Tafuta

Papa:Tujikabidhi kwa Mungu wa tumaini badala ya vita na upotoshwaji wa kidigitali!

Kabla ya Sala ya Malaika katika Siku Kuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili,Papa aliakisi juhudi kubwa za kumiliki na kutawala, uchu wa pesa na kuwa marafiki wenye nguvu,mifano ya uwongo inayo metameta hutoka katika vyombo vya habari na mitandaoni.Ushauri wake ni kujiachia katika unyenyekevu wa huruma ya Baba,kama Bikira alivyoitikia kuwa:'Tazama mimi hapa'kwa Malaika Mkuu Gabrieli.Leo ni siku nzuri ya kuungama kwa sababu Bwana anasamehe yote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakaifu Francisko, mara baada ya Misa Takatifu, alielekea katika Dirisha la Jumba la Kitume kwa ajili ya Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 8 Desemba 2024. Papa Francisko akianza tafakari yake aliwatakia kila la baraka ya sikukuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili na kwamba Injili inasimulia vipindi muhimu vya historia ya ubinadamu wakati Malaika Gabrieli alimtangazia Maria kuwa atachukua mimba ya Mtoto wa Mungu, Yesu (Lk 1,26-38). Ni tukio ambalo linaamsha ajabu na hisia kubwa zaidi kwa sababu Mungu, Aliye Juu Zaidi, Mwenyezi, kupitia Malaika anazungumza na msichana mdogo kutoka Nazareti, akiomba ushirikiano wake kwa ajili ya mpango wake wa wokovu. Papa Francisko ametoa ushuri: “Ukipata muda leo, tafuta Injili ya Mtakatifu Luka na usome tukio hili. Ninakuhakikishia kwamba itakufaa, vizuri sana!”

Waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana

Kama katika tukio la uumbaji wa Adamu lililochorwa na Michelangelo katika Kikanisa cha Sistine, ambapo kidole cha Baba wa mbinguni kinagusa kile cha mwanadamu; kwa hivyo hapa pia, wanadamu na wa kimungu wanakutana, mwanzoni mwa Ukombozi wetu, "wanakutana na utamu wa ajabu," katika wakati uliobarikiwa ambapo Bikira Maria alitamka "ndiyo, tazama mimi hapa." Yeye ni mwanamke kutoka mji mdogo wa pembeni na anaitwa milele katikati ya historia: hatima ya ubinadamu inategemea majibu yake, ambayo yanaweza kutabasamu na kutumaini tena, kwa sababu hatima yake imewekwa katika mikono nzuri. "Atamleta Mwokozi, aliyechukuliwa mimba kwa Uwezo wa  Roho Mtakatifu."

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Kwa hiyo Maria, aliposalimiwa na Malaika Mkuu Gabrieli kuwa, "amejaa neema" (Lk 1:28), Msafi, kabisa katika huduma ya Neno la Mungu, na daima pamoja na Bwana, ambaye anajikabidhi kwake kikamilifu. Papa alisema “Hakuna kitu ndani yake kinachopinga mapenzi yake, hakuna kitu kinachopinga ukweli na upendo. Hapa kuna furaha yake, ambayo vizazi vyote vitaimba. Tufurahi kwa Sababu Mkingiwa Dhami ya Asili  a iltupatia Yesu ambaye ndiye wokovu wetu! Papa Francisko aidha alisema, tukitafakari fumbo hili tunaweza kujiuliza: katika wakati wetu, tukichochewa na vita na kujikita katika juhudi za kumiliki na kutawala, je ninaweka wapi tumaini langu? Kwa nguvu, kwa pesa, kwa marafiki wenye nguvu? Je, ninaweka matumaini yangu hapo? Au katika huruma ya Mungu isiyo na kikomo? Na ninapokabiliwa na mifano mingi ya uwongo ya kumetameta inayozunguka kwenye vyombo vya habari na kwenye mtandao, ninatafuta wapi furaha yangu? Iko wapi hazina ya moyo wangu? Je, ni katika ukweli kwamba Mungu ananipenda kwa hiari, kwamba upendo wake daima hutangulia mbele yangu, na je, yuko tayari kunisamehe ninapomrudishia toba yangu?

Tafakari ya Papa kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana
Tafakari ya Papa kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana

Na  "Katika tumaini hilo la kimwana katika upendo wa Mungu?" Au je, ninajidanganya katika kujaribu kujidai nafsi yangu na mapenzi yangu kwa gharama yoyote ile? Kwa njia hiyo Papa Francisko amesema “kaka na dada  wakati ufunguzi wa Mlango Mtakatifu wa Jubile unakaribia, tufungue milango ya mioyo na akili zetu kwa Bwana aliyezaliwa na Maria asiye na do ana  tuombe maombezi ya Maria. Aidha alitoa ushauri kuwa “ Nami nitakupa ushauri. Leo ni siku nzuri ya kuamua kufanya Kuungama vizuri. Ikiwa huwezi kwenda leo hii, Juma hili, basi  hadi Dominika  ijayo, ufungua moyo wako na Bwana anasamehe kila kitu, yote!. Na hivyo katika mikono ya Maria tutakuwa na furaha zaidi.” Alihitimisha Papa

08 December 2024, 14:20