Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu 

Kard.Grech:Mmo ndani ya Sinodi na ulizeni maswali yenye kujenga

Katika hotuba kwa njia ya video ya Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu kwa viajana wa vyuo vikuu ambao watazungumza na Papa Februari,24 kwa njia ya Mtandao kuhusu hali halisi ya wahamiaji na masuala ya mazingine na ya kiuchumi na zaidi mipango mengine ya maisha na kuwashauri kuuliza maswali yanayostahili kwa maana wao wamo ndani ya Sinodi na Kanisa linawasikiliza.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Muwe  na hekima na kujiuliza maswali yanayostahili ndiyo mwaliko wa  Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, aliyowashauri kwa njia ya video, Wanafunzi wa vyuo vikuu, wa Bara la Marekani yote Kusini na Kaskazini ambao tarehe 24 Februari 2022 kutokea Chuo Kikuu cha Loyola huko Chicago wanafanya mkutano wa kisinodi kwa kuongozwa na mada: “Kujenga madaraja Kaskazini hadi kusini”, ambapo sehemu ya mkutano huo, atashiriki Baba Mtakatifu kwa njia ya Mtandao. Papa ataungana nao ili kuweza kujibu baadhi ya maswali ambayo watamuuliza vijana hao.

Katika tafakari ya Kardinali Grech amesema, vina wanao mikononi mwao wakati ujao, wana maono ya mipango ,lakini pia hata wana hofu za kutokuona ndoto zao na maono yao yanatimilizika, hivyo anawaomba wanafunzi kutumia ufunguo wa hekima na kuwa na mahusiano na Papa.  Kardinali, Grech akifikiria juu mchakato wa Sinodi  unaeondelea, amesema kuwa Kanisa lipo linasikiliza maswali ya Watu wa Mungu na kwamba Kanisa kwa sas ana  linajitahidi kusikiliza maswali ya watu wote na kwao pamoja wannajiuliza, hivyo ni matarajio yake kwamba mkutano wao unaweza kutoa mchango katika mchakato wa safari ya Sinodi. Amehitimisha ujumbe wake kwa njia ya video  kwa kutoa wito kwa vijana wote na kuwashauri washiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kisinodi, katika hatua ya kwanza ya mashauriano ambapo wao wanaweza kuweli kushirikia katika makanisa mbali mbali mahalia.

Ili kujiandaa na masunguzo na Papa katika siku hizi, vikundi 7 vya wanafunzi 20 kila kimoja kinafanya kazi: 3 kutoka Marekani na Canada, 1 kutoka Mexico, 1 kutoka Caribbean na Amerika ya Kati, 1 kutoka Brazil na 1 kutoka Amerika ya Kusini. Kila kikundi kimejumuisha vijana kutoka vyuo vikuu tofauti, vya kibinadamu na maeneo ya sayansi, ambao wanashiriki historia zao, wakitafakari juu ya maslahi yao ya kawaida na kutambua mipango thabiti kwa pamoja ili kushirikiana pamoja. Kila kundi litachagua wanafunzi kama wawakilishi wao ili kufanya mazungumzo na Papa Francisko. Malengo ya mpango wa tarehe 24 Februari kuwezesha mikutano ya kweli na midahalo ya kujenga kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu, kuwapa sauti ya kukuza ujenzi wa madaraja na uhusiano wa kudumu unaoleta maelewano ya pande zote, kukuza suluhishi madhubuti na mipangao uendelevu wa mazingira, haki ya kiuchumi na maendeleo shirikishi ya watu, kupendekeza mtindo wa sinodi ya kusikiliza na utambuzi, ili kutunza uzoefu na mitazamo ya wanafunzi, hasa wahamiaji au wale wanaotoka katika familia za wahamiaji.

24 February 2022, 15:50