Migogoro nchini Ukraine. Migogoro nchini Ukraine. 

Kard.Parolin:Mwenye jukumu katika ulimwengu azuie janga la vita

Katibu wa Vatican ametoa neno baada ya shambulizi la Urusi huko Ukraine:“Bado kuna muda kwa ajili ya mapenzi mema na kwa ajili ya mazungumzo”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Urusi imefanya  uvamizi nchini Ukraine kwenye mgogoro ambao umeendelea kwa siku hizi, kwa kuipiga miji na vituo kadhaa, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican amethibitisha kwa vyombo vya habari Vatican  kuwa: “Mbele ya kuongezeka kwa  mgogoro wa Ukraine, maneno ya Baba Mtakatifu aliyotamka jana baada ya Katesi yake, yanasikika kabisa kwa dhati”.  Papa alionesha “uchungu mkubwa, huzuni na wasiwasi”. Na aliwaalika sehemu zote husika zijiepushe na kitendo chochote kinachosababisha mateso zaidi kwa watu, kudhoofisha kuishi pamoja kati ya mataifa na kudharau sheria za kimataifa”.

Mwenye jukumu mikono la ulimwengu azuie janga la vita

Wito huo kweli ni wa dharura baada ya vifaru vya Urusi na wanajeshi kuvuka mpaka na kuingia nchini Ukraine.  Kardinali amesema “hiki  ni kile ambacho vita kamili huenda kwa bahati mbaya kuwa halisi, "lakini bado kuna wakati wa kuwa na mapenzi mema, bado kuna nafasi ya kufanya mazungumzo, bado kuna nafasi kwa ajili ya zoezi la hekima ambalo  huzuia kuwepo kwa maslahi ya washiriki, hulinda matamanio halali ya kila mtu na kuuepusha ulimwengu kutokana na wazimu na vitisho vya vita. Sisi waamini hatupotezi matumaini juu ya mwanga wa dhamiri ya wale ambao wana hatima za ulimwengu mikononi mwao. Na tunaendelea kuomba na kufunga Jumatano ijayo ya Majivu kwa ajili ya amani nchini Ukraine na ulimwenguni kote”.

24 February 2022, 17:02