Ulimwengu unamwona Papa tena,salamu kutoka Gemelli: “Asanteni nyote"
Na Salvatore Cernuzio – Roma
“Asante ninyi nyote”
Huyo hapa Papa, hapa anatokea tena kwa waamini 3,000 waliokusanyika tangu asubuhi katika uwanja wa Hospitali ya Gemelli ambao katika siku hizi 38 za kulazwa hospitalini kumeonekana mlolongo usiokatizwa wa maombi kwa ajili ya kupona kwake. Yalikuwa ni maneno machache kutoka kwenye balcony ya ghorofa ya tano, akionesha uso uliochoka, mikono juu ya magoti na iliyoinuliwa kupungia na kubariki. Kidokezo cha tabasamu katika kuona na kusikia umati huo ukipiga kelele: "Francesco, Francesco!", "Tunakupenda!", "Tuko hapa kwa ajili yako!"
Salamu kwa Carmela, "mwanamke mwenye maua ya manjano" "Asante nyote!" Papa alisema kwa sauti dhaifu. Salamu ilitarajiwa, lakini Papa alitaka kuonekana na kusikilizwa. Macho yake yalitazama upande mmoja wa uwanja hadi mwingine, basi, kama ilivyo kawaida yake, na alizingatia jambo moja: Bi Carmela Mancuso, mwenye umri wa miaka 78 kutoka Calabria, aliyekuwa mstari wa mbele akielekeza kwenye balcony ndogo, akiwa ameshikilia shada la maua ya njano. Aliondoka katika kituo cha Mtakatifu Pietro kwenda Gemelli. Na amefanya hivyo karibu kila siku kwa zaidi ya mwezi mmoja, lakini pia amefanya mara nyingi wakati wa Katekesi kila Jumatano. "Na ninamwona mwanamke huyo mwenye maua ya manjano! Ni mwema!" Papa alisema.
Mzunguko wa makofi, kwaya ya "Uishi muda mrefu Papa”, ilisikika. Bi Carmela yule yule aliyeinamisha kichwa chake, akaburuzwa chini na uzito wa machozi yake. "Sijui la kusema. Asante, asante, asante, kwa Bwana na Baba Mtakatifu. Sikufikiri kuwa 'nimeonekana' hivyo," alitoa maoni yake mara moja baadaye kwa vyombo vya habari vya Vatican. "Alitakiwa kutoa baraka na badala yake aliona shada langu la waridi. Namtakia apone haraka na arudi kwetu kama hapo awali."
Kukumbatia watu
Kulikua na matashi mema yaliyotolewa na wauguzi, madaktari, na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki waliokusanyika ndani. Kulikuwa na waamini wa mataifa mbalimbali, Shirika la Auxilium ambao waliinua kabla ya saa 6 kamili bango kubwa na bendera kutoka duniani kote na wito wa amani. Kulikuwa na mtu aliyefikisha miaka 75 jana ameshikilia ishara ambayo alimkabidhi Papa Francisko kwa maombezi ya mtangulizi wake Yohane Paulo II. Na kulikuwa na kikundi ambacho kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro kilichukua msalaba wa Jubilei - ule uliotumiwa kwa hija kwenye Mlango Mtakatifu - na kufika hadi Gemelli: "Ni muhimu kuwa hapa,” walibainisha. Kulikuwa na Emanuela na Adam, pamoja na watoto wao watatu, ambao baada ya Misa “karibu” walitaka kuwachukua watoto kumsalimia Papa Francisko: “Tulisali kila siku mezani kwa ajili yake, ilikuwa sawa kwamba walimwona,” baba huyo alisema. Kisha kulikuwa na Sr Geneviéve Jeanningros, mtawa wa Bustani ya Luna huko Ostia, anayejikitia na shughuli za uchungaji Roma na kikundi cha Sinti lakini pia cha mashoga na watu waliobadili jinsia. Jamaa wa zamani wa Papa ("mtoto wa kutisha", anamwita) ambaye huenda kumsalimia kila Jumatano kwenye katekesi katika uwanja wa Mtakatifu Petro au katika Ukumbi wa Paulo VI. “Nisingeweza kungoja kwamba Papa Francisko ajitokeze na kutoka," alitoa maoni kwa vyombo vya habari vya Vatican. "Hatukuweza kuvumilia tena. Tunamtakia kila la heri. Heri njema.”
Kuaga wakati wa kutoka hospitalini kupitia Mtakatifu Maria Mkuu
Mara tu baada ya kutoka kwenye balcony, umati wa watu ulisogea kuelekea lango la Gemelli ili kumnasa Papa atoke akiwa katika mtindo wake wa kawaida na ambao sasa unajulikana sana, wa Gari la Fiat 500L nyeupe. Salamu na nyimbo zaidi ziliambatana na njia ya Papa ndani ya gari, na madirisha yakiwa yamefungwa. Mwelekeo ni Mtakatifu Maria Mkuu katika basilika ambayo haijawahi hata mara moja - baada ya safari ya kimataifa au upasuaji na kulazwa hospitalini - Jorge Mario Bergoglio ameshindwa kutembelea kusali kwa Salus Populi Romani na kumshukuru kwa ulinzi wake.
Kabla ya kutokea kwenye balcony ya hospitali, Papa Francisko alitaka kuwasalimu kwa ufupi wafanyakazi na wasimamizi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki na Gemelli Polyclinic: mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu, Profesa Elena Beccalli; rais wa Mfuko wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Agostino Gemelli IRCCS, Dk. Daniele Franco; pia Mkuu wa Kitivo cha Tiba na Upasuaji cha Chuo Kikuu cha Kikatoliki, profesa Antonio Gasbarrini; makamu rais wa Mfuko, Giuseppe Fioroni; mkurugenzi mkuu, Marco Elefanti, msaidizi mkuu wa kikanisa wa Chuo Kikuu, Askofu Claudio Giuliodori, na Profesa Sergio Alfieri, mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Tiba-Upasuaji ya Policlinico na mkuu wa timu ya matibabu ya Gemelli; mkurugenzi wa afya wa Mfuko wa Hospitali ya Gemelli, Andrea Cambieri.