2022.01.28 taccuini Nogara 2022.01.28 taccuini Nogara 

Shajara za mkurugenzi wa majumba ya makumbusho zinaonesha mwanga na giza la shoah

Shajara kama arobaini hivi ambamo Mkurugenzi wa zamani wa Majumba ya Makumbusho Vatican,aliweza kuandika mawazo na mikutano ya kila siku.Kwa mujibu wa mhusika wa Pango Hifadhi la la Jumba la Makumbusho Vatican,amesema ni wajibu wa kutunza na ambaye alipata zawadi ya shajara hizo kutoka kwa familia.Balozi Osio anakumbusha taarifa zilizojikita katika jitihada ya kulinda wasomi wa Kiyahudi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mara ya kwanza wameonesha filamu ndogo inayoonesha shajara 42 za Bartolomeo Nogara aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa Majumba ya Makumbusho Vatican. Mhusika huyo aliongoza taasisi hiyo tangu 1920 hadi kifo chake kilichotokea mnamo 1954, na alikuwa na tabia ya kuandika mawazo yake na mikutano yake kila siku. Alikuwa akienda na shajara yake daima kwa mujibu wa uthibitisho wa Marta Bezzini, mhusika wa Pango hifadhi la kihistoria la Majumba ya Makumbusho Vatican na ambaye mnamo 2018 alipokea zawadi hiyo kutoka kwa familia ya huyo Nogara.

Shajara unaonesha kipindi kirefu cha mapapa watatu

Ni hati ambazo zinaonesha thamani kubwa ya safari ya upyaisho iliyoweza kufanya uzoefu wa miaka hiyo ya majumba ya makumbusho ya Vatican, si tu kwa upande wa usimamizi, lakini hata ule wa kuhifadhi, kuorodhesha na kupyaisha. Kwa kufungua vifungu vifupi vilivyomo kwenye kurasa katika shajara ndogo ndogo, Bezzini anathibitisha kuwa vinafafanua kipindi kirefu cha mapapa watatu.  Kuanzia na ule wa Papa Benedikto XV; Pio XI na Pio XII”. Hadi kufikia kwamba kila sura inaonesha shughuli ya tangu  asubuhi na pia ya  mchana.

Herminie Speier ni mwanamke wa kwanza kufanya kazi Vatican

Balozi Bernardino Osio, mjumbe wa familia ya Nogara, aliita kazi hiyo kuwa ni  mantiki muhimu. Katika shajara hizo pia zinaonesha kukutana na watu ambao walimwomba wakubaliwe kuwa kama walinzi wa majumba ya makumbusho. Mawasiliano yaliongezeka hasa wakati wa Vita vya II vya Kidunia, ingawa kiukweli yalianza miaka ya 1930, mara  baada ya sheria za kwanza za ubaguzi zilizotungwa mnamo 1933 na Reich ya Tatu ambayo iliamuru kufukuzwa kwa maafisa wasio Waaryani. Ni katika muktadha huo, mwaka 1934, ambapo mwanamke mmoja aliajiriwa kwa mara ya kwanza mjini Vatican. Huyu ni Hermine Speier, ambaye, kama Myahudi, aliondolewa kutoka Taasisi ya Archaeological ya Ujerumani huko Roma ambako alifanya kazi tangu 1928.

Kuokoa wasomi wa Kiyahudi

Osio anasema kwamba alifika kwenye Makumbusho ya Vatican kwa idhini ya Papa Pius XI, kama msimamizi wa maktaba ya picha, jukumu aliloshikilia hadi kustaafu kwake katika miaka ya 1950, baada ya uongofu wake kuwa mkatoliki wakati wa Ukombozi. Bezzini anathibitisha kuwa “yaliyomo kwenye shajara yanaorodheshwa. Mchakato unafuata mpangilio wa wakati: tunasoma na kuandika, tukijaribu kutambua watu waliotajwa na matukio muhimu zaidi yaliyotajwa kwenye kurasa katika miaka hii yote”. Kwa wazi, umakini hauelekezwi tu kwa kipindi cha miaka miwili 1943-1944. Ingawa Osio anatoa onyo kuwa hata wakati wa utawala wa Kinazi wa Roma kulikuwa na hatua kadhaa za Nogara kuokoa wasomi wa Kiyahudi na wasomi .

Mawasiliano na Balozi wa Ujerumani Ernst von Weizsäcker na mtaalamu wa vitu vya kale Ludwig Pollak hayakufaulu. Na hata kwa msomi Mario Segre, ambaye pia alipendekezwa na Sekretarieti ya Vatican na  Monsinyo  Montini( ambaye baadaye alikuwa Papa Paulo VI. Wote wawili waliishia Auschwitz. Katika hali nyingine, hata hivyo, matokeo yalikuwa tofauti. Wengi waliandikishwa kuwa Walinzi wa Palatine ambao katika kipindi hicho walikuwa wamefikia wanachama 1,500 ikilinganishwa na 3-400 katika miaka ya nyuma alisisitza ana Osio.

Mambomu yaliyoanguka mjini Vatican 1943

Kuna vipindi vingi vilivyoibuliwa na maandishi ya Nogara. Miongoni mwa hawa, Osio anakumbuka mabomu yaliyoanguka Vatican katika majira ya baridi ya 1943 na hofu kwamba majeshi ya Ujerumani yalikuwa tayari kumteka nyara Papa na kumpeleka Ujerumani. “Taarifa kutoka kwa idara za ujasusi za Uingereza na Marekani, alisema zilimfanya Monsinyo Montini kwenda kwenye nyumba ya mkurugenzi wa makumbusho wakati wa usiku kumtazama akiwa amewasha moto mkononi mwake kwa ajili kuona hali ya usalama huko Vatican ili kumjificha Papa Pio XII".

29 January 2022, 15:26