Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Allegro con spirito
Ratiba Podcast
Moja ya Picha za Katekesi za Papa Moja ya Picha za Katekesi za Papa   (Vatican Media)

Papa,Katekesi,Msamaria:nipe maji ya kunywa:Mungu ni huruma anatusubiri daima!

Baba Mtakatifu katika tafakari ya Katekesi,Machi 26 anaendelea kuonesha mikutano kati ya Kristo Yesu na watu mbalimbali ambaopo katika tafakari anafafanua Msamaria aliyeombwa na Yesu maji ya kunywa.Yesu anatusubiri na anajifanya kupatikana wakati tunawaza kuwa hatuna tena matumaini.Hata kama maisha yetu yanaweza kuonekana yameharibika,Mungu anaweza kutufanya kuanza upya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, imechapisha Katekesi iliyoandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko, na ambayo alikuwa azungumze tarehe 26 Machi ambapo ilifutwa kutokana na kuelendelea na mapumziko ya  baada ya kurudi kutoka Hospitali ya Gemelli Roma,  alikokuwa amelezwa kwa sababu ya uongwa wa  Mkamba kwanza na baadaye nemonia ya pande mbili  na sasa yupo  nyumbani Mtakatifu Marta mjini Vatican. Katekesi hii ni mwendelezo kuhusu mada ya: “Roho Mtakatifu na Bibi Arusi. Roho Mtakatifu anawaongoza watu wa Mungu kuelekea kwa Yesu, tumaini letu” kama sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Katika muktadha huo, tafakari hii ni  Maisha ya Yesu na mikutano mbali mbali kwa kujikita na mada ya Msamaria aliyeombwa maji ya kunywa na Yesu(Yh 4,7).

Kwa kuongozwa na kifungu cha Injili ya Yh 4,10 kisemacho: “Yesu akamwambia Msamaria: “kama ungejulia zawadi ya Mungu na yule anayekwambia : Naomba maji ya kunywa!”, unagemwomba Yeye na Yeye  angeweza kukupatia maji ya uzima.” Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, mara baada ya kutafakari kuhusu Mkutano na Nikodemu, ambaye alikuwa amekwenda kutafuta Yesu usiku, leo tutafakari vipindi vile ambavyo utafikiri hasa yuko anatusubiri pale, katika njiapanda ya maisha yetu. Ni mkutano ambayo inatushangaza, na mwanzo labda tunaweza kuwa kidogo hatuamini: tunatafuta namna ya kuwa na busara na kusubiri kile ambacho kinatokea.

'Yesu anatusubiri na anajifanya kupatikana wakati hatuna matumaini'

Uzoefu huu bilashaka ulikuwa hata wa yule mwanamke Msamaria, ambaye anazungumziwa katika sura ya nne ya Injili ya Yohane (Yh 4,5-26). Yeye hakutegemea kukutana na mwanaume  katika kisima cha maji saa sita, na zaidi alikuwa akitegemea kutokukuta mtu yeyote.  Kiukweli alikuwa anakwenda kuteka maji katika kisima kwa saa zisizo za kawaida, yaani kulipokuwa na joto kali. Labda mwanamke huyo alikuwa na aibu ya maisha yake, kabisa alikuwa anahisi kuhukumiwa, bila kueleweka, na kwa njia hiyo alikuwa amejibagua, alivunja mahusiano na wote. Ili kwenda Galilaya kutoka mji wa Yuda,  Yesu angeweza kuchagua njia nyingine na kukatisha kwenda Samaria. Na pia ingekuwa hata hakika zaidi, kwa mtazamo, mahusiano ya mivutano kati ya Wayahudi na Wasamaria. Kinyume chake Yeye alipita pale na kusimama katika kisima hasa wakati ule! Yesu anatusubiri na anajifanya kupatikana wakati tunawaza kuwa kwetu,  hatuna tena matumaini. Kisimani, zamani katika Mashariki ya Kati, ni eneo la mkutano, mahali ambapo mara nyingi waliunganisha ndoa, ni eneo la uchumba. Yesu alitaka kumsaidia mwanamke huyo kuelewa mahali pa kutafuta jibu la kweli la shauku yake  ya kuwa anapendwa.

'Mada ya shauku ni msingi wa kuelewa mkutano wa Msamaria'

Baba Mtakatifu Francisko anakazi kusema kuwa mada ya shauku, ni msingi kwa ajili ya kuelewa mkutano huo.  Yesu alikuwa wa kwanza kuelezea shauku yake: “ Ninaomba maji ya kunywa” (Yh 4,10). Pamoja na kufungua mazungumzo, Yesu anafanya kuonesha udhaifu, kwa njia hiyo ya kumweka mtu mwingine kwa urahisi na kuhakikisha kuwa haogopi. Kiu mara nyingi hata katika Biblia ni picha ya shauku. Lakini Yesu hapa ana kiu kwanza kabisa ya wokovu wa mwanamke yule. “ Yule aliyekuwa anaomba maji, anasema Mtakatifu Agostino, alikuwa na kiu ya imani ya mwanamke huyu.” Ikiwa Nikodemu alikuwa amekwenda kwa Yesu, usiku, hapa Yesu anakutana na mwanamke msamaria, saa sita, wakati ambao kuna mwanga zaidi. Kiukweli ni wakati wa maonesho. Yesu anajifanya kumwonesha kuwa ni masha na zaidi anaweka nuru juu ya maisha yake. Na anamsaidia kutazama kwa namna mpya historia yake, ambayo ilikuwa ngumu na uchungu; alikuwa amepata wanaume watano, na sasa alikuwa na wa sita na ambaye hakuwa mme wake. Idadi ya namba sita, si kwa bahati mbaya, lakini kawaida huonesha kutokamilika. Labda alikuwa katika kuota mme wa saba, ambaye hatimaye angeweza kutosheleza shauku ya mwanamke huyo,  ya kuwa anapendwa kiukweli. Na mme huyo anaweza kuwa Yesu pekee. Wakatialipotambua kuwa Yesu anajua maisha yake, mwanamke huyo alijaribu alibadilisha mazungumzo juu ya masuala ya kidini ambayo yalikuwa yakiwagawanya  Wayahudi na Wasamaria.

'Yule unayemsubiri ni mimi'

Papa amesisitiza kuwa “inatokea wakati mwengine hata sisi, wakati tunasali: katika wakati ambao Mungu anataka kugusa maisha yetu  na matatizo yake, tunapopotea wakati mwingine katika tafakari ambayo zinatupatia udanganyifu wa sala ya kufanikiwa.  Na kwa hiyo, kiukweli, tunaamsha vizingiti vya kujilinda. Bwana lakini daima ni mkuu zaidi na mwanamke yule Msamaria, ambaye kwa mujibu wa kanuni za kiutamaduni hakupaswa hata kusema neno,  anatoa ufunuo wa juu zaidi: anazungumza naye juu ya Baba, ambaye lazima aabudiwe katika roho na kweli. Na wakati yeye  kwa mara nyingine tena kwa mshangao, anabainisha kuwa katika mambo hayo ni bora kusubiri Masiha, Yesu alimwambia kuwa: “Ni mimi, ambaye ninazungumza nawe”(Yh 4,26). Ni kama tamko la upendo: Yule ambaye unayemsubiri ni mimi; Yule ambaye anaweza hatimaye kukujibu shauku yako ya kuwa unapendwa. Kutokana na hilo, wakati huo mwanamke alikimbia kwenda kuwaita watu wa kijiji, kwa sababu ni hasa uzoefu wa kuhisi kupendwa ambao unaibua utume. Ni tangazo gani linaweza kupelekwa ikiwa siyo uzoefu wake wa kuwa ameeleweka, amepokelewa, amesamehewa? Ni picha ambayo inatupasa kutufanya tutafakari juu ya utafutaji wetu wa njia za kuinjilisha. Ni pale hasa kama mtu anayependa, msamaria alisahau chungu chake chini ya miguu ya Yesu. Uzito wa chungu  kila juu ya kichwa chake, kila mara ambapo alirudi nyumbani, kilikuwa kinamkumbusha hali yake na  maisha yake ya wasiwasi.

'Kuweka chungu chini ya miguu ya Yesu'

Lakini sasa chungu chake amekiweka chini ya miguu ya Yesu. Wakati uliopita hauna tena uzito zaidi; yeye amejipatanisha. Na ndivyo hivyo hata sisi; kwenda kutangaza Injili, tunahitaji kwanza kabisha kutua mzigo wa historia yetu miguuni pa Bwana, kukabidhi kwake uzito wa wakati wetu uliopita. Ni watu waliojipatanisha tu, wanaweza kupeleka Injili.  Baba Mtakatifu anahitimisha kwa kusema: “Kaka na dada, tusipoteze matumaini” hata ikiwa historia yetu inaonekana nzito, ngumu na labda iliyoharibika, daima tuna uwezekano wa kuikabidhi kwa Mungu na kuanza upya safari. Mungu ni huruma na anatusubiri daima.”

Katekesi ya Papa 26 Machi 2025
26 Machi 2025, 12:19
Prev
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031     
Next
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930