Tafuta

2025.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana. 2025.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko ametoa wito wa serikali kufuta au kupunguza madeni ya nchi maskini

Katika maombi ya Papa baada ya sala ya Malaika wa Bwana yameelekezwa kwa viongozi wa kisiasa hasa wa mapokeo ya Kikristo kuwa mfano mzuri wa kutekeleza kielelezo kilichopendekezwa na Siku ya Amani Duniani kwa kielelezo cha kijamii,pamoja na maana ya Jubilei kuhusu msamaha wa madeni.Papa ametoa shukrani mwanzoni mwa 2025, kwa wote wanaofanya kazi ya mazungumzo katika maeneo ya migogoro kwa ajili ya amani.Amemshukuru Rais Mattarella kwa salamu zake

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ndugu wapendwa, wote na Warumi na mahujaji na wale wote wanaofuatilia kupitia vyombo vya habari, ninawatakia kila la kheri kwa mwaka mpya. Ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Italia kwa kumbukumbu katika ujumbe wake kwa Taifa na ninajibu kwa moyo mkunjufu kumhakikishia maombi yangu. Heri ya Mwaka Mpya, Mheshimiwa Rais! Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko alianza kusema mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana Jumatano tarehe Mosi Januari 2025 akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican. Papa aliendelea kusema kuwa: “Papa Mtakatifu Paulo VI alitaka siku ya kwanza ya mwaka iwe Siku ya Amani Duniani. Mwaka huu ina sifa, kutokana na Jubilei, kwa mada ya kipekee: ile ya msamaha wa madeni. Wa kwanza kusamehe madeni ni Mungu, kama sisi daima tunamwomba katika sala ya "Baba yetu," ikimaanisha dhambi zetu na kujitolea wenyewe kuwasamehe wale ambao wametukosea.

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Kwa njia hiyo “Na Jubilei inatutaka tutafsiri msamaha huu katika kiwango cha kijamii, ili pasiwepo na mtu, pasiwepo na  familia,pasiwepo na  watu wanaokandamizwa na madeni. Kwa hiyo Papa ameongeza “ninawahimiza watawala wa nchi zenye mtamaduni za Kikristo kuonesha mfano mzuri kwa kufuta au kupunguza madeni ya nchi maskini zaidi iwezekanavyo. “Ninawashukuru kwa maombi na mipango yote ya kujitolea kwa ajili ya amani inayoendelezwa kila sehemu ya dunia na jumuiya za kijimbo na parokia, na vyama, harakati na vikundi vya kikanisa, kama vile Maandamano ya Kitaifa ya Amani yaliyofanyika jana huko Pesaro,” nchini Italia

Waamini katika katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Papa amewasalimu washiriki wa hafla ya "Amani katika nchi zote" iliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika nchi mbalimbali. Amewasalimia Jumuiya ya Mtakatifu 'Egidio, aliowaona katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Papa ametoa shukrani zake kwa wale wote wanaofanya kazi kwa ajili ya  mazungumzo na mazungumzo katika maeneo mengi ya migogoro. “Tuombe kwamba mapigano katika kila nyanja yakome na kwamba amani na upatanisho vielekezwe kikamilifu.” Papa kama kawaidia amefikiria Ukraine, Gaza, Israel, Myanmar, Kivu na watu wengi wanaoteswa vitani. Akielezea alivyoona filamu na picha za uharibifu uliosababishwa na vita kwenye programu "ya Picha Yake."(Hiki ni kipindi kitolewacho katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Italia (TV2000). Papa amesema “ Kaka na dada, vita huharibu, huharibu daima! Vita daima ni kushindwa, daima.”

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu kadhalika aliwasalimu wote tena, Warumi na mahujaji, hasa bendi za muziki za baadhi ya shule za Marekani: kutoka Michigan, California, Oklahoma na North Carolina. “Asante kwa muziki wenu! Kama vile ninavyowasalimu waamini wa Pontevedra, Hispania, na wajitoleaji wa Udungu wa Domus. Amewasalimu watoto wa Parokia ya Mkingiwa dhambi na kuwaomba wapambanie amani. Hatimaye aliwatakia wote mwanzo mwema wa mwaka, kwa baraka za Bwana na Mama Bikira. Tafadhali wasisahau kumuombea. Mlo Mwema, mchana mwema na kwaheri ya kukuona!

