Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Allegro con fuoco
Ratiba Podcast
Jarida la “Civiltà Cattolica” linalohaririwa na kuchapishwa na Shirika la Wayesuit, kwa Mwaka 2025 linaadhimisha Kumbukizi ya Miaka 175 tangu kuanzishwa kwake. Jarida la “Civiltà Cattolica” linalohaririwa na kuchapishwa na Shirika la Wayesuit, kwa Mwaka 2025 linaadhimisha Kumbukizi ya Miaka 175 tangu kuanzishwa kwake.  

Kumbukizi ya Miaka 175 ya Jarida la "Civilta Cattolica" 1850-2025

Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza Wayesuit wote wanaoshirikiana na kushikamana ili kuhakikisha kwamba, Jarida hili linachapishwa na kwamba, hii ni fursa ya kumshukuru Mungu ambaye ameendelea kuwa pamoja nao katika utume huu ambao umeandamana na vizazi vingi, kwa kujenga na kudumisha urafiki na mafungamano ya kijamii; likitoa maadili na kuendelea kufasiri matukio mbalimbali kwa mwanga wa imani, matumaini na mapendo thabiti! Uinjilishaji!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Jarida la “Civiltà Cattolica” linalohaririwa na kuchapishwa na Shirika la Wayesuit, kwa Mwaka 2025 linaadhimisha Kumbukizi ya Miaka 175 tangu kuanzishwa kwake. Hii ilikuwa ni changamoto iliyotolewa na Mwenyeheri Papa Pio IX na kuanza kuchapishwa tarehe 6 Aprili 1850, kipindi kilichokuwa na misukosuko nchini Italia na Bala la Ulaya katika ujumla wake. Wayesuit, wakajifunga kibwebwe ili kuhakikisha kwamba, Jarida la “Civiltà Cattolica” linavuka mawimbi haya mazito na hivyo kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu. Tangu wakati huo, Jarida hili limeendelea kuwa aminifu kwa Mafundisho Tanzu ya Kanisa Katoliki, Mamlaka fundishi ya Kanisa “Magisterium” na hivyo kuendelea kusoma alama za nyakati. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe aliomwandikia Padre Nuno da Silva Gonçalves, Mkurugenzi mkuuu wa Jarida la “Civiltà Cattolica” tangu Oktoba 2023 anasema anawapongeza Wayesuit wote wanaoshirikiana na kushikamana ili kuhakikisha kwamba, Jarida hili linachapishwa na kwamba, hii ni fursa ya kumshukuru Mungu ambaye ameendelea kuwa pamoja nao katika utume huu ambao umeandamana na vizazi vingi, kwa kujenga na kudumisha urafiki na mafungamano ya kijamii; likitoa maadili na kuendelea kufasiri matukio mbalimbali kwa mwanga wa imani.

Padre Nuno da Silva, Mkurugenzi mkuu wa Jarida la Civilta Cattolica
Padre Nuno da Silva, Mkurugenzi mkuu wa Jarida la Civilta Cattolica

Baba Mtakatifu anawashukuru kwa huduma hii, ambayo Wayesuit wanaitoa kwa ajili ya Kanisa kama sehemu ya mchakato wa kukuza heshima, ukweli sanjari na kukoleza mazungumzo na majadiliano katika medani mbalimbali za maisha na utume wa Kanisa. Baba Mtakatifu anapenda kuwatia shime kuendeleza utume huu kwa kujikita katika uandishi bora, usiofungamana na upande wowote na hivyo kuendelea kuzama katika tunu msingi za Kiinjili, kwa kusikiliza sauti zote za upole na hivyo kuzimwilisha mintarafu maisha na utume wa Kanisa. Mwishoni mwa ujumbe wake, Baba Mtakatifu anawaweka chini ya ulinzi na tunza ya Mtakatifu Inyasi wa Loyola na kwamba, anatumia fursa hii kutuma baraka zake za kitume kwa Shirika zima la Wayesuit kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 175 tangu kuanzishwa kwa Jarida hili. Wakati Jarida hili linaadhimisha Kumbukizi ya Miaka 170 tangu kuanzishwa kwake, Baba Mtakatifu Francisko aliwashukuru Wayesuit kwa huduma hii makini wanayoendelea kuitoa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa la Kristo sehemu mbalimbali za dunia! Baba Mtakatifu katika ujumbe wake huo aliwataka Wayesuit kusoma alama za nyakati na kuendelea kujikita katika ustaarabu wa Kikatoliki unaofumbatwa katika dhana ya Msamaria mwema, yaani huduma makini kwa watu wa Mungu sehemu mbalimbali za dunia. Huu ni wakati wa kusoma alama za nyakati, kwa kujikita katika kipaji cha ubunifu, ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi katika lugha wanayoifahamu. Jarida lijikite zaidi katika mchakato wa kupambana na chuki, ubinafsi na maamuzi mbele.

Kardinali Pietro Parolin, Kumbukizi ya Miaka 175 ya Jarida la C. Cattolica
Kardinali Pietro Parolin, Kumbukizi ya Miaka 175 ya Jarida la C. Cattolica

Baba Mtakatifu Francisko aliwaambia Wayesuit kwamba, wasi wasi na ugumu wa maisha iwe ni fursa ya kusoma alama za nyakati ili kutambua mpango wa Mungu kwa ajili ya mwanadamu! Jarida la “Civiltà Cattolica” limeipokea changamoto hii kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko na kwa sasa linaanza kuchapishwa pia kwa Lugha ya Kichina na kusambazwa kwa njia ya mitandao ya kijamii. Lengo kuu ni kuendelea kuwa ni chombo cha Habari Njema ya Wokovu. Wayesuit wanaandika ukurasa mpya wa urafiki unaowakutanisha na utamaduni wa watu wa Mungu nchini China. Jarida la Civiltà Cattolica limekuwa ni sawa na mwandishi mwenye elimu ya Ufalme wa mbinguni, kwani wametoa katika hazina yao vitu vipya na vya kale.Hii ni sehemu ya ujumbe ulioandikwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Padre Antonio Spadaro, S.J., Mkurugenzi mkuu wa Jarida la “Civiltà Cattolica” kwa wakati huo, katika uzinduzi wa Jarida hilo lililoanza pia kuchapishwa kwa lugha ya Kichina. Baba Mtakatifu aliwataka Wayesuit kujenga madaraja yanayowakutanisha watu; ili kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kiekumene, ili kulinda na kudumisha tunu msingi za maisha ya kiutu! Kardinali Pietro Parolin, alipenda kuchukua fursa hii kutoka katika undani wa moyo wake, kuwapongeza na kuwashukuru Wayesuit kwa jitihada zao. Ni matumaini yake kwamba, Makala kwa lugha ya Kichina itakuwa ni fursa makini ya kutajirishana kitamaduni na kisayansi miongoni mwa watu wa Mungu wanaotafuta uzuri na ukweli. Ni matumaini yake kwamba, makala kwa lugha ya Kichina yataandaliwa na kuhaririwa kwa ari na moyo mkuu, ili yalete mvuto kwa wasomaji na kama hatima ya kazi hii ni kusaidia mchakato wa ujenzi wa ustaarabu ambao uko wazi kwa ajili ya majadiliano na amani ya kudumu kwa watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia!

Jarida Miaka 175
02 Aprili 2025, 15:17
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031