Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Maurice Muhatia Makumba kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Kisumu, Kenya Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Maurice Muhatia Makumba kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Kisumu, Kenya 

Askofu Mkuu Maurice M. Makumba Jimbo Kuu la Kisumu, Kenya

Askofu mkuu mteule Maurice Muhatia Makumba wa Jimbo kuu la Kisumu alizaliwa mwaka 1968. Tarehe 15 Oktoba 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Kakamega. Tarehe 19 Desemba 2009, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Nakuru na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 27 Februari 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Maurice Muhatia Makumba wa Jimbo Katoliki la Nakuru, nchini Kenya, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Kisumu kuanzia tarehe 18 Februari 2022. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Maurice Muhatia Makumba wa Jimbo kuu la Kisumu, Kenya alizaliwa tarehe 19 Mei 1968 huko Lirhanda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 15 Oktoba 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Kakamega.

Tarehe 19 Desemba 2009, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Nakuru na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 27 Februari 2010. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 20 Novemba 2021 akatemteua kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Kisumu. Kumbe, kwa muda wa miaka 27 amelitumikia Kanisa kama Padre na miaka 11 kama Askofu, akifundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu. Tarehe 18 Februari 2022, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kisumu.

Jimbo kuu la Kisumu

 

18 February 2022, 15:04