Tafuta

2022.02.08 Papa Mstaafu Benedikto XVI 2022.02.08 Papa Mstaafu Benedikto XVI  

Nyanyaso Ratzinger:Aibu,uchungu na ombi la dhati la msamaha

Katika barua kwa waamini wa Munich,Papa Mstaabu anazungumzia juu ya nyanyaso za Makleri kwa kutumia maneno ya “mea maxima culpa”aliyorudia katika Misa:aiai wennye tunaburuzwa katika makosa makubwa sana ikiwa hatukabiliani na ulazima wa maamuzi na uwajibikaji”.

VATICAN NEWS

Papa mstaafu Benedikto XVI ameingilia kati, mwenyewe moja kwa moja ili kutoa neno lake kuhusu ripoti ya nyanyaso katika jimbo la Munich - Freising mahali ambapo yeye aliwahi kuwa Askofu Mkuu kwa karibia miaka mitano hivi. Anafanya hivyo katika barua inayoonesha ladha ya kujiweka katika nafsi ya kuungama na kuonesha uchungu kwa sababu ya nyanyaso na makosa ambayo yalithibitisha wakati wa kipindi chake akiwa katika maeneo hayo. Katika sehemu ya kwanza ya barua ya Ratzinger anaandika kuhusu alivyoishi “siku za kutafakari dhamiri na tafakari”, mara tu baada ya kuchapishwa kwa ripoti. Anashukuru ukaribu ambaoumeoneshwana wengi. Anamshukuru yule aliyeshiriki na yeye kutazama pamoja zana za hati na kuandaa majibu yaliyotumwa katika Tume. Na kama alivyokuwa tayari amefanya, siku zilizopita anaomba tena msamaha wa makosa ambayo hayakukusudiwa wakati wa uwepo wake kwenye mkutano wa tarehe 15 Januari 1980, wakati walipoamua kumkaribisha katika jimbo lake padre mmoja aliyekuwa anapata matibabu. Na anasema kwamba  kwa namna ya pekee anashukuru imani na msaada wa sala ya Papa Francisko aliyomwelekeza yeye binafsi.

Katika sehemu ya pili ya barua hiyo, Papa Mstaafu anaeleza alivyoshaangazwa“kila siku Kanisa kuweka katikati ya kila aina ya maadhimisho ya misa, ya kuungama dhambi zetu na kuomba msamaha. Tuombe Mungu aliye hai hadharani ili kusamehe dhambi zetu, dhambi yetu kubwa”. PapaMstaafu anaendelea kueleza kuwa ni wazi neno kubwa, ni hali yenye  maana moja ya kila siku, ambayo anajiuliza ikiwa hata leo hii hapaswi kuzungumza kosa kubwa. Na anaamini kwamba hata ikiwa dhambi ni kubwa kiasi gani, Bwana anamsamehe ikiwa yeye ana uwezo wa kuacha ang’utwe na Yeye na pia akiwa tayari kwa dhati kubadilika binafsi. Joseph Ratzinger kwa maana hiyo anakumbuka mazungumzo ya moja kwa moja na waathirika wa nyanyaso walizofanya makleri. “Katika mikutano yangu yote hasa wakati wa ziara za kitume na waathirika wa nyanyazo za kijinsia, kwa upande wa mapadre, niliwatazama kwenye macho na matokeo ya kosa kubwana lilijifunza kujua kuwa sisi wenyewe tunakuja kubuluzwa ndani ya kosa kubwa ikiwa tunadharau au hatukabiliani nalo na ulazima wa kufanya maamuzi na uwajibikaji, na kamakwa bahati mbaya ilivyotokea na inatokea”.

Papa Mstaafu anandika tena kuwa “Kama ilivyokuwa mikutano hiyo kwa mara nyingine tena ninaweza kuelezea tu mbele ya waathirika wote wa nyanyaso za kijinsia aibu yangu ya kina na uchungu wangu mkubwa na ombi langu la wazi la msamaha. Nilipata uwajibikaji mkubwa katika Kanisa Katoliki. Na uchungu wangu zaidi ni kwa ajili ya nyanyaso na makosa ambayo yamethibitishwa katika kipindi changu nilichokuwa katika maeneo hayo. Kila kesi binafsi ya nyanyaso za kijinsia ni la kutisha na lisilosemekana. Kwa waathirika wa nyanyaso, ninawaonea huruma ya kina na kulalamika kwa kila kesi binafsi”. Papa Mstaafu Benedikto XVI anasema kwa maana hiyo ya kuelewa daima zaidi karaha na hofu ambazo Kristo alifanya uzoefu katika Mlima wa mizeituni alipoona kila kitu kinakuwa cha kutisha na wakati angeweza kwa dhati kukizuia. Katika wakati huo, mitume waliokuwa wamelala, amesema wanawakilisha kwa bahati mbaya hali halisi ambazo hata leo hii zinaonekana kwa upya na ambazo "mimi ninahisi kuwemo. Kwa maana hiyo kinachobaki ninaweza kusali tu kwa Bwana na malaika wote na watakatifu na ninyi wapendwa kaka na dada ili msali kwa ajili yangu kwa Bwana Mungu wetu”.

