Shughuli za kidiplomasia za Vatican ni kitovu cha Mkutano wa Makardinali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Sinodi, huduma ya kidiplomasia ya Vatican na jukumu la mwanamke katika Kanisa, ndizo mada ambazo zimekabiliwa kwenye kikao cha mwisho cha Baraza la Makardinali na Papa Francisko ambaye aliunganika akiwa katika nyumba ya Mtakatifu Marta, Vatican kilichofanyika kwa siku ya tarehe 21-23 Februari 2022. Kwa mujibu wa msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, amebainisha jinsi mkutano huo walikuwapo Kardinali Parolin, Bertello, Maradiaga, Marx, O’Malley, Gracias, Besungu, pamoja na Katibu wa Baraza monsinyo Marco Mellino.
Sinodi ni mchakato wa usikivu
Kwa mujibu wa taarifa za mkutano, ulifunguliwa na mazungumzo mbali mbali ambapo Makardinali wameingilia kati kuelezea hali halisi za kijamii, kisiasa na kikanisa katika kanda zao wanazotokea; baadaye walitafakari juu ya kauli mbiu ya Sinodi kama mchakato wa kusikiliza na kung’amua katika moyo wa utambulisho wa Kanisa na ulazima wa kuwa na uongofu ambao unaombwa kila mkeli na walei.
Shughuli za mabalozi wa vatican katika hali halisi ya kisiasa
Baadaye kati ya mada nyingine zilizoguswa ni tafakari juu ya mantiki zinazohusiana na huduma ya kidiplomasia ya Vatican kwenye nchi mbali mbali, jukumu na shughuli za mabalozi katika mtazamo wa kisiasa na kikanisa. Wakiendelea katika mkutano wao zaidi, wajumbe wa Baraza la Makardinali, walisikiza na kutoa maoni ya hotuba ya mtaalimungu Sr. Linda Pocher, kuhusu jukumu la mwanamke na msingi wa Mama Maria katika Kanisa. Mkutano ulihimimishwa Jumatano 23 Frbruari jioni saa 11.30 ,wakati mkutano ujao unatarajiwa kufanyika mwezi wa nne mwaka huu. Mkutano uliopita ulikuwa umefanyika kati ya tarehe 13 na 14 Desemba 2021 na ulikuwa umejikita juu ya janga la uviko na maendeleo ya mchakato wa safari ya Sinodi.