Siku ya Somo wa Baba Mtakatifu:Papa awatembelea wanopatiwa chanjo dhidi ya Covid
Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, kwa waandishi wa habari, Papa Francisko amesalimia waliokuwapo wakijiandaa kupata chanjo katika ukumbi huo. Baada ya mzunguko huo amesimama na kutoa zawadi ya yai la chokolati, ambalo limegawiwa kwa watu wote kwa msaada wa watu wa kujitolea, kwa kufuata lakini kanuni za hatua za kiafya zinazohitajika. Hata hivyo video fupi inaelezea yenyewe kilichojiri.
Wakati Papa anatoka nje, waliokuwapo wameweza kuimba wimbo wa matashi mema ya Siku ya mwajina wake, Mtakatifu George, ambapo Baba Mtakatifu, amesimama na kuzungumza na watu wa kujitolea katika hali ya siku kuu na upendo. Amewashukuru na kuwahimiza wandelee na jitihada zao
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Sadaka ya Kitume ya Baba Mtakatifu, wametoa shukrani kwa wale wote ambao wanaendelea kuchangia kwenye mpango wa mchakato wa chanjo ulionzishwa ukiongozwa na mada “ chanjo iliyositishwa” ambayo itaruhusu kusaidia wengi ambao wanasubiri chanjo katika nchi maskini zaidi. Mapema kabla ya saa 5:00 hivi, Papa Francisko maerudi nyumba ya Mtakatifu Marta anakoishi. Kwa siku ya leo, wahitaji hao watapewa chanjo ya pili karibu watu 600 kati ya 1400 wenye kuhitaji ambao tayari wamepata dozi ya kwanza wiki chache zilizopita.