Papa Mstaafu abahitimisha barua yake kwa maneno haya: “Hivi karibuni nitakuwa mbele ya mwamuzi mkuu wa maisha yangu. Hata kama katika kutazama nyumba ya maisha yangu marefu ninaweza kuwa na hofu  na woga mwingi, lakini  bado nina moyo wa furaha kwa sababu ninaamini kabisa kwamba Bwana sio tu hakimu sahihi, lakini wakati huo huo rafiki na ndugu ambaye tayari yeye mwenyewe ameteseka kutokana na mapungufu yangu na kwa hiyo, kama hakimu, wakati huo huo ni mtetezi wangu(Paraclete). Kwa kuzingatia saa ya hukumu, neema ya kuwa Mkristo inakuwa wazi kwangu. Kuwa Mkristo kunanipa maarifa, zaidi ya hayo, urafiki na mwamuzi wa maisha yangu na kuniruhusu kuvuka kwa ujasiri mlango wa giza wa kifo" .

Pamoja na barua ya Papa Mstasfu Benedikto XVI imechapisha hata kurasa tatu zilizoaririwa na wahudumu wanne, wataalam wa sheria: Stefan Mückl, Helmuth Pree, Stefan Korta na Carsten Brennecke, ambao tayari walikuwa wamehusika katika kuandaa kurasa 82 za jibu la swali la Tume. Majibu yake yaliyoambatanishwa na ripoti juu ya nyanyaso za Munich, yalikuwa  yameibua mkanganiko wa maoni na kulikuwa na makosa kiuandishi ambao ulipelekea kuthibitishwa ukosefu wa Askofu Mkuu Ratzinger katika Mkutano ambao ulitoa maamuzi ya kumpokea kuhani aliyekuwa amechafuliwa na nyanyaso. Katika majibu mapya, wataalam wanabainisha kuwa Kardinali Ratzinger, katika wakati huo alipompomaribisha kuhani ambaye alikuwa atibiwe Munich, alikuwa hana utambuzi kwamba alikuwa amenyanyaswa. Na katika mkutano wa Januari 1980 hapakuwa pemetajwa sababu ambazo zilipelekea kutibiwa na wala maamuzi ya kumfanya awe katika shughuli za kichungaji. Hati inathibitisha kile ambacho kilithibitishwa na Ratzinger.

Katika taarifa hiyo wanaelezea kwa kinagaubaga kwa nini makosa hayo mwanzoni yalikataliwa na Ratzinger: Profesa Mückl pekee ndiye aliyeruhusiwa kutazama hati katika toleo la kielektroniki, bila kupewa uwezekano wa kuhifadhi, kuchapisha au kunakili hati. Katika awamu iliyofuata ya ufafanuzi, Dk. Korta bila kukusudia alifanya makosa ya unukuzi, akiamini kwamba Ratzinger hakuwepo 15 Januari  1980. Kwa hiyo, Papa Benedikto XVI hawezi kuhusishwa na hitilafu hii ya unukuzi kama uwekaji wa fahamu za uwongo au uongo". Hata hivyo tayari mnamo 2010 katika makala tofauti ya habari, hawakuwahi kukataa kuzungumza juu ya uwepo wa Ratzinger katika mkutano huo, na Papa mstaafu mwenyewe katika wasifu wake ulioandaliwa na Peter Seewald na kuchapishwa mnamo 2020, anathibitisha uwepo wake. Wataalam wanathibishwa kuwa hakuna kesi iliyotathimini na ripoti kwamba Joseph Ratzinger alikuwa na utambuzi wa nyanyaso za kijinsia zilizofanywa au shaka juu ya nyanyaso za kijinsia zilizofanya na makuhani. Hati haionesha jaribio lolote kwa maana ya kinyume na matokeo kwa kujibu sahihi maswali juu ya hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika  kuwakilishi, na hata wawakili wenyewe ambao waliandika ripoti wamesema kwamba walidhani kwamba Ratzinger alijua, lakini bila uthibitisho wao huu kuthibitishwa na ushuhuda au hati.

Hatimaye, wataalamu wanakanusha kwamba katika majibu waliyoandika kwa niaba ya Papa Mstaafu uzito wa tabia ya maonesho ya kuhani ulipunguzwa. "Katika kumbukumbu yake, Papa Benedikto XVI hakupunguza tabia ya maonesho, lakini alilaani waziwazi. Maneno yanayotumiwa kama dhibitisho la madai ya kupunguzwa kwa maonesho hayana muktadha”. Katika majibu yake, Papa Mstaafu Benedikto XVI alisema kuwa nyanyaso, ikiwa ni pamoja na maonesho, ni ya kutisha, dhambi", ya kulaumiwa kiadili na haiwezi kurekebishwa. Katika tathmini ya wataalam ilikumbukwa tu kwamba kwa mujibu wa sheria iliyokuwa ikitumika wakati huo, maonesho hayakuwa uhalifu chini ya sheria ya kanoni, kwa sababu sheria ya jinai inayohusiana haikujumuisha tabia za aina hiyo katika kesi hii”.

Kiambatisho kilichotiwa saini na washiriki wanne ambao ni wataalam wa sheria, ambao Papa Mstaafu amejitwika jukumu la kazi yao, inachangia kufafanua kile kilichotokea katika akili na moyo wa Ratzinger, na ni matokeo ya utafiti wa washirika wake. Papa Mstaafu Benedikto wa kumi na sita anakariri kwamba hakufahamu nyanyaso zilizofanywa na makuhani wakati wa uaskofu wake mfupi. Lakini kwa maneno ya unyenyekevu na ya kina ya Kikristo anaomba msamaha kwa hatia kubwa sana ya unyanyasaji na makosa, hata yale yaliyotokea wakati wa mamlaka yake.

08 February 2022, 16:11