Kard Ouellet:Shauku ya Papa ni Kanisa la kisinodi linakuwa la Maria na kimisionari
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Akitoa hotuba yake tarehe 25 Novemba 2021 katika Mkutano wa kwanza wa Kikanisa wa Bara la Amerika ya Kusini na Caribbien ambao unaendelea hadi Dominika tarehe 28 Novemba 2021, Kardinali Marc Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu na Rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini alifungua hotuba hiyo kwa kuuliza maswali kuwa: Je ni ndoto gani ya Kanisa la Sinodi? Ni mkakati gani wa Mawasiliano: je ni njia zipi kwa ajili ya uongofu wa kimisionari
Kwa kujibu Kardinali Ouellet amesema kuwa: “Ndoto ya Papa Francisko ya Kanisa la Sinodi inahusishwa na utendaji wa Roho Mtakatifu. Papa anatutaka tujifunze kumsikiliza Roho katika ngazi zote za Kanisa: kuanzia mtaa wa mwisho katika miji mikuu ya Amerika ya Kusini hadi vyuo vikuu, parokia, vyama vya kitume na harakati za watu, n.k. Kusikiliza kile ambacho Roho Mtakatifu anasema kunamaanisha kuwa makini, kutokuwa na haraka na kuwa na ubaguzi. Baba Mtakatifu Francisko havutiwi na mtindo mpya wa Kanisa bali imani ya watu watakatifu wa Mungu. Papa anatumaini kwamba, kupitia mang’amuzi ya imani, sote tunaweza kuchangia katika kufanya upya mioyo na maisha yetu.”
Kanisa la Sinodi ni Kanisa lililo katika safari ya imani ambayo haiwezi kutenganishwa na matumaini na mapendo. Papa hatarajii programu mpya ya kichungaji kutoka kwa Baraza la Kikanisa la Amerika ya Kusini na Carribieni, lakini msukumo mpya kwa utume wa bara. Kwa upande wa Papa, mpango wa Mabaraza ya maaskofu wa Amerika ya Kusini na Carribieni (Celam) ni fursa kwa ajili ya uongofu wa kibinafsi, wa kichungaji, wa sinodi na wa kimisionari. Isisahaulike kwamba Kristo alitaka kutangazwa katika nchi za Amerika ya Kusini kwa njia ya umoja, maarufu na ya upole na mmisionari lakini mwanamke aliyezoeleka: Mama Yetu wa Guadalupe. Ni lazima tufikirie mustakabali wa Amerika ya Kusini katika mwanga wa safari ya Maria wa Makanisa yetu kwa karne nyingi”, alisisitiza Kardinali.
Kanisa la sinodi katika Amerika ya Kusini litakuwala Mama Maria. Kardinali Ouellet pia alikumbuka kwamba kuna vipimo vitatu vya Kanisa la Sinodi vilivyoainishwa na Baba Mtakatifu Francisko. Hivyo ni vile vinavyooneshwa katika sehemu ya kauli mbiu isemayo “Umoja, Ushiriki na Utume”. Kushiriki kunamaanisha kuamsha imani, ili sote tuanze safari, twende kuelekea kwa Yesu. Ni lazima tuamshe imani, tupokee zawadi ya ushirika wa Utatu, tushiriki na kila mtu, kwa upendo, ambayo ni neema ya kuwa wanafunzi. Imani ya Kikristo ni zawadi, neema kubwa sana ya kupokelewa kwa shukrani. Kardinlia ametoa wito kwamba Safari ya sinodi lazima iwe safari ya waliobatizwa waliojitolea kumshuhudia Kristo ulimwenguni kote.
Kardinali Ouellet pia amekumbusha kwamba kuanzia tarehe 17 hadi 19 Februari 2022 litafanyika Kongamano la Kitaalimungu la Kimataifa mjini Roma likilenga mada: “Kwa ajili ya taalimyngu msingi ya upadre” na kuandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu. Miongoni mwa malengo hayo ni yale ya kuchochea tafakari ya kitaalimunguna kujitolea kiutendaji, kwa kulenga hasa ubatizo, msingi wa miito yote. Kanisa la Sinodi alisema Rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, liko hai ikiwa lina mwamko wa kiutendaji, yaani, mwamko wa kuitikia kwa Bwana wake kwa imani hai, shukrani, upatikanaji, shauku kwa ajili ya Injili. Ndoto ya sinodi ya Papa Francisko si ya kiitikadi, ya kimkakati, au ya upatanisho, bali ni ndoto ya baba, ya Maria, ikolojia fungamani, ya kimisionari na ya kindugu, yenye matumaini kwa wanadamu wote. Tunashiriki ndoto yake ya kinabii ya imani hai.