Siku ya Uvuvi duniani 2021:Ni lazima kutenda pamoja kusimamisha ukiukaji haki za binadamu
Na Sr. Angella Rwezaula- Vatican
Bado kuna ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu baharini. Wito mwingine kwa mashirika ya kimataifa, serikali, makampuni kuzuia suala hili na ikiwa hatutaingilia kati inawezeka kuwa vigumu zaidi kutokomeza unyanyasaji unaotokea na gharama ya kibinadamu na kiuchumi itakuwa kubwa sana kwa sekta hiyo. Hiki ndicho kiini cha Ujumbe ulioandikwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Kibinadamu katika fursa ya Maadhimisho ya Siku ya Uvuvi Duniani Dominika, tarehe 21 Novemba 2021. Mawazo yake, hasa mwaka huu, yanakwenda kwenye nyanja za kibiashara na viwanda na kunukuu maneno ya Papa Francisko manmo Julai 2019 kwa washiriki wa Mkutano wa Ulaya wa utume wa " Stella Maris kwamba: " ... bila wavuvi, sehemu nyingi duniani watakufa kwa njaa."
Kadinali Peter Turkson akiwa sanjari na madhumuni ya siku hii tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1998 ameweka wazi sana mfumo wa maisha wa sekta hiyo ambayo inaajiri idadi kubwa ya wafanyakazi na kuzalisha moja ya bidhaa za chakula zilizosindikwa zaidi duniani yaani samaki. .. Kuingia katika ulimwengu wa wafanyakazi hawa kwa mujibu wa kardinali ni kama kujitosa katika bahari kubwa na ya kina, inayojumuisha makabila na mataifa tofauti, ya watu wanaosafiri bila kuchoka ili kujibu"mahitaji yasiyotosheka ya ulimwengu wetu. Leo, uvuvi wa kibiashara na wa viwandani umenaswa katika mtandao wa matatizo na changamoto"unaohusishwa na ukiukwaji wa haki na janga hili.
Lakini ni juu ya haki ambazo Kardinali amejikita nazo, kwa sababu ameeleza kwamba licha ya mikataba na juhudi za kimataifa, wakati wavuvi wanaondoka bandarini kuingia kwenye maji,na kusafiri maili na maili kutoka fukwe wa bara bila kuwa na uwezo wa kushuka mara kwa mara kwa miaka, na wanakuwa mateka wa hali ngumu sana kuwafuatilia. Hizi kazi ambazo hazina mwisho wa mchana na usiku kwa kuvua samaki iwezekanavyo, katika hali yoyote ya hali ya hewa, ya uchovu mwingi na majeraha, fikiria tu kwamba kuna vifo zaidi ya 24,000 kwa mwaka, kwa maana hiyo sekta ya uvuvi ni mbaya , ambayo familia hazipati fidia, bila kusahau ukweli kwamba miili mara nyingi huzikwa baharini bila kupata upendo wa ndugu zao karibu au utunzaji.
Kama Kanisa Katoliki , linatambua baadhi ya ubora katika hali ya kibinadamu na kazi ya wavuvi; pamja na hayo yote , wanazingatia kuwa kuna bado ukikwaji mkuwa wa haki za watu baharini. Kwa mara nyingine tena , wanatoa wote kwa mashirika ya kimataifa, kwa serikali za nchi , jamii ya kiraia na wadau mbali mbali washrika wa uvuvi na mashirika yasiyo ya kiserikali ili waunganisha nguvu zao kusimamisha ukiukwaji huo. Matatizo ambayo yanikumba sekta ya uvuvi yamesukana sana. Ikiwa hawazingatii nia zao katika kuendelea kwa nyanyaso , na ukiukwaji baharisi na bila kufanya kazi pamoja na wavuvi ili wahakikishwe na kusaidiwa, inawezekana kugeuka mgogoro mkubwa wa kutokuundoa na gaharama ya kibinadamu na kiuchumi inaweza kuwa kubwa kwa viwanda. Kwa kufuata mafundisho ya Injili na Mafundisho ya Kanisa Katoliki, Vatican daima imekuwa na matashi mema ambayo yanahusu kuheshimu haki hizi za kibinadamu na ndiyo hali yenyewa kwa ajili ya maendeleo jamii na kiuchumi ya nchi yoyote ile. Hadhi ya binadamu inapoheshimishwa na haki zake kutambuliwa na kuthibitishwa, ubunifu pia unachanua na kujitegemea na mtu binadamu anaweza kujifafanua kwa kuanzisha mambo mengi kwa ajili ya wema wa pamoja (rej. Fratelli tutti 22).
Ujumbe wa Kardinali Turkson wa siku hiyo, unatoa mwaliko kwa Mapadre wanaowahudumia mabaharia, wavuvi pamoja na familia zao, watu wanaojitolea zaidi kuwadumia mabaharia na wavuvi katika bandari huku wakitembelea meli wa Stella Maris waendelee kwa huruma ya utume wao kupokea wavuvu kwa kutambua katika nyuso zao uso wa Yesu Kristo mteswa na kutoa msaada kwa kiroho na kimwili kwa vifaa. Kama asemavyo Papa Francisko katika Waraka wa “Fratelli tutti”: kuishi na sintofahamu mbele ya uchungu sio uachaguzi mzuri, hatuweza kuacha yote pembezoni mwa maisha” Hili linapaswa kutukasirisha hadi kutufanya tutoke katika utulivu wetu na kutuhusisha katika mateso ya binadamu” (Ft 68). Katika Siku ya Uvuvi duniani, haris zetu kwa sababu ya ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu baharini inakuwa ndiyo kiini kulingana na haki za binadamu na kazi ya wavuvum kwa sababu kama alivyosema Papa Francisko mnamo Juali 2019 kwa washiriki wa Mkutano wa Ulaya wa Utume Baharini wa Stella Maris, “…bila wavuvi, sehemu mbali mbali wangekufa kwa njaa”.