Tafuta

2024.12.04 Wata wa Shirika la Familia Takatifu ya Nazareh wakiadhimisha miaka 150 ya kuanzishwa kwa shirika. 2024.12.04 Wata wa Shirika la Familia Takatifu ya Nazareh wakiadhimisha miaka 150 ya kuanzishwa kwa shirika.  (Vatican Media)

Papa,Watawa wa Familia Takatifu ya Nazareth:kukua katika imani ya tafakari kwa Mwana wa Mungu!

Kupitia mioyo iliyofunguliwa kwa Bwana na kwa mkutano wa kweli na wa kibinafsi na Bwana Yesu,‘mlango’ wa wokovu wetu,Jumuiya zenu na ziwe 'vizingiti daima' ndani na kwa njia ambayo ni lengo la karama ya familia zenu ambazo zinaweza kupata kimbilio,tumaini na amani katika Kristo Mwokozi wetu.Ni ushauri wa Papa akikutana na Shirika la Familia Takatifu ya Nazareth tarehe 4 Desemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatato tarehe 4 Novemba 2024 amekutana na watawa wa Shirika la Familia Takatifu ya Nazareth , ambapo katika hotuba yake Papa amewakaribisha katika fursa ya mwanzo wa maadhimisho ya miaka 150 ya Shirika lao. Papa Francisko amesema kuwa wanapoadhimisha tukio hilo muhimu, nimatumaini yake kwamba itakuwa fursa kwao kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema nyingi zilizopokelewa katika historia yao, na kwa kila mmoja wao kupyaishwa kiroho katika utumishi wa furaha kwa Bwana. Inafaa kuona ni kwa jinsi gani kwamba kumbukumbu yao imeanza mwanzoni mwa mwaka mpya wa kiliturujia, katika kipindi cha Majilio, pamoja na tarajio lake la subira na lililojaa matumaini katika ahadi za Bwana, ambalo linaweza kutumika kama kielelezo cha kutuwezesha kukuza imani kubwa zaidi katika majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Papa Francisko kwa njia hiyo ameomba kuwa, maadhimisho yao yawasaidie washiriki wa Shirika lao, na wote wanaosaidia katika utume wake  mbalimbali, kukua katika imani ya tafakari kwa Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili, hasa katika Sakramenti Takatifu na kwa watu wanaowahudumia.

Papa Francisko amekutana na watawa wa Shirika la Familia Takatifu ya Nazareth
Papa Francisko amekutana na watawa wa Shirika la Familia Takatifu ya Nazareth

Kwa kuongezea, Baba Mtakatifu alisema kuwa “Wakati huo huo, Jubilei yenu wenyewe kwa furaha inakwenda sambamba na Mwaka Mtakatifu ambao Kanisa zima linakaribia kuanza. Jubilei ni nyakati za thamani za kutathmini maisha yetu, kama watu binafsi na kama jumuiya. Zaidi ya hayo, ni fursa za kutafakari, kukumbuka, na kusikiliza kile ambacho Roho Mtakatifu anatuambia leo (rej. Ufu 2:7).” Kwa njia hiyo Papa alisisitiza kwamba “Kupitia mioyo iliyofunguliwa kwa Bwana na kwa mkutano wa kweli na wa kibinafsi na Bwana Yesu, ‘mlango’ Yh 10:7.9) wa wokovu wetu, ( Spes Non Confundit, 1),  Jumuiya zenu na ziwe 'vizingiti daima' ndani na kwa njia ambayo ni lengo la karama ya familia zenu  ambazo zinaweza kupata kimbilio, tumaini na amani katika Kristo Mwokozi wetu.

Papa na watawa wa shirika la Familia Takatifu ya Nazareth
Papa na watawa wa shirika la Familia Takatifu ya Nazareth

Kuhusiana na hilo Papa amekazia kusema kuwa: “ hatuwezi kukosa kukumbuka familia nyingi katika siku zetu ambazo zimeharibiwa na vita na jeuri au kuhamishwa ndani au kutoka katika nchi zao. Maombi yenu na matendo yenu ya upendo yaakisi daima upendo wa Yesu, ili muwe ishara za matumaini kwa wale wanaopatwa na magumu ya aina yoyote.” Kwa kuhitimisha Papa amewahakikishia maombi yake kwamba Familia Takatifu ya Nazareti itaendelea kuwa kielelezo chao thabiti katika shughuli zao zote, anawaombea kwa hiari ninyi ameapatia  baraka za Mwenyezi Mungu za utulivu wa furaha. Ameomba pia wasali kwa ajili yake.

Papa akutana na Watawa Familia Takatifu

 

04 December 2024, 09:44