Chuo Kikuu Katoliki kutoa madawa kwa Papa jwa msaada mahitaji ya dawa Tanzania
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Dawa muhimu za kuokoa maisha zitawasili hivi karibuni katika hospitali nchini Tanzania, vifaa hivyo vikiwa ni pamoja na bandeji, mafuta kwa ajili ya wanaoungua na vifaa vingine vilizotolewa zawadi kwa Papa Francisko na Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu. Sehemu ya kwanza ya mchango huo iliyotangazwa tarehe 5 Novemba mwaka jana, ilitolewa, wakati Papa alipotembelea Hospitali Gemelli, Katika Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu kuadhimisha Misa kwa ajili ya kumbu kumbu ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Kitivo cha Tiba na Upasuaji. Mnao tarehe 24 Januari 2022 mchana Kardinali Kardinali Konrad Krajewski Msimamizi wa Sadaka ya Kitume ya Papa akiwa pamoja na Askofu Mkuu Nunzio Galantino, Rais wa Utawala wa Urithi kitume Kitume walipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Papa.
Makabidhiano haya yalifanyika katika mkutano usio rasmi katika uwanja wa Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican mahali anapokaa Papa Francisko , kwa masanduku matatu ya madawa ya lazima na vifaa muhimu vya matibabu, vilivyo wakilishwa na wajumbe kutoka Chuo Kikuu katoliki, wakiongozwa na mkuu wa Chuo hicho Dk. Franco Anelli, mkurugenzi mkuu, Paolo Nusiner, mkuu wa Kitivo cha Tiba na Upasuaji, Dk. Rocco Bellantone, na Dk. Marcello Pani, mkurugenzi wa duka la dawa la hospitali ya Gemelli.
Kwa mujibu wa Mkurugenia Anelli ameelezea juu ya zawadi hiyo na kuhusu uwasilishaji mwingine wa sehemu ya pili ya dawa unaotarajiwa katika wiki zijazo, ambazo msimamizi wa Kitume ataweza kutuma katika vituo vya Lebanon, Siria na Sudan, lakini sehemu ya kwanza inatumwa katika vituo vya afya nchini Tanzania. Hivi ni vifaa vya matibabu na dawa ambazo ni kawaida kwa upande wa Ulaya kuwa navyo majumbani lakini, kwa upande mwingine, katika nchi nyingi ni vigumu kupata au havipatikani kwa urahisi, ameeleza Mkurugenzi Anelli kuhusiana na dawa na vifaa hivyo.
Kwa mujibu wake amesema Kiukweli, jambo moja ambalo Papa Francisko mara nyingi anasisitiza kwa mkuu wa Chuo Kikuu katoliki ni kwamba moja ya vipengele vya mshikamano na tahadhari kwa wengine ni kukumbuka kuwa jambo la kawaida katika nchi tajiri, kama vile kupata mahitaji msingi, maji, chakula kwa upande mwingine katika nchi nyingine maskini ni shida sana na wakati mwingine ni dhahiri kukosa kabisa.Kutokana na tafakari hiyo ndipo wao waligunda kuwa hata vitu vidogo vidogo kama hivyo kwa upande wa Ulaya vinaweza kuwa msaada mkubwa katika nchi nyingine zenye uhitaji au kukosa kabisa.
Dawa zilizotolewa, na zilizokubaliwa kutoka duka la dawa la hospitali ya Gemelli na Famasi ya Vatican kwa hakika ni antibiotics, antihistamines na cortisones, antiseptics na disinfectants, analgesics na antispasmodics, anti-inflammatory na antipyretic, anticoagulants, diuretics, antihypertensive na hypoglycemic agents, antidiarrheals, gastroprotectors, antidiabetics, antiepileptics, creams mbali mbali kwa ajili ya majeraha ya kuunguzwa na moto, mavazi ya wauguzi na wahudunumu na bandeji. Vifaa hivyo vitaweza kufikia vituo mbali mbali vya kiafya vvya Tanzania, Lebanon, Siria na Sudan.