito hasa wa Roma, wito wake wa Ulimwengu.
Katika nuru ya Neno la Mungu ambalo limesikika, wito huo unaweza kufafanuliwa namna hii: “Roma inaitwa kukaribisha wote kwa sababu wote wanaweza kujitambua kuwa wana wa Mungu na ndugu kati yao.” Kwa njia hiyo, katika wakati huu, Papa alisema: "tunataka kuinua shukrani zetu za asante kwa Bwana kwa sababu ameturuhusu kufanya kazi, na kufanya kazi, hasa kwa sababu alitupatia tufanye hilo kuwa na maana kubwa, kwa upeo huo mkubwa ambao ni “Matumaini ya Udugu.”
Kauli mbiu ya Jubilei ya“Mahujaji wa Matumaini” imejaa utajiri mkubwa kwa maana ambayo inaendena na uwezekano tofauti wa matarajio, ambayo ni kama njia zinazopishana za kuhiji. Moja ya njia hizo kubwa za tumaini ya kutembelea, ni Udugu. Ni njia ambayo Papa alisema kuwa aliipendekea katika Waraka wake wa kitume wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu. Ndiyo, tumaini la ulimwengu lipo katika udugu! Na ni nzuri kufikiria kwamba Mji wetu katika miezi iliyopita umekuwa sehemu ya ujenzi kwa kusudi hili, kwa maana hiyo kwa ujumla: kujiandalia kukaribisha wanawake na wanaume wa ulimwenguni pote, wakatoliki na wakristo wa madhehebu mengine, waamini wa kila dini, watafutaji wa ukweli, wa uhuru, wa haki na wa amani, wote ni wanahija wa matumaini na wa udugu.
Baba Mtakatifu kadhalika alisisitiza kuwa: “Lakini tunapaswa kujiuliza: haya matarajio yana msingi? Matumaini ya ubinadamu kidugu ni kauli mbiu tu ya kurudia au ina msingi wa jiwe? ambapo inawezekana kujenga kitu chenye msimamo na kudumu? Jibu linatolewa na Mtakatifu Mama wa Mungu kwa kutuonesha Yesu. Matumaini katika Ulimwengu wa kidugu siyo itikadi, siyo mfumo wa kiuchumi, na siyo maendeleo ya kiteknolojia. Matumaini ya Ulimwengu wa kidugu ni Yeye, Mwana aliyefanyika Mwili, aliyetumwa na Baba ili wote tuweze kugeuka kuwa kile ambacho sisi ni, yaani Wana wa Baba ambaye yuko mbinguni na kwa hiyo kaka na dada karibu yetu.
Kwa njia hiyo, Papa Francisko amesisitiza kuwa wakati tunashangaa kwa shukrani, matokeo ya kazi iliyofanyika katika mji, tushukuru kazi ya wengi, wanawake na wanaume ambao wametengeneza na kumshukuru Meya (Roberto Gualtieri aliyekuwapo miongoni mwa viongozi wa serikali ya Italia) kwa kazi ya kupeleka mji mbele. Tuwe na dhamiri ambapo ilikuwa ujenzi stahiki, ujenzi ambao uliwahusu kila mmoja wetu: ni ule ambao kila siku, nitamruhusu Mungu abadili ndani mwangu kile ambacho sisitahili kuitwa mwana, yaani ambacho siyo cha kibinadamu, na ambapo nitajitahidi, kila siku kuishi kama kaka na dada wa karibu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko alisema kuwa: “Mtakatifu Mama yetu, atusaidie kutembea pamoja, kama mahujaji wa matumaini, katika njia ya udugu.” Bwana atubariki sisi sote na kutusamehe dhambi na kutupatia nguvu kwa ajili ya kwenda mbele ili kwenda mbele katika hija kwa mwaka ujao. Asante."