Papa atuma ujumbe kwa Washiriki wa Kongamano la II la Ekaristi,Rwanda
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Ujumbe uliolekezwa kwa Askofu Vincent Harolimana, wa Jimbo la Ruhengeri,na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Rwanda (CEPR) kwa ajili ya Kongamano la II la Ekaristi Takatifu kitaifa lililoanza tarehe 4 hadi 8 Desemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko anaungana kwa furaha na shukrani za waamini wote wa Kikristo katika Nchi hiyo ya Afrika. Ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Papa anasisitiza juu ya uwajibikaji kwa kukabiliana na njia ya kimwili na hadhi ya binadamu.
Akitazama Kaulimbiu ya Kongamano hilo isemayo: “Tumkazie macho Yesu katika Sakramenti ya Ekaristi: chemchemi ya matumaini, udugu na amani” Papa Francisko amebainisha kuwa inatoa fursa ya kutafakari Ushirika, ambao ni kitovu cha maisha yote ya Kikristo na ishara inayoshikika ya upendo wa Kristo kwa wanadamu wote." Kwa njia hiyo kwa kuiishi, kulingana na Papa Francisko, inatuhimiza kujitoa kama zawadi kwa wengine, huku tukifanya kazi kwa makubaliano ya pamoja kujenga ustaarabu wa upendo.”
Kwa kuzingatia Jubilei ya miaka 125 tangu uinjilishaji ulipoanza nchini Rwanda, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wote nchini humo kuanza tena kwa “Kristo, mkate wa uzima”, huku akisisitiza kuonesha mshikamano kwa yeyote anayejikuta katika mazingira magumu.” "Ni lazima tuwe ishara dhahiri za tumaini," kwa kuchukua maneno kutoka katika Hati iliyotangaza Mwaka mtakatifu, 2025 ya Spes non confundit,” yaani Matumaini hatakatishi tamaa. Baba Mtakatifu aidha alibainisha " Ekaristi inakumbusha wajibu wa kawaida kuelekea mahitaji ya kimwili na ya kiroho ya binadamu, huku ikichochea matumaini katika Utatu." Asili yake "kimsingi ya uhusiano inaalika watu kuishi katika jumuiya, badala ya kutengana. Na kwa hiyo kuishi Umoja, kuvunja vizuizi vya kikabila, lugha utamaduni, alihitimisha.