Papa:ikiwa mtoto au mtu aliye hatarini yuko salama,Kristo anahudumiwa na kuheshimiwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto ambao ulifunguliwa Jumatatu tarehe Machi 24 na utahitimishwa Ujumaa tarehe 28 Machi 2025. Ujumbe huo uliotiwa saini huko Hospitalini Gemelli tarehe 20 Machi 2025 Papa Francisko. Papa anawatumia salamu zake za uchangamfu na “maelekezo fulani kwa ajili ya huduma yao muhimu. Hakika ni kama “oksijeni” kwa Makanisa ya mahalia pamoja na jumuiya za kidini, kwa sababu popote mtoto au mtu aliye hatarini akiwa salama, hapo mnamtumikia na kumheshimu Kristo.” Katika utaratibu wa kila siku wa kazi yenu- hasa katika maeneo yaliyokosa fursa zaidi - ukweli wa kinabii unakuwa ukweli hasa kuzuia unyanyasaji si blanketi la kutandazwa juu ya dharura, lakini ambayo ni moja ya misingi ambayo juu yake inaweza kujenga jumuiya aminifu kwa Injili. Kwa hili, ninatoa shukrani zangu."
Sera za kuzuia katika jumuiya mbali mbali
Papa Francisko anaeleza umuhimu wa jitihada zao zinavyopaswa kuwa: “ Kazi yenu haiwezi kupunguzwa kuwa itifaki za kutumiwa, lakini inayokuza ulinzi: muundo unaoelimisha, kuangalia kuzuia, kusikiliza na ambayo inarejesha heshima.” Aidha Papa alisema kuwa wao wanapoanzisha sera za kuzuia, hata katika jumuiya za mbali zaidi, waaandika ahadi: kwamba "kila mtoto, kila mtu aliye hatarini, atapata mazingira salama katika jumuiya ya kikanisa. Hii ndio injini ya kile kinachopaswa kuwa kwetu ubadilishaji muhimu.”
Maombi matatu ya Papa:ushirikiano na Curia Romana,ukarimu na kujenga ushirikiano na vyombo vya nje
Papa Francisko katika Ujumbe wake anatoa ombi lake kuwa: “Leo, ninawaomba ahadi ya mambo matatu: 1. Kuendeleza kazi ya pamoja na Mabaraza ya Curia Romana; 2. Kutoa ukarimu na kutunza majeraha ya roho kwa wahanga na walionusurika, kwa mtindo wa Msamaria mwema. Kusikiliza kwa sikio la moyo, ili kwamba kila ushuhuda haupati rejista ya kukusanywa, lakini huruma ya kina ambayo kwayo kuna kuzaliwa upya; 3. Kujenga ushirikiano na vyombo vilivyo nje ya Kanisa - mamlaka za kiraia, wataalamu, vyama - ili ulinzi uweze kuwa lugha ya ulimwengu wote.
Kwa miaka 10 wamewezesha mtandao kukua ndani ya Kanisa
Kwa kuhitimisha ujumbe huo Baba Mtakatifu anabainisha kwamba:“ Katika miaka hii kumi, mmewezesha mtandao wa usalama kukua ndani ya Kanisa. Muendelee! Mundelee kuwa walinzi wanaokesha ulimwengu unapolala. Roho Mtakatifu, mwalimu wa kumbukumbu hai, atulinde na majaribu ya kuondoa huzuni badala ya kuyaponya. Asante kwa ukumbusho wenu katika maombi. Mimi pia ninawasindikiza na ninamwomba Bwana na Bikira Mwenyeheri awasimamie, ili muendelee na safari yenu kwa ari na matumaini," anahitimisha Papa.