Papa Francisko amemteua Monsinyo Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Papa Francisko amemteua Monsinyo Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. 

Askofu Mkuu Mambé J-Sylvain Emien, Balozi wa Vatican Nchini Mali

Askofu mkuu mteule Mambé Jean-Sylvain Emien alizaliwa tarehe 16 Septemba 1970 huko Jacqueville, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa kwenye Jimbo Katoliki la Yopougon, nchini Pwani ya Pembe “Ivory Coast”. Tarehe 2 Februari ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa Monsinyo Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Mali na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Mambé Jean-Sylvain Emien alikuwa ni mshauri wa Ubalozi wa Vatican. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Mambé Jean-Sylvain Emien alizaliwa tarehe 16 Septemba 1970 huko Jacqueville, Pwani ya Pembe.

Askofu mkuu Mambè ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali.
Askofu mkuu Mambè ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa kwenye Jimbo Katoliki la Yopougon, nchini Pwani ya Pembe “Ivory Coast”. Askofu mkuu mteule Mambé Jean-Sylvain Emien, ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Alianza utume wake katika diplomasia ya Kanisa tarehe Mosi Julai 2005. Na tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na wajibu wake huko nchini Angola, Nigeria, New Zealand, Hispania, Jamhuri ya watu wa Czech, Guinea na Mali.

Balozi Mali

 

07 February 2022, 15:06