Angalisho lililotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linasema, ni marufuku kubariki "ndoa" ya watu wa jinsia moja kwa sababu ni kinyume cha mapenzi ya Mungu katika kazi ya uumbaji. Angalisho lililotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linasema, ni marufuku kubariki "ndoa" ya watu wa jinsia moja kwa sababu ni kinyume cha mapenzi ya Mungu katika kazi ya uumbaji. 

Msimamo wa Kanisa Katoliki "NO" Kwa Ndoa za Watu wa Jinsia Moja!

Angalisho kuhusu wasi wasi juu ya kubariki “ndoa” ya watu wa jinsia moja: Ni marufuku kubariki “ndoa ya watu wa jinsia moja” kwa sababu si mamlaka ya Kanisa. Na hapa hakuna ubaguzi wala maamuzi mbele kuhusiana na mielekeo ya watu hawa kijinsia. Hili ni jibu makini la wasiwasi kuhusu uwezekano wa Kanisa kubariki “ndoa ya watu wa jinsia moja” “Responsum ad dubium”.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Luis Francisco Ladaria Ferrer, S.J., Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Askofu mkuu Giacomo Morandi, Katibu mkuu wa Baraza wametoa angalisho kuhusu wasi wasi juu ya kubariki “ndoa” ya watu wa jinsia moja kwa kusema ni marufuku kubariki “ndoa ya watu wa jinsia moja” kwa sababu si mamlaka ya Kanisa. Na hapa hakuna ubaguzi wala maamuzi mbele kuhusiana na mielekeo ya watu hawa kijinsia. Hili ni jibu makini la wasiwasi kuhusu uwezekano wa Kanisa kubariki “ndoa ya watu wa jinsia moja” “Responsum ad dubium”. Ni katika muktadha huu, Mapadre hawana ruhusa ya kubariki “ndoa” ya watu wa jinsia moja wanaotaka mahusiano yao yaweze kutambuliwa na Kanisa Katoliki. Baba Mtakatifu Francisko ameridhia angalisho hili na kutaka lichapwe na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Kitume: “Amoris laetitia” yaani “Furaha ya Upendo ndani ya familia”, kifungu cha 250 anasema:

“Kanisa linaiga kwa dhati kabisa msimamo wa Bwana Yesu, ambaye kwa upendo usio na mipaka amejitoa afe kwa ajili ya kila mtu bila ubaguzi. [275] Pamoja na Mababa wa Sinodi niliangalia hali za familia ambapo ndani yake wapo watu wenye mwelekeo wa ushoga, hali ambayo ni ngumu kwa upande wa wazazi na wa watoto pia. Tungependa kwa mara nyingine tena kusisitiza kuwa, pasipo kujali mwelekeo wake wa kijinsia, kila mtu anastahili kupewa heshima kwa utu wake na anastahili kupokelewa kwa heshima na hivi “kila hali ya ubaguzi usio haki” [276] iepukwe, na hasa kila aina ya mashambulizi na ukatili. Familia za namna hii lazima zipewe kwa heshima huduma za kichungaji, ili wale wenye mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja wapate msaada wanaouhitaji ili katika maisha yao wayatambue na kuyatekeleza kikamilifu mapenzi ya Mungu. [277]”

Ikumbukwe kwamba, baraka ni sehemu ya Sakramenti ya Ndoa na ni tendo la Liturujia ya Kanisa. “Ndoa” ya watu wa jinsia moja ni kinyume cha mpango wa Mungu uliofunuliwa katika kazi ya uumbaji. Ndoa kimsingi inaundwa kwa ukubaliano kati ya bwana na bibi. Umoja, kutovunjika na uwazi kwa uzazi ni hali ya lazima za ndoa. Tofauti na uelewa huu kuhusu Sakramenti ya Ndoa ni kwenda kinyume cha kanuni maadili na mafundisho ya Kanisa. Kumbe, baraka ya Kanisa inatolewa tu kwa bibi na bwana wanaofunga ndoa kadiri ya mpango wa Mungu katika kazi ya uumbaji.

No Baraka kwa Mashoga
16 March 2021, 15:41