Papa Francisko:mama wengi wamevunjika moyo kwa sababu ya vita vya kinyama
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku ya Amani ulimwenguni, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana ya kwanza tarehe Mosi Januari 2025, akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican. Kwa kuwageukia waamini na mahujaji wengi waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu alianza kusema kuwa “Mshangao na furaha ya Noeli inaendelea katika Injili ya Liturujia ya leo(Lk 2,16-21) ambayo inasimulia kufika kwa wachungaji katika horini Betlehemu. Baada ya tangazao la Malaika, kiukweli walikwenda kwa haraka na kumkuta Maria na Yosefu na mtoto, amelazwa katika malisho ya wanyama (Lk 2,16). Mkutano huo uliwajaza wote mshangao, kwa sababu wachungaji, walieleza kile ambacho kilisemwa kwako kuhusu mtoto (Lk 2,17): Mtoto aliyezaliwa ni Mwokozi , Kristo Bwana (Lk 2,11).
Papa Francisko amesema kuwa “Tutafakari kile ambacho wachungaji waliona huko Betlehemu, mtoto na hata kile ambacho hawakuona, yaani Moyo wa Maria ambao ulikuwa unatunza na kutafakari matukio hayo (Lk 2,19). Awali ya Yote, mtoto Yesu: jina hilo kwa kiyahudi maana yake ‘Mungu anaokoa’ na ndiyo hasa atakachofanya. Bwana, kiukweli alikuja duniani kwa ajili ya kutupatia maisha yake mwenyewe. Tufikirie hili: watu wote ni watoto, lakini hakika hakuna mmoja wetu aliyechagua kuzaliwa. Mungu kinyume chake alichagua kuzaliwa kwa ajili yetu: Yesu ni onesho la upendo wake wa milele, anaoleta amani ulimwenguni. Mtoto mchanga Masiha, ambaye anaonesha huruma ya Baba, anafanana na moyo wa Maria, Bikira Mama. Moyo huo ni sikio ambalo lilisikiliza tangazo kutoka kwa Malaika; kwa moyo huo ni mkono wa mchumba aliotoa kwa Yosefu; moyo huo ni mkumbatio ambao ulimzunguka Elizabeti katika uzee wake.
Katika moyo wa Maria,mama yetu unadunda matumaini, unadunda matumaini ya ukombozi, wa kukombolewa kwa kila kiumbe. Akina mama wote wana moyo daima kwa ajili ya watoto wao. Leo hii katika siku ya kwanza ya Mwaka, unaojikita katika amani, tufikirie wakina mama wote ambao wanafurahi katika mioyo yao na mama wote wambao mioyo yao imejaa uchungu,kwa sababu watoto wao,wamechukuliwa na vurugu,jeuri na chuki. Jinsi gani ilivyo nzuri amani. Vita ni unyama ulioje, unaovunja mioyo ya akina mama! Katika mwanga wa tafakari hizi kila mmoja wetu anaweza kujiuliza: ninajua kukaa kimya na kutafakari kuzaliwa kwa Yesu? Na ninatafuta kutunza ndani ya moyo tukio hilo ujumbe wake wa wema na wa wokovu? Na ninaweza mimi kubadilika zawadi hu kubwa sana katika ishara ya bure ya amani, ya msamaha na ya maridhiano? Kila mmmoja atatufa lolote la kufanya na hii itakuwa vizuri. Maria, Mtakatifu Mama wa Mungu, atusaidie kutunza katika moyo na kushuhudia katika ulimwengu furaha ya Injili.