Karibu nyumbani Papa!
Andrea Tornielli
Zimepita siku 38 tangu tarehe 14 Februari, wakati papa Francisko alikuwa ameacha Vatican kwa ajili ya kulazwa katika Hospitali ya Gemelli. Majuma magumu kwa mgonjwa wa miaka 88 aliyekuwa ameshikwa na ugonjwa wa Mkamba wa pande mbili. Tahari za madaktari hazikunyamaza kuelezea hali ngumu, mgogoro ambao alipitia, mgumu sana katika mtazamo wa vipimo vya kliniki. Lakini siku alizopitia zilikuwa hasa za kusindikizwa na mto wa sala kwa ajili ya afya: sala binafsi, sala za kijumuiya, rozari, oya misa. Waliosali kwa ajili ya Papa hawakuwa wakatoliki tu, na wala wakristo tu. Walisali kwa ajili ya Papa hata wanawake na wanaume wa dini nyingine. Walituma mawazo mazuri na matashi mema hata watu wasio amini. Ni kwa ajili ya watu wote katika sala ambao kwa salamu fupi leo hii imependwa na imefikiriwa.
Tumeishi na Askofu wa Roma kwa siku hizi ndefu za mateso, tulisubiri, tulisali, tulishikwa hisia kali wakati rehe 7 Machi, Papa Francisko alipopenda sauti yake iweze kuwafikia wote, kwa kuwashukuru waamini waliokuwa katika sala kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, na waliokuwa wameunganishwa nao ulimwenguni kote. Tulitiwa moyo, usiku wa Dominika ya tarehe 16 Machi, wakati kwa mara ya kwanza tulioona hata kama ni upande wa mgongo wake, picha ambayo alikuwa akisali mara baada ya maadhimisho ya misa katika kikanisa kilichopo Ghorofa ya 10 ya Hospitali ya Gemelli. Baada ya kuhangaika sana lakini pia uaminifu mwingi na kujikabidhi kwa mpango wa Yule anayetupa sisi maisha kila dakika na ambaye kila dakika anaweza kutuita kwake, leo hii tumemuona. Tumepokea kwa upya baraka yake katika siku ambayo amerudi tena mjini Vatican.
Kutoka katika chumba cha hospitali kwa majuma haya, Papa Francisko alitukumbusha kuwa maisha ni ya hadhi yanayotakiwa kuishi kila dakikira na kila dakika yanaweza kuombwa. Alitukumbusha kuwa mateso na udhaifu unaweza kugeuka kuwa fursa ya kushuhudia kiinjili, kwa ajili ya kutangaza Mungu ambaye anakuwa Mwanadamu, na anateseka na sisi kwa kukubali kuwambwa juu ya Msalaba. Tunamshukuru kwa ajili ya kusema akiwa katika chumba cha hospitali, kuwa vita vilionekana bado kuwa vya kipuuzi, kwa ajili ya kutueleza kwamba ni lazima tuipokonye dunia silaha na kwa hiyo tusiiweke tena katika kujaza ghala zake za silaha na vyombo vipya vya kifo; kwa ajili ya kusali na kuteseka kwa matueso yake kwa ajili ya amani kiasi cha kuwa hatarini leo. Karibu nyumbani Baba Mtakatifu!