Kard.João Braz de Aviz:Mali za kiutamaduni za Kanisa zihifadhiwe&kulindwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali João Braz de Aviz, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume wakati wa uwakilishi kwa vyombo vya habari Vatican, kuhusu lengo la Mkutano wa Kimataifa unaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Karama na ubunifu. Kuorodhesha, usimamizi na mipango ya ubunifu kwa ajili ya urithi wa kiutamaduni wa jumuiya maisha ya Watawa”, utakaofanyika kwa siku mbili mnamo tarehe 4 na 5 Mei 2022, na ambao umeaandaliwa na Baraza la Kipapa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume pamoja na Baraza la Kipapa la Utamaduni amesema kwamba ni kutaka kuibua matatizo ya msingi ya usimamizi wa urithi wa kiutamaduni wa jumuiya za watawa, kuwasilisha, katika eneo la utafiti, mazoea mazuri ya ulinzi na uimarishaji ulioanzishwa na taasisi zenyewe au na vituo vya utafiti vya vyuo vikuu, na kuhamasisha kampeni ya utaratibu, kuorodhesha mali hizo ambazo huzifanya zijulikane kwanza na taasisi zenyewe na kuhakikisha uhifadhi wao mzuri.
Kardinali De Aviz alisema kwamba leo hii inaonekana wakati umefika wakati wa kuchanganya rasilimali, katika ngazi ya kitaasisi na katika ngazi ya watawa, ikijumuisha katika usemi huo wa taasisi za kitawa, monasteri, taasisi za kilimwengu na jumuiya za maisha ya kitume, na hivyo, hata kwa ushirikiano wa pande zote mbili za Mabaraza ya kipapa zenye uwezo na uwepo katika kamati ya kuhamasisha ya Baraza la Maaskofu wa Italia, na wa chuo kikuu cha Kipapa. Kwa maana hiyo Kardinali ndipo ametoa mwaliko kwa wanaume na wanawake waliowekwa wakfu kutafakari juu ya thamani ambayo mali ya kiutamaduni inaendelezwa namna gani kama ujumbe katika jamii ya leo huu, juu ya hatima yao ya mwisho, juu ya uhusiano wao walio nao na karama ya kila taasisi na mwelekeo wa kinabii wa karama ile ile. Kardinalo Avis aidha amebainisha kuwa wanafahamu kwamba hakuna mipango ya usimamizi ulio mzuri wa urithi wa kiutamaduni na taasisi za watawa, lakini pia ni vigumu kuzijua, kuziweka wazi, kama ilivyo vigumu kuhesabu na kuelezea urithi wa watu waliowekwa wakfu.
Akiendelea na ufafanuzi huo Kardinali kwa maana hiyo amesisitiza kuwa katika uwanja huo kuna ugumu wa lengo katika kuratibu shughuli za kawaida, kama vile hesabu/ orodha ya jumla ya urithi wa kiutamaduni wa watawa, hata katika ngazi ya kitaifa, ijapokuwa hakuna ukosefu wa vyombo vya uratibu, kama vile mikutano ya kitaifa ya wakuu wa mashirika makuu. Kardinali De Aviz vile vile alisisitiza kwamba wasisahau kuwa tofauti na makanisa mahalia yanayoratibiwa na askofu wa jimbo, taasisi na nyumba za watawa hufurahia uhuru zaidi, kwa sababu ziko chini ya udhibiti wa wakuu wao na wa mashirika yao makuu na Taasisi za waliowekwa wakfu, katika dhahania zilizoamuliwa na haki. Hata hivyo, taasisi zote, monasteri na jumuiya watawa na vyama vya kitume wote wanaitwa kuunganisha nguvu zao ili kuchukua hatua muhimu ambayo ni ya kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za picha za mali za kiutamaduni, ambazo manufaa yake hujitokeza kwa mfano katika tukio la kurejesha kazi zilizoibiwa au kurejesha mali iliyoharibiwa na majanga ya asili.
Naye Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni, akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari amesema kwa mfano wenye maana sasa ni wa ushirikiano kati ya mabaraza mawili ya kipapa. Kwa upande wa Ulaya, mbele ya urithi mkubwa wa kiutamaduni, unaojumuisha mali isiyohamishika na mali zinazohamishika, kumbukumbu na maktaba, ambayo inahitaji umakini zaidi katika suala la ulinzi na uboreshaji, idadi ya watu waliowekwa wakfu katika miaka 30 iliyopita imerekodi kupungua kwa zaidi ya asilimia 57% katika upande wa kike, na asilimia 44% katika upande wa kiume, ametaja takwimu Kardinali. Mbele ya kukabiliwa na upungufu huo, Kardinali Ravasi amesema ni wazi kwamba, kwa kuzingatia urithi wa kiutamaduni, ni muhimu kuamsha haraka vyombo vya uchunguzi na ulinzi, kuanzia na ufahamu kwamba urithi wa kiutamaduni pia unaweza kuchukuliwa kuwa rasilimali, mali ya ushuhuda ambao kwa kufuata karama ya kuitangaza tena kwa upya, kutafakari kwa upya na kuifanya kuwa ya sasa zaidi.
Hata hivyo miiongoni mwa mambo yatakayozungumzwa katika mkutano ujao Kardinali, Ravasi amejikita zaidi hasa kufafanua mada ya matumizi ya kikanisa ya majengo ambayo hayatumiki tena, suala ambalo ni nyeti sana kwa sababu sekta za kidini ni kubwa kimapokeo na kuachwa kwao amesema kunahusisha hali ya uozo, kama machafuko ya kweli ya kungo cha mijini. Katika matumizi ya majengo yake, Kanisa lina moja ya maonesho yake ya moja kwa moja katika mazingira ya ndani, na matumizi potofu, ya kubahatisha au ya kubinafsisha daima ni sababu ya kueleweka kashfa kwa jumuiya za kiraia, na matokeo ya mara kwa mara katika magazeti yenye kutafuta maslahi ya kikanda. Vile vile Kadinali kwa kutoa dokezo alisisitiza kwamba sehemu ya nne ya mkutano huo “itajaribu kutambua mazoea mazuri ya kutumia tena ambayo yanaheshimu matumizi ya awali ya majengo, ambayo kwa hiyo yanapendelea kusudi jipya la kijamii, upendo na kiutamaduni.