Hija ya kitume ya Papa Francisko Slovakia:wakristo wawe wasukaji wa mazungumzo
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Katika mahubiri yake Papa amewapa onyo la kutupunguza imani katika sukari ambayo inaleta utamu wa maisha. Mbele ya Yesu huwezi kubaki umesimama ukiwa umevaa viatu miguu miwili. Kwa maana hiyo ametoa mwaliko wa kuwa katika hija ya safari daima na kwamba Kanisa linaposimam, basi lipenda. Na wakati wa kuaga Nchi hiyo Papa amewambia jinsi ambavyo anawapeleka wote ndani ya moyo wake. Habari katika picha zinaonesha matukio halisi ya siku hii.
Papa Francisko akiagana na Rais na kupanda ndege ya kurudi Roma. Mara baada ya kusali pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Slovakia, kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Šaštin Papa Francisko amerejea jijini Vatican.
Video inaonesha wakati muhimu wa Misa Takatifu katika madhabahu ya Mama Maria wa Mateso saba.
Huu ulikuwa ni wakati mwingine wa kipekee wa Papa Francisko kukutana na Jumuiya ya Warom. Jumanne tarehe 14 Septemba 2021, Papa amepata nafasi ya kutembelea Jumuiya ya Warom wanaoishi huko Luník IX. Hili ni eneo la watu maskini ambalo kimsingi linakosa mahitaji muhimu ya binadamu. Watu wote wanapaswa kushirikishwa katika mchakato wa maendeleo fungamani ya binadamu, ili kulinda na kudumisha: utu, heshima na haki msingi za binadamu Papa Francisko amesema ndani ya Kanisa hakuna mgeni wala “mtu wa kuja” wote ni watoto wa Mungu walioumbwa kwa sura na mfano wake.
Sherehe za kuaga Papa Francisko akiwa uwanjani kurudi Roma.