Baba Mtakatifu Francisko akutana na kuzungumza na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko akutana na kuzungumza na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia mjini Vatican. 

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia Akutana na Papa Francisko

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Rais wa Zambia, wamezungumzia masuala ya kiuchumi na kijamii nchini Zambia sanjari na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Zambia katika ujumla wao. Wamegusia pia masuala chanjo ya UVIKO-19 na changamoto zake Barani Afrika pamoja na ushirikiano wa kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 19 Februari 2022 amekutana na kuzungumza na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia na ambaye baadaye amebahatika kukutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu mkuu msaidizi wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Rais wa Zambia, wamezungumzia masuala ya kiuchumi na kijamii nchini Zambia sanjari na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Zambia katika ujumla wao.

Papa Francisko akutana na kuzungumza na Rais wa Zambia.
Papa Francisko akutana na kuzungumza na Rais wa Zambia.

Baba Mtakatifu pamoja na Rais wa Zambia wameridhishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Vatican na Zambia. Wamezungumzia pia kuhusu chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 na changamoto zake Barani Afrika. Kwa pamoja wameonesha nia ya kutaka kuandika makubaliano ya pamoja kama alama ya ushirikiano unaosimikwa katika heshima. Mazungumzo yameendelea kwa viongzo hawa wawili kubadilishana mawazo katika masuala ya Kimataifa na Kikanda.

Papa Zambia

 

19 February 2022, 15:42