Tafuta

Wakimbizi katika mwendo Wakimbizi katika mwendo 

Kazi kwa ajili ya wote,ujumuishi wa wahamiaji na wakimbizi

Chapisho la taarifa kutoka katika kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu.Mwezi Januari ilijikita kutoa taarifa juu ya fursa za kutazama wakati ujao wa jamii yetu kwa njia ya kazi.

Na Angella Rwezaula –Vatican.

Katika kipindi hili kikubwa cha janga katika kiuchumi na kijamii, kinawaliisha sehemu kubwa sana na changamoto kwa ngazi za kijamii, lakini na kuwakilisha urahisi wa fursa za  jamii yetu. Katika kipindi hiki kigumu kinatahiji kuwa na umakini kwa namna ya pekee ya masuala ya Kanisa. Ndivyo Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu inakilisha katika taarifa yao ya mwezi Februari 2022 kwa kijikita na mada ya “ Kazi kwa ajili ya wote, kujumuisha wahamiaji na wakimbizi. Ili kuweza kujenga wakati ujao ulio na haki ambao kuwa binadamu inapewa kipaumbele kwamba ni lazima kuacha dhana ya sasa ya kazi kama njia inayolenga kuzalisha na kurudi kwa asili ya actus personae yaani  kitendo cha mtu. Kazi ni katika huduma ya mwanadamu, na si kinyume chake. Kwa dhana hii, Kanisa Katoliki linatambua wajibu wa kufanya kazi, ili kuchangia maendeleo ya binadamu, na haki ya kufanya kazi, ili kujikimu mwenyewe na familia yake.

Kuwalinda wanaoingia kwenye soko la ajira.

Wale ambao hawana ajira wana hatari ya kujikuta wameachwa kwenye kando ya jamii. Kuanzia msingi huu, taarifa hii inatazama changamoto kuu ambazo wahamiaji na wakimbizi wanakabiliana nazo wanaposhughulika na ulimwengu wa kazi. Uangalifu hasa unaoneshwa kulipwa gharama kwa athari za janga kwenye aina hizi. Kutengwa kwao katika ajira yoyote kutnachunguzwa, na matokeo yake ya kuwa na  haja ya kufanya kazi kwa njia isiyo ya kawaida na ya hatari. Taarifa hiyo pia inawasilisha mazoea mazuri yanayolenga kuwezesha upatikanaji wa kazi, pamoja na kuwalinda wanaoingia kwenye soko la ajira.

Tume ya Vatican COVID-19

Kwa kuzingatia umuhimu mkubwa wa kazi katika kukuza ghadhi na maendeleo fungamani ya binadamu, mnamo Novemba 2021 Tume ya Vatikani COVID-19 ilizindua Mpango Kazi kwa Wote. Na Tume ya Vatican  inakusudia kuanzisha, kwa kushirikiana na jumuiya za kikatoliki duniani kote, njia ya pamoja ya utambuzi juu ya mustakabali wa ajira na mabadiliko muhimu ya kimuundo, ili kuandaa mustakabali ambao kuna kazi kwa wote. Jumuiya za Wakatoliki wa maeneo mahalia zimeonesha wasiwasi mkubwa juu ya kuzorota, wakati wa janga hilo, la kukosekana kwa usawa wa kijamii na kiuchumi na kiikolojia tayari katika sekta ya kazi, na jinsi virusi vyenyewe vimebadilisha ukosefu huu wa usawa kuwa mtandao wa kuimarisha dhuluma. Kwa hivyo, jumuiya hizi za mahalia zimesisitiza haja ya mabadiliko makubwa katika enzi ya baada ya UVIKO-19. Kwa kuzingatia mashaka na shuhuda hizi hasa zinazotoka pembezoni mwa jamii, na Tume ya Vatican CVC-19 itaunganisha waunda mabadiliko na mazoea mazuri kutoka ulimwenguni kote ili kupendekeza njia shirikishi kuelekea siku zijazo, kuanzia uundaji wa nafasi za ajira ambazo ni za ubora,  yenye heshima, endelevu na thabiti. Masuluhisho haya yanatungwa kuchukua umbo la rasilimali za kichungaji zinazotungwa kwa kiwango cha ndani, na kwa kuzingatia tafakari bora zaidi za kisayansi na kitheolojia zinazopatikana, pamoja na uwezo wa kuhamasisha hatua za pamoja na matumaini ya maisha bora ya baadaye.

Papa Francisko

Katika jamii iliyoendelea kweli, kazi ni sehemu ya lazima ya maisha ya kijamii, kwa sababu sio tu njia ya kupata mkate, lakini pia njia ya ukuaji wa kibinafsi, kuanzisha uhusiano mzuri, kujieleza, kushiriki zawadi, kujisikia. kuwajibika kwa ajili ya kuboresha ulimwengu na, hatimaye, kwa kuishi kama watu. Kwa maneno haya yaliyochukuliwa kutoka kwa Waraka wa Ndugu Wote (n. 162), Papa Francisko anatuachia ujumbe wazi juu ya umuhimu wa kazi kwa mustakabali wa binadamu. Ili kujiondoa katika dhiki hii na ndoto ya ulimwengu bora zaidi, Baba Mtakatifu anatuomba sisi watu wa Mungu, “kufanya udugu kuushinda ubinafsi”; kusikiliza “kilio kinachoinuka kutoka pembezoni mwa jamii” na kuwalenga wale walio pembezoni, kuwa ni washiriki hai katika mchakato wa mabadiliko. Kama ilivyosemwa na Papa Francis katika Laudato si '(n. 128), "kusaidia maskini kwa pesa lazima iwe suluhisho la muda la kushughulika na dharura. Lengo la kweli linapaswa kuwa kila wakati kuwaruhusu maisha yenye heshima kupitia kazi ”.

Athari za mgogoro kiuchumi kwa wahamiaji

Katika ujumbe wake kwa Siku ya Amani Duniani 2022, Papa Francisko alisisitiza kwamba athari za mgogoro katika uchumi usio rasmi, ambao mara nyingi huhusisha wafanyakazi wahamiaji, umekuwa mbaya. Wengi wao hawatambuliwi na sheria za kitaifa, kana kwamba hazikuwepo; wanaishi katika mazingira hatarishi kwa ajili yao na familia zao, wakikabiliwa na aina mbalimbali za utumwa na bila mfumo wa ustawi unaowalinda”. Baba Mtakatifu anatuuliza tuangalie ni wafanyakazi wangapi wahamiaji wanaokidhi mahitaji ya kimsingi ya jamii zilizoendelea zaidi. Wengine hujaribu kuishi bila kazi thabiti, na mara nyingi ni wahasiriwa wa unyonyaji. Wakati huo huo, katika kitabu Hebu turudi kwenye ndoto, Papa Francisko anathibitisha kwamba katika nyanja hizi za kuwepo hukaa, hata hivyo, harakati za  kijamii, ya parokia na ya elimu yenye uwezo wa kuweka watu katikati, na kuwafanya wahusika wakuu tena. Ukweli huu hujaribu kubadilisha udhalimu kuwa uwezekano: Ninawaita washairi wa kijamii anahitimisha Baba Mtakatifu. Katika kutafuta kwao utu na kukataa kwao kujihusisha na udhalimu, anaona chanzo ambacho mabadiliko yanatoka. Kutokana na msukumo huu taarifa hii inakuwa hai, ambayo inakusudia kutoa sauti kwa hawa washairi wa kijamii. Kwa maelezo zaidi:

https://migrants-refugees.va/2022/02/10/work-for-all-including-migrants-and-refugees/

11 February 2022, 17:13