Tafuta

Mama Kanisa ametenga Mwezi Oktoba kila mwaka kwa ajili ya kuhamasisha ari na mwamko wa kimisionari kwa kuchangia kwa sala na sadaka ili kuimarisha mchakato wa uinjilishaji. Mama Kanisa ametenga Mwezi Oktoba kila mwaka kwa ajili ya kuhamasisha ari na mwamko wa kimisionari kwa kuchangia kwa sala na sadaka ili kuimarisha mchakato wa uinjilishaji. 

Sala ya Kuombea Shughuli za Kimisionari kwa Mwezi Oktoba

Juma la kwanza, Kanisa limejikita zaidi katika kuombea misioni; juma la pili, imekuwa ni fursa ya kuombea misioni zinazodhulumiwa kutokana na imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Juma la tatu, waamini wamehamasishwa zaidi kujenga na kudumisha mshikamano na ukarimu kwa ajili ya utume wa Kanisa. Na juma la nne ni kwa ajili ya shukrani na sala kwa ajili ya utume wa Kanisa.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, - Dar es Salaam.

Mama Kanisa katika kipindi cha Mwezi wa Oktoba anapenda kuwahamasisha waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki kikamilifu katika kuombea shughuli za kimisionari pamoja na kuchangia kwa hali na mali mchakato wa shughuli za kimisionari kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Juma la kwanza, Kanisa limejikita zaidi katika kuombea misioni; juma la pili, imekuwa ni fursa ya kuombea misioni zinazodhulumiwa kutokana na imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Juma la tatu, waamini wamehamasishwa zaidi kujenga na kudumisha mshikamano na ukarimu kwa ajili ya utume wa Kanisa. Na juma la nne ni kwa ajili ya shukrani na sala kwa ajili ya utume wa Kanisa. Ifuatayo ni Sala kwa ajili ya kuombea uenezaji wa imani. Sala hii inasaliwa mwezi wa kumi na nyakati nyingine zinazofaa:

Ee Mungu Baba yetu, ulianzisha Kanisa lako katika Kristo kama Sakramenti ya Wokovu ulimwenguni, wape Roho wako wale ambao umewateua kuongoza na kukoleza watu wako na kuhuisha ndani mwao ari ya umisionari. Waimarishe mapadri, wanaoshiriki katika utume wa wokovu wa Mchungaji mwema, waweze kuwaelimisha wakristo ambao Bwana aliwakabidhi kwa Kanisa lake, ili kwa kuhimizwa kwa mifano yao na kwa neno lako, waweze kushiriki katika uinjilishaji wa ulimwengu kwa sala, sadaka, majitoleo binafsi, na kuguswa kwa ajili ya miito ya umisionari. Wape watawa wa kiume na wa kike nguvu yako ili waweze kutoa ushuhuda katika kueneza injili kwa wote na kutoa huduma yenye upendo kwa maskini, wale walio mbali sana na wanaoteseka.

Imarisha Jumuiya ya Wakristo ili waweze kuhamasisha malezi ya umisionari wa mapadri, wa jumuiya za kitawa, na wale wanaofanya kazi za kichungaji. Ewe Kristo, Bwana wa Uijilishaji na Mwinjilishaji wa kwanza tuma Roho wako awashe moto kwa wabatizwa wote watambue wito wao wa umisionari. Tumuombe Maria Malkia wa Mitume na Misioni aweze kutangulizana nasi na kudumu na wale wote ambao wamewekwa wakfu kuwa watangazaji wa ufalme wako na kulisimika Kanisa ndani ya nchi. Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Mlinzi wa Misioni – utuombee. Mtakatifu Francisko Xavier, Mlinzi wa Misioni- Utuombee. Amina.

Sala ya Kimisionari

 

17 October 2019, 10:06