Tafuta

Papa ametoa wito wa kuacha vita hata wazo kwa Siria na Ukraine kwamba watu wanateseka hata wanapokabiliwa na majira ya baridi kali. Papa ametoa wito wa kuacha vita hata wazo kwa Siria na Ukraine kwamba watu wanateseka hata wanapokabiliwa na majira ya baridi kali.  (ANSA)

Papa atoa wito na kusitisha vita vya kutisha na kuwa ni chukizo kwa Mungu

Papa Francisko ametoa wito mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,Dominika ya I ya Majilio kwa Jumuiya ya kimataifa kufanya kazi ili kukomesha migogoro.Papa amekumbusha mfano wa Argentina na Chile ambao walizuia kuzuka kwa vita kwa njia ya mazungumzo,pia ameonesha furaha ya usitishaji wa mapigano nchini Lebanon, akitumaini kuwa mapatano yatadumu na pia yanaeweza kuenea hadi Gaza ambapo idadi ya watu imechoka na vita hivyo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Doiminika ya Kwanza ya Majilio, tarehe Mosi Desemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro amesema: “Katika siku za hivi karibuni maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Amani na Urafiki kati ya Argentina na Chile yaliadhimishwa. Kwa upatanisho wa Vatican mzozo wa eneo ulimaliza ambao ulileta Argentina na Chile kwenye ukingo wa vita. Hii inaonesha kwamba tunapoachana na matumizi ya silaha na kushiriki katika mazungumzo, tunakuwa kwenye njia nzuri. Ninakaribisha usitishaji vita uliofikiwa katika siku za hivi karibuni nchini Lebanon na ninatumaini kwamba unaweza kuheshimiwa na pande zote, na hivyo kuruhusu wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na mzozo wote wa Lebanon na Israel kwa kuruhusu kurejea kwa haraka na usalama nyumbani, pia kwa msaada mkubwa wa Jeshi la Lebanon na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.”

Wito kwa Jumuiya ya kimataifa

Katika hali hii, ninatoa mwaliko mkubwa kwa wanasiasa wote wa Lebanon, ili Rais wa Jamhuri achaguliwe mara moja na taasisi zirejeshe utendaji wake wa kawaida, kuendelea na mageuzi yanayohitajika na kuhakikisha jukumu la nchi kama mfano wa kuishi kwa amani kati ya nchi, dini mbalimbali. Baba Mtakatifu akiendelea alisema kuwa: “Ni matumaini yangu kuwa mwanga wa amani ambao umefunguka unaweza kusababisha usitishaji vita katika nyanja nyingine zote, hasa huko Gaza. Ninajali sana juu ya ukombozi wa Waisraeli ambao bado wanashikiliwa mateka na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Palestina waliochoka.”

Tuiombee Siria na Ukraine

Papa Francisko ameomba: “tunaiombee Siria, ambako kwa bahati mbaya vita vimetawala na kusababisha wahanga wengi. Niko karibu sana na Kanisa la Siria. Hebu tuombe! Ninaonesha wasiwasi wangu, maumivu yangu, kwa mzozo ambao unaendelea kumwaga damu ya Ukraine inayoteswa. Kwa takriban miaka mitatu tumekuwa tukishuhudia mlolongo wa kutisha wa vifo, majeraha, vurugu na uharibifu.” Baba Mtakatifu kwa kuongeza alisema “Watoto, wanawake, wazee, wanyonge ndio waathirika wa kwanza. Vita ni jambo la kutisha, vita humchukiza Mungu na ubinadamu, vita haimwachi mtu yeyote, vita daima ni kushindwa, kushindwa kwa wanadamu wote!” Na tufikirie kwamba majira ya baridi yametufikia na hatari ya kuzidisha hali za mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao. Hii itakuwa miezi migumu sana kwao. Kuendelea kwa vita na baridi ni vya kusikitisha. Kwa mara nyingine tena ninatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na kwa kila mwanamume na mwanamke mwenye mapenzi mema, kufanya kila awezalo ili kukomesha vita hivi na kufanya mazungumzo, udugu na maridhiano kutawala.”

Tunapojiandaa na Noeli tuwape watu amani

Papa amekazia kusema kuwa “Ahadi iliyofanywa upya iongezwe katika kila ngazi. Na tunapojiandaa na Noeli, tunapongojea kuzaliwa kwa Mfalme wa Amani, watu hawa wapewe tumaini thabiti. Kutafuta amani ni jukumu, si la wachache, bali la kila mtu.” “Ikiwa kutojali na mambo ya kutisha ya vita yatatawala, familia nzima ya kibinadamu inashindwa…. Familia nzima ya kibinadamu imeshindwa!” Papa amesisitiza kuwa, “tusichoke kuombea watu hao waliojaribiwa vikali na kumwomba Mungu zawadi ya amani.”

Salamu

Papa aendelea kutoa salamu kwamba “ Ninawasalimu ninyi nyote kwa upendo, waamini wa Roma na mahujaji waliotoka Italia na nchi mbalimbali. Hasa, ninawasalimia vikundi kutoka Barcelona, ​​​​Murcia na Valencia, na tufikirie Valencia, jinsi inavyoteseka! na kutoka Gerovo huko Kroatia.Ninawasalimu waamini wa Arco ya Trento na wale wa Sciacca, na kundi la Kirumi la Vijana Wakereketwa wa Maria. Na ninawasalimu watoto wa Maria Mkingiwa. Ninawatakia wote Dominika Njema  na  mwanzo mwema wa Majilio. Tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kukuona!

Papa baada ya Angelus
01 December 2024, 13:20