Nia ya Papa ni kuchungulia dirishani Dominika 23 Machi baada ya saa 6 kwa ajili ya baraka!
Vatican News
Papa Francisko anatarajia kuchungulia kutokea katika dirisha la Hospitali ya Gemelli kesho tarehe 23 Machi 2025, muda mfupi baada ya saa 6:00 kamili mchana saa za Ulaya (baadaye kidogo ya saa 8 kamili mchana saa za Afrika Mashariki na Kati), ili kusalimia na kutoa baraka zake. Nakala ya tafakari ya Malaika wa Bwana itatolewa kama katika Dominika zilizopita. Vyombo vya habari vya Vatican vitakuwepo kwa ajili ya huchukuaji na usambazaji wa picha hizo. Taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya habari, Vatican imeripotii leo hii, Jumamosi tarehe 22 Machi 2025.
Taarifa za afya Papa, Mchi 21
Jana, Ijumaa jioni tarehe 21 Machi 2025, Ofisi ya vyombo vya habari, Vatican ilitoa sasisho kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko, ambayo bado ni thabiti na uboreshaji mdogo katika mifumo yake ya mazozi ya viungo na kupumua. Siku za Papa zilipita kati ya tiba ya madawa na tiba ya mazozi ya viungo na ya kupumua pamoja na maombi na kazi kidogo.
Papa Francisko hakupokea wageni wowote. Wakati wa usiku hatumii tena uingizaji hewa ya mitambo na barakoa, bali oksijeni ya mtiririko wa juu kwa kutumia pua na wakati wa mchana hatumii mtiririko wa juu sana bali kidogo.
Taarifa inayofuata ya matibabu inatarajiwa si zaidi ya Jumatatu. Wakati huo huo, tunapoendelea kumwombea afya njema jioni ya Jumamosi tarehe 22 Machi 2025, mida ya saa 1.30, kama kawaida ya siku hizi, sala ya Rozari Takatifu itaongozwa na Monsinyo Giordano Piccinotti, rais wa Utawala wa Urithi wa Makao ya Kitume, Vatican.