Barua ya rais Mattarella kwa Papa

Rais wa Jamhuri, ya Italia Bwana Sergio Mattarella, tarehe 1 Januari 2025  alituma ujumbe  kwa Baba Mtakatifu Francisko, ikiwa ni Siku ya Amani duniani. Katika ujumbe huo anaandika kuwa "Baba Mtakatifu, ningependa kutoa shukrani za shukrani kwako, kwa niaba ya Jamhuri ya Italia na mimi mwenyewe, kwa ujumbe wako "Utusamehe makosa yetu, utupe amani yako." Uchambuzi unaoufanya katika hafla hii ya Siku ya 58 ya Amani Duniani unatilia shaka dhamiri ya kila mwanamke na kila mwanaume mwenye mapenzi mema. Kila mtu, Wakuu wa Nchi na Serikali, wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, mamlaka za kiraia na za kidini wanaitwa kushughulikia majeraha ya ulimwengu, na mgawanyiko unaotia wasiwasi wa kijamii na kiuchumi, na kuongezeka kwa vitisho kwa maendeleo ya amani kati ya Mataifa.

Rais Matarella anabainisha kuwa: “Ni utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria zinazotambuliwa na halali kwa wote walio katika hatari, kutokana na mipango ya uharibifu inayofanywa na watendaji wa serikali na wasio wa serikali. Ni Sheria, ulinzi wa kuishi pamoja kati ya watu na nchi, ambayo inakiukwa. Ni - mara nyingi zaidi na zaidi - heshima ya mtu imeharibika. Mwanzoni mwa mwaka wa Jubilei ambayo imezinduliwa hivi karibuni, mada iliyochaguliwa kwa ajili ya ujumbe inasisitiza ipasavyo hitaji la mabadiliko ya kiutamaduni ambayo huturuhusu kututambua sisi sote kama "wadeni" na, kwa hivyo, muhimu kwa kila mmoja wetu.”

Mustakhabali wa ubinadamu

Rais anabainisha kuwa "Ufahamu huu ungetosha kusababisha utafutaji - wenye mantiki zaidi, wenye busara, wenye kuona mbali - wa vichocheo vya mshikamano, huku tukiona jinsi vurugu, unyonyaji na tofauti zinavyofunika matarajio ya mamilioni ya watu katika mabara yote. Kaka Papa alivyotarajia kwa 2025  kuwa "uwe mwaka ambao "amani inakua" na kwamba Papa anapendekeza ishara za haraka na za ujasiri. Ni juu ya kila mtu, kibinafsi na katika muktadha wa marejeo ya kijamii, kukubali mwaliko huu wa kuamini katika mazungumzo na amani, kufanya zaidi ili kudhibiti kwa ufanisi hali ya kimuundo ya uhamiaji, uharibifu wa mazingira, hatari na fursa zinazohusiana na teknolojia mpya.

Mandhari yote ambayo yanaathiri mustakabali wa ubinadamu na ambayo Majisterio Yake ya juu hulipa kipaumbele zaidi. Italia, ambayo ina msingi wa hati yake ya kikatiba katika kukataa vita, katika kukataa hukumu ya kifo, katika utambuzi wa haki za kimsingi na uhuru, na katika kutafuta amani na haki kati ya mataifa, itaweza tu kuchangia, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayoendelea na utambuzi wa njia za ukuaji wa haki na endelevu, kwa jicho hasa kwa vizazi vichanga. Bila wao, kiukweli, zoezi lenyewe la tumaini lingekuwa la uwongo. Nina hakika Baba Mtakatifu, kwamba Waitaliano wote wanajiunga katika matashi ya dhati ambayo ninayo furaha kuwahutubia kwa ajili ya ustawi wao wa kibinafsi na wa kiroho, na vilevile kwa kuendeleza matunda kwa kazi mnayofanya katika huduma ya Kanisa Katoliki na la Ubinadamu.”

Papa baada ya sala ya Malaika 1 Januari 2025
01 January 2025, 15:37