Papa:kukusanyika kwenu ni kukumbatia mwaliko wa Yesu wa kuingia mlango mwembamba!
Na Angella Rwezaula – Vatican
Ni kutoka katika Hospitali ya Gemelli, jijini Roma ambapo Baba Mtakatifu Francisko alitia saini ujumbe wake wa ukaribu kwa mahujaji walioshiriki katika hija ya Jubilei ya Jimbo kuu la Napoli lakini ambayo pia imewahusu waamini wengi, wengi wao wakitoka katika majimbo mengine ya Italia, ambapo siku ya Jumamosi tarehe 22 Machi 2025 walivuka Mlango Mtakatifu wa kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo aliwaelekea kaka na dada wote wa Napoli na majimbo mengine. Aliwasalimu maaskofu wao katika fursa hiyo ya Hija ya kijubilei kijimbo ambayo wamehitimiza.
Kardinali Battaglia akisoma ujumbe wa Papa(Vatican Media)
Kukumbatia mwaliko wa Yesu wa kuingia mlanngo mwembamba
Papa alibainisha kuwa katika Jubilei hiyo “inaonesha umoja unaowakusanya ninyi kama jumuiya inayowazunguka Wachungaji wenu na Askofu wa Roma, pamoja na kujitolea kukumbatia mwaliko wa Yesu wa kuingia “kupitia mlango ulio mwembamba”(Mt 7:13). Upendo uko hivi: unatuunganisha na kutufanya kukua pamoja. Kwa sababu hii, ingawa tumepitia njia mbalimbali, imewaleta ninyi hapo pamoja kwenye kaburi la Petro, ambapo mnaweza kutoka tena na nguvu zaidi katika imani na umoja zaidi katika upendo.”
Misa ya wanahija wa kijubilei kutoka Napoli na majimbo mengine mengi(VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Papa ameshukuru sala anazoombewa
Papa Francisko katika ujumbe huo aidha alibainisha kuwa: “Katika siku hizi nimeona kuungwa mkono na ukaribu wenu hasa kwa maombi mliyonisindikiza. Kwa hiyo, hata kama siwezi kuwa pamoja nanyi kimwili, ninawaonesha furaha yangu kuu kwa kujua kwamba mmeunganishwa pamoja nami na ninyi wenyewe katika Bwana Yesu kama Kanisa.” Papa alihitimisha kwa kuwabariki kuwa “Ninawabariki na kuwaombea. Na ninapendekeza kwenu: ninyi pia muendelee kuniombea. Asante.”
Misa ya wanahija kutoka Napoli na majimbo mengine (VATICAN MEDIA Divisione Foto)