Wajumbe wa Baraza la kawaida la Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu. Wajumbe wa Baraza la kawaida la Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu. 

Mchakato wa Sinodi:Tathimini ya kwanza na changamoto

Tarehe 26 Januari iliyopita lilifanyika Baraza la XV la Kawaida la Sinodi ya Maaskofu kwa njia ya mtandao ili kutathimini mwendelezo wa mchakato ulioanzishwa mwezi Oktoba.Mapya yamekubaliwa kwa furaha lakini kuna changamoto zinazopaswa kukabiliwa na pia ukosefu wa uhakika na utambuzi ambao uongofu wa kisinodi unaalika kila mbatizwa katika mchakato huo kuhitaji kipindi kirefu cha kufanya mang'amuzi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuna kutosheka  katika umbo la Baraza la kawaida la Sinodi ya Maaskofu baada ya miezi mitatu tangu kuanza kwa mchakato wa Sinodi kwa ajili ya Kanisa katika safari. Mapya katika mchakato huoni uzoefu ambao unaibua furaha kubwa na mwendelezo lakini hata idadi kubwa mashaka nachangamoto za kubaliana nazo. Ndiyo mambo yaliyoelezwa katika taarifa ambayo imefupishwa ya mkutano uliofanyika hivi karibuni tarehe 26 Januari 2022 na ambao uliendelea kwa mikutano kumi tano kwa njia ya mtandao iliyoandaliwa kati ya mwezi Novemba na Desemba na Sekretarieti Kuu ya Sinodi na wahusika kwa ajili ya Sinodi ulimwenguni kote. Ikumbukwe kwamba mara baada ya kuzinduliwa na Papa mnamo tarehe 9 na 10 Oktoba jijini Vatican, Sinodi ilianza katika hatua ya kijimbo mnamo tarehe 17 Oktoba 2021, katika Makanisa mahalia kwa mchakato wa kufanya mang’amuzi,  kiini kikiwa ni kusikiliza na kufanya mashauriano na watu wa Mungu.

Kuna furaha na shauku katika nchi za Bara la Afrika, Amerika Kusini na Asia

Katika taarifa hiyo pia inabainisha kwamba leo hii kuna majimbo mengi sana na hali halisi za kikanisa ambazo zimeanza tayari mchakato wa Sinodi na kuna shauku kati ya walei na watawa ambao wanaendeleza maisha kwa kuanzisha mambo mengi sana ili kuhamasisha mashauriano na mang’amuzi ya Kikanisa. Ishara ya tumaini na kazi ya Roho Mtakatifu ambaye anaendeleza kubadili wote ambao wamejihusisha kama wajumbe wa jumuiya moja ya kikanisa. Kutoka Kanda hadi kanda ulimwenguni, nyakati na mitindo ya mashauriana na ya washiriki yatofautiana. Kwa ujumla imerekodiwa furaha na shauku katika nchi za Bara la Afrika, Amerika Kusini na Asia na kila mahali kwa ujumla wamepongeza hatua ya kusikiliza kwa Watu wa Mungu ambapo uiaendelea hadi mwezi Agosti 2022 na sio tena mwezi Aprili kama ilivyokuwa imetabiriwa mwanzoni.

Changamoto ya lugha kwa ajili ya kuenezwa Hati ya Sinodi Ulimwenguni

Takwimu nyingine zinatazama kueneza Hati  ya Sinodi ulimwenguni na sehemu ya  kiekumene na kidini. Kila mara kwa mujibu wa Baraza, la sekretarieti ya Sinodi ni kwamba, imetafsiriwa kwa matatizo makubwa hasa mahali ambapo kuna lugha nyingi katika Nchi. Shauku na tamanio la kutoa mchango katika mchakato katoliki umerekodiwa na madhehebu mengine ya kikristo wakati eneo la kidini, linaonekana kuwa dogo mahali ambapo wakristo ni wachache, lakini hata katika kesi hiyo kwa mujibu wa Baraza, kuna matarajio ya kutoa mchango wa maana kubwa.

Tovuti na mitandao ya kijamii kueleza kinachoendelea

Hata kwa upande wa mawasiliano yametoa nafasi muhimu kwa kuanzishwa mchakato wa kisinodi. Katika majimbo mengi na mabaraza ya maaskofu zimeibuka web na kurasa kwenye mitandao ya kijamii, ili kusimulia kile ambacho kinatukia kwa ngazi mahalia. Na zaidi kuna nafasi rasimi katika tovuti ya kitaasisi: synod.va, ambazo zinakaribisha uzoefu na rasilimali zilizotoka kwa ngazi mahalia (synodresources.org), na tovuti  ya sala kwa ajili ya sinodi(prayforthesynod.va) ambayo iliandaliwa pamoja na Mtandao wa Kimataifa ya wa sala ya Papa na Umoja wa Kimataifa wa Wakuu wa Mashirika.

Mchakato wa sinodi pia unaonesha baadhi ya changamoto zinazojitokeza

Katikawakati muhimu kama ule wa Sinodi, shauku na mvuto unaambatana na changamoto ambazo Baraza linaangazia na matatizo ambayo hayafichiki. Ni suala la woga na utulivu kati ya waamini na mapadre, lakini pia kutokuaminiana kati ya walei ambao wana shaka kwamba mchango wao utazingatiwa kweli, au kuna vikwazo vinavyoletwa na janga ambalo litafanya liwe vigumu kusikiliza na kuwasiliana moja kwa moja kati ya watu. Mchakato wa sinodi pia unaonesha baadhi ya changamoto zinazojitokeza mara kwa mara kwa mujibu wa maelezo ya Baraza katika tamko lao kama vile haja ya kuwa na malezi, hasa katika kusikiliza na kupambanua, hatari ya kujitegemea katika mikutano ya kikundi, haja ya kuboresha ushiriki wa vijana; ushirikishwaji wa wale wanaoishi pembezoni mwa taasisi za kikanisa na hatimaye, hali ya kukosa mwelekeo iliyooneshwa na baadhi ya mapadre.

Mchakato wa Sinodi uendelee hata zaidi ya hapo

Kwa kumalizia Baraza linaelezea, kutokuwa na uhakika kunaojitokeza, pamoja na nguvu, lazima kushughulikiwa. Mchakato wa uongofu  wa sinodi utakuwa mchakato mrefu na utahitaji muda zaidi kuliko mchakato wenyewe. Pendekezo ni kwamba njia katika ngazi mahalia  iendelee katika mchakato mzima na hata baada ya hapo, ili jumuiya ya kikanisa iweze kuzidi kufanya sinodi ionekane kama mwelekeo msingi wa Kanisa. Wakati huo huo, Dokezo linatolewa kusaidia majimbo  na vituo vya emabaraza ya maaskofu kufafanua ripoti kamilifu. Jambo limependekezwa wazo kwamba utayarishaji wa ripoti yenyewe ni kitendo cha utambuzi, ambacho ni kusema tunda la kiroho, la mchakato na kazi ya pamoja.

07 February 2022, 12:33