Salamu za siku ya kuzaliwa kwa Papa kutoka kwa Rais Mattarella na CEI
Vatican News.
Wakati milipuko mingi ya vita, hata katika maeneo ya karibu na Italia, inaendelea kusababisha maombolezo na kusambaratisha mfumo wa kijamii wa jumuiya nzima, maneno yake na wito wake ni, kwa waamini na wasioamini, hatua maalum ya kutazama kila wakati kwa uchungu mwingi au kutotulia kwa karibu. Rais wa Jamhuri ya Italia Sergio Mattarella aliandika hayo katika ujumbe kwa Papa Francisko wakati wa siku yake ya kuzaliwa tarehe 17 Desemba 2024 ambapo ametimiza miaka 88, na kumtakia heri nyingi. Mkuu wa Nchi ya Italia alisisitiza kwamba Papa Francisko, katika mahubiri yake ya ujasiri, shughuli nyingi na nzito za kichungaji na ziara nyingi za kitume, ameshuhudia hamu ya kila mtu ya maisha ya kila siku akiishi kwa amani na maelewano, kwa ishara ya uhuru, mshikamano, kuheshimiana na anakumbuka onyo lililooneshwa katika Barua yake ya Kitume ya Dilexit nos ambayo anataka kusisitiza utu wa mwandamu usitegemee vitu vinavyopatikana kwa nguvu ya pesa. Hatimaye, akikumbuka kauli mbiu ya Jubilei ijayo: “Matumaini hayakatishi tamaa” ambapo muda si mrefu utafunguliwa Mlango Mtakatifu, Juma lijalo Rais, Mattarella anatumaini kwamba kila mtu anaweza kufanya uchaguzi wa ujasiri kwa haki na manufaa ya wote.
Kukumbatiwa kwa Kanisa la Italia
Kwa upande Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia pia alituma salamu zake za heri na Baraka kwa Baba Mtakatifu na kumwambia wazo la upendo, na huku akikumbatiwa na jumuiya zote za kikanisa na kumhakikishia ukaribu na sala ya Makanisa nchini Italia. Baraza la Maaskofu Italia linabainisha kuwa mara kadhaa katika Upapa wake alitukumbusha umuhimu wa moyo, na kwamba mwaka huu alitupatia Waraka wa Dilexit nos, dira ya kweli kwa ulimwengu wetu ambao unaonekana kupotea njia na hivyo Maaskofu wa Italia wanaonesha nia yao ya kujitolea kurejea kwenye kiini, ili kugundua tena nguvu inayosukuma ya wema unaobubujika kutoka moyoni; kwa kujifunza kutoka kwa Kristo, Mungu aliyechagua upole na udhaifu wa mtoto ili kubuni upya upendo ambapo uwezo wa kupenda unazidiwa na ubinafsi, uovu na dharau na kuwa na usikivu wa watu ambao wakati mwingine ni vigumu kupata sababu za kusonga mbele na kuendelea kuwa na matumaini. Nia ni kuwabeba mioyoni mwetu wale wote walio pembezoni, wasio na sauti, wanaopata upweke, kukata tamaa, kuteseka na"kuishi Jubilei kwa utimilifu na kulifanya Kanisa la Italia kuwa la kimisionari zaidi na zaidi, kukaribisha zaidi, kwani inahitaji Njia ya Sinodi ya Kitaifa. Walikumbuka maneno yake ya Ushauri kwa Kanisa la Italia.
Shukrani kutoka kwa Vicariate ya Roma
Shauku ya upendo na uchangamfu pia ilitoka Vikarieti ya Roma, ambapo ujumbe uliotumwa uliotiwa sahihi na Kardinali Baldassare Reina, ambaye aliomba baraka nyingi kutoka kwa Bwana juu ya Papa na juu ya huduma ambayo anafanya kwa upendo na kujitolea katika Kanisa la Roma na jumuiya yote ya waamini, kwa shukrani za dhati, anatoa shukrani kwa mafundisho yake yenye mwanga, ambayo yanathibitisha kuwa ni zawadi ya thamani na chemchemi ya matumaini kwa Kanisa na kwa ajili ya binadamu ambayo mara nyingi huwa na migawanyiko, migogoro na mateso. Katika kufanya upya dhamira yetu ya kuwatumikia maskini na wasiojiweza tunatiwa moyo na mfano wako mzuri na ushuhuda wako usio na kuchoka wa imani na mapendo,” anahitimisha Kardinali, Reina.