Papa ataruhusiwa kutoka hospitalini Gemelli,Machi 23
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Habari, zilizotarajiwa kwa takriban siku arobaini, zimekuja mwanzoni mwa mkutano huo, wa pili baada ya ule wa mnamo Februari 21, ambapo madaktari Sergio Alfieri na Luigi Carbone walifanya leo alasiri Jumamosi tarehe 22 Machi 2025 katika Ukumbi wa Hospitali ya Gemelli kwamba: Papa Francisko ataruhusiwa kesho, Dominika tarehe 23 Machi 2025. Baada ya kukaa hospitalini kwa muda mrefu kutokana na nimonia ya sehemu mbili iliyompata katika miezi ya hivi karibuni, baada ya matukio ya shida ambayo yaliweka maisha ya Papa kuwa hatarini, baada ya matangazo, ya vyombo vya habari, habari rasmi na habari za uongo kuenea hasa kupitia mitandao ya kijamii, na baada ya mlolongo wa maombi usiokatizwa katika mabara matano, Papa Francisko anarejea "nyumbani." Anarudi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, mjini Vatican ambako kupumzika kwa muda mrefu kunamngoja na kuendelea kwa matibabu ya mazoezi ya viungo na kupumua. Yale yale ambayo amekuwa akiendelea kufanyiwa siku hizi katika Hospitali ya Gemelli, Roma.
Tangazo la kuruhusiwa kutoka hospitalini
Ishara za mshangao kutoka kwa waandishi wa habari wengi waliokuwepo kwenye ukumbi wa Gemelli na wengine tayari walikuwapo kwa ajili ya kurekodi kuonekana kwa Papa kutoka hospitalini wakati wa Sala ya Malaika, iliyotangazwa Jumamosi asubuhi, Mchi 22na kuthibitishwa mchana - ikiambatana na habari iliyosomwa mbele ya kamera za waandishi wa habari na Dk. Sergio Alfieri, mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Tiba na Upasuaji hospitalini Gemelli na mkurugenzi wa timu iliyofualitia matibabu ya Papa wakati wa kulazwa hospitalini. Kando yake alikuwa ni Dk. Luigi Carbone, naibu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi wa Mji wa Vatican na mwakilishi wa matibabu ya Baba Mtakatifu, na Matteo Bruni, Msemaji mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican. "Habari njema ambayo nadhani dunia nzima inasubiri ni kwamba kesho Baba Mtakatifu anaruhusiwa; kesho atarudi Mtakatifu Marta," Dk Alfieri alisema. Na kisha akaelezea muhtasari "mdogo na muhimu" wa kile kilichotokea tangu tarehe 14 Februari 2025. Hiyo ni siku ya kulazwa hospitalini wakati Papa alidhihirisha kushindwa kupumua kwa papo hapo kutokana na maambukizi kwenye mapafu. Kwa hiyo ni virusi, bakteria na fangasi ambazo zilisababisha nimonia kali ya pande mbili. Hii ilihitaji matibabu ya pamoja ya kifamasia wakati wa kulazwa hospitalini,” alisisitiza Dk. huyo.
Mgogoro na Matibabu
Vipindi viwili "vigumu sana"vilimgusa Papa na ambapo mtaalamu huyo alisema, Papa Francisko "alikuwa katika hatari ya maisha." Matibabu ya madawa, usimamizi wa oksijeni ya juu na uingizaji hewa ya mitambo isiyo ya uvamizi, hata hivyo, imesababisha uboreshaji wa polepole na wa hatua kwa hatua, na kuruhusu Baba Mtakatifu kuibuka kutoka katika matukio muhimu zaidi." Papa "hakuwa na bomba la uingizaji hewa na daima alibaki macho, na mwelekeo mzuri. Kwa hiyo kuruhusiwa kesho kutafanyika katika hali ya vipimo imara, na imara kwa angalau majuma mawili. Maagizo ya wafanyakazi wote wa matibabu, sasa, ni kuendelea kwa sehemu ya matibabu ya dawa kwa muda mrefu na kwa mdomo. Pia ni muhimu kuchunguza kipindi cha kupumzika wakati wa kupona angalau miezi miwili.”
Kupona huko Mtakatifu Marta
Kwa hiyo, "kuruhusiwa kutoka katika ulinzi," alisema Dk. Carbone, akielezea kwamba huko Mtakatifu Marta hakuna kituo maalum au chumba kilichowekwa, lakini "mahitaji" yote yalitathminiwa, sawa na yale ya wagonjwa wote walioruhusiwa na ugonjwa wa kupumua. "Tumetathmini mahitaji ya Baba Mtakatifu, ambayo kwa kawaida ni hitaji la oksijeni kwa muda anaohitaji. Huduma ya afya ambayo "Idara ya Afya na Usafi inaweza kumpatia Baba Mtakatifu huko Mtakatifu Marta" na huduma ya masaa 24 kwa dharura yoyote. Tumejiandaa kumkaribisha nyumbani."
Urejesho wa sauti
Madaktari hao kisha walijibu maswali ya waandishi wa habari, wakianza na yale ya sauti ya Papa, kufuatia habari zilizosambaa jana kuhusu ugumu wa Papa wa kuzungumza. "Unapokuwa na nimonia ya pande mbili, mapafu yako yameharibiwa na misuli yako ya kupumua pia inakuwa katika shida," Dk. Alfieri alielezea. "Moja ya mambo ya kwanza hutokea ni kupoteza sauti yako kidogo. Ni kama wakati fulani unatumia sauti kubwa sana." Na kama ilivyo kwa wagonjwa wote, vijana kwa wazee, lakini hasa wazee, “itachukua muda kurudi kwa sauti kama ilivyokuwa hapo awali.” Ikilinganishwa na siku kumi zilizopita, hata hivyo, maboresho makubwa yamerekodiwa kutokana na mtazamo huu pia. Ni vigumu kusema kuhusu kuanza kuzungumza, lakini kwa kutazama maboresho tunatumaini yatakuwa ya haraka," alisema Dk. Carbone.
Kuanza tena kwa kazi
Kuhusu kurejeshwa katika kazi, wataalam hao wawili walieleza kwamba tayari katika siku hizi za kulazwa hospitalini Papa "daima aliendelea kufanya kazi na ataendelea kufanya hivyo hata atakaporejea Nyumbani, Mtakatifu Marta. Sasa, hata hivyo, hataweza kuanza tena kazi mara moja: pendekezo ni "kuchukua muda unaofaa wa kupumzika na kupona. Kwa sababu hiyo hiyo, haipendekezwi kukutana na makundi ya watu au watu binafsi au kutimiza ahadi muhimu,” Madaktari hao wamesisitiza. Kwa kuongeza walisema “Papa Francisko hakika atafanya hivyo, lakini mara tu atakapomaliza matibabu yaliyowekwa na uboreshaji wa kliniki unaotarajiwa unaweza kurekodiwa."
Madaktari hata hivyo hawakutoa vipimo sahihi vya nyakati, wala hawakuzungumzia juu ya "hofu" fulani kwa kipindi hiki cha baada ya kulazwa, isipokuwa zile za kurudi tena au maambukizi mapya ambayo ni sawa na yale ya mgonjwa yeyote ulimwenguni. Kwa vyovyote vile, Dk. Alfieri, alifafanua kwamba Papa hajawahi kuwa na Uviko wala hana kisukari,” na alihakikisha kwamba "maambukizi makubwa zaidi yametatuliwa: kuna baadhi ya bakteria ambao wameshindwa, baadhi ya virusi ambavyoo wingi wa virusi umepungua. Baadhi ya fangasi wamepungua mbele yao lakini itachukua muda mrefu, miezi mingi, kushindwa.” Kwa hivyo ikiwa swali ni: bado ana nimonia ya pande mbili? Jibu ni hapana. Ikiwa ameponywa kabisa aina zote za virusi kwenye mapafu(polymicrobial): itachukua muda.”
Papa anafurahi kurudi
Wakijibu maswali zaidi ya waandishi wa habari na madaktari wengine waliokuwepo wa vyombo vya habari, kuhusiana na kupungua uzito kwa Papa, Dk. Alfieri na Carbone walieleza kuwa "hatukumpima Papa, lakini atakuwa amepungua uzito. Mtaona kesho jinsi vazi lake lilivyo kubwa," Alfieri alitania, akiongeza kwamba Papa Francisko ana hifadhi, kwa hivyo kwa mtazamo huo hatuna wasiwasi.” Kwa Swali jingine kuhusu Bergoglio kuandika na kula walisema: “anaandika na anakula, labda alipokuwa mgonjwa sana, sasa kwa kuwa ana nafuu, "ameanza kula tena hatua kwa hatua." Madaktari hao wawili walisisitiza kuwa ni chaguo lao kumruhusu("Daima ni chaguo la madaktari"), lakini Papa Francisko alikuwa akitarajia hilo kwa muda: "Amekuwa akituuliza kwa siku 3-4: ni lini nitarudi nyumbani?"
"Ni wazi kwamba Baba Mtakatifu angeweza kwenda nyumbani siku chache zilizopita, wakati alipogundua kuwa alikuwa akiimarika, anapumua vyema, na anaweza kufanya kazi zaidi," Dk. Carbone alisema. Kwa kuongezea Dk. Alfieri alisema hivi: “Alikuwa mfano mzuri wa mgonjwa, kwasababu alijua jinsi ya kusikiliza mapendekezo ya kila mtu.” “Na kila mtu, ikiwa ni pamoja na wataalam muhimu wa magonjwa ya kuambukiza na ugonjwa wa kisukari, waliamini kuwa huu "ulikuwa wakati mwafaka pia wa kutobaki hospitalini tena, kwa sababu maendeleo zaidi yapo nyumbani. Hospitali, hata kama inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza, kusema ukweli, ndio mahali pabaya zaidi pa kupona, kwa sababu ndiyo mahali ambapo unapata maambukizi mengi zaidi."
Hali ya ucheshi
Kwa kutazama wakati ujao, kuanzia kesho, Dk. Bruni alithibitisha kwamba kuonekana kwa Papa kutoka Gemelli kutafanyika, kisha atarudi Mtakatifu Marta, mara moja baadaye kwa namna ambayo haijatajwa. Hakuna maelekezo ya ibada za Juma Takatifu, za ziara ya Mfalme Charles (inayotajwa kutoka Buckingham) tarehe 8 Aprili, ya safari inayotarajiwa sana ya Nikea kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso. Haya yote yataonekana, wakati huo huo habari njema ya kurudi kwake nyumbani, na tahadhari muhimu, kwa matumaini ya "kupona haraka" na kwa uhakika wa hali nzuri ya ucheshi haijawahi kupotea kabisa lakini katika wakati mgumu zaidi inapungua kidogo.” Walieleza. "Ni wazi kwamba alipokuwa mgonjwa sana ilikuwa vigumu kwake kuwa katika hali nzuri," alisema Dk. Alfieri. “Asubuhi moja, kama vile kila asubuhi tulipoenda kusikiliza mapafu yake, baada ya kupitia wakati mbaya, tulisema: ‘Baba Mtakatifu, hujambo?’ Alipojibu ‘mimi bado niko hai’, tulielewa kuwa alikuwa mzima, hata alikuwa amerejesha hali yake nzuri ya ucheshi